Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

Mtoto aliyezaliwa mwaka 2004 wakati kaka Aikaeli anapewa cheo, kama ni wa kike basi kifua kimeshaota chuchu.

Anazungumziwa Mbowe kwa sababu ni kiongozi wa chama ambacho muda wowote kinaweza kuwa mbadala wa CCM.

Yaani ukiwepo upungufu wa maadili kwenye uongozi ndani ya CHADEMA, maana yake ni kwamba siku chama kikipewa ridhaa, upungufu huo utakuwa sehemu ya maadili mabovu ya kitaifa.

CHADEMA inatazamwa kitaifa zaidi ndio maana watu wanakuwa na ujasiri wa kuuliza mbona kaka anazeekea kwenye cheo.

CHADEMA haiwezi kusema kwamba yenyewe ni taasisi ambayo haina haki ya kujadiliwa, tukumbuke kuwa ruzuku wanayoipata ni kodi ya mwananchi wa kawaida, hivyo mwananchi anayo haki ya kuhoji mambo yanayoonekana kutoendana na hali halisi ya kisiasa.
 
M/kiti amekuwa mwiba kwa ccm, hawalali wanamuota Mbowe kuwa watamuondoaje Chadema, Mbowe amekuwa nguzo muhimu kwa chadema na mageuzi kwa ujumla hapa Tanzania, ccm Kama kawaida yao wamezoea siasa za mtelemko lkn kwa Mbowe wamechemka sasa kazi ni moja, propaganda za kumchafua Mbowe zinazoongozwa na chakubanga, sasa hivi ukimuliza chakubanga ccm ina wanachama wangapi yeye atakujibu Mbowe hafai kabisa, ni mbinafsi, yaani mzimu wa Mbowe ndani ya viunga vya lumumba unatembea, siajabu mtu akikurupushwa usingizini anaweza kumtaja Mbowe. Chaajabu ukikutana na watu wa lumumba kati ya viongozi wa vyama ni yupi kakaa mrefu wao watakimbilia kusema ni Mbowe, hebu tuangalie :-
1. Cuf - m/kiti wake yupo pale miaka mingapi?
2. UDP -
3. TLP -
4. UPDP -
Wote hawa hawajawahi kubadilishwa kwanini Mbowe? Kuna jambo, chadema kuweni makini na mkakati wa ccm. Tujiulize, kuna mtu anaruhusiwa kugombea uenyekiti wa ccm? Au kuhoji kofia mbili za uongozi wa kitaifa? Kama haiwezekani kwao, kwanini wahoji kwa wenzao?
 
Mtajua nyie wenyewe kama bado ni muhimu ama sio muhimu ila sie ni mbele kwa mbele
 
Prof Assad kasema Tanzania haihitaji viongozi wenye nguvu bali taasis imara.
 
Lwakatare, Komu, Kubenea na Lissu ni kundi hasi dhidi ya Mbowe ndani ya Chadema.
 
naona thread za team mbowe zinaendelea kumwagika tu hapa jukwaani, kunani hapo ufipa?!
 
Leo hiii ni haohao wanaotumia jeshi kumrudisha madarakani.hizi akili za jamaa sijui zikoje?,wao kwao mbowe ndo kakaa muda mrefuu kuliko lipumba.

Mbona hawazungumzii mihela ya ruzuku ya cuf wanayompa lipumba licha ya kua mahakama imezui?.au ile ya lipumba sio ruzuku?
 
Back
Top Bottom