Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

Hili jambo huwa silielewi kabisa. Kweli Mbowe kama binadamu ana madhaifu yake, lakini inakuwaje ni CCM ndiyo wanataka kuweka ukomo wa uenyekiti wa Mbowe CHADEMA?

Yaani ni kama Wamarekani waseme ni kwa nini wajerumani wanaendelea kumchagua Angela Merkel kuwa Kansela wao. CCM kuhusu Mwenyekiti wa Taifa hakuna mahali kwenye katiba yao pamewekwa ukomo wa muda, bali wanabadilishana kwa kutegemea "Tamaduni" ya chama hicho na wala si kwa uchaguzi kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho hakuna kugombea nafasi ya mwenyekiti Taifa.

Sasa chama ambacho huwa hakifanyi kabisa uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa, kinakuwaje na nguvu ya kimaadili kuwaambia CHADEMA wabadilishe Mwenyekiti wao Taifa? Kwani kwenye Katiba ya CHADEMA kuna kipengele kinakataza mtu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa zaidi ya mara moja?

Ni sawa na walivyouchoka uhai wa Lisu na wanaosemekana wako kwenye list!. CCM is an association of monsters!
 
Hili jambo huwa silielewi kabisa. Kweli Mbowe kama binadamu ana madhaifu yake, lakini inakuwaje ni CCM ndiyo wanataka kuweka ukomo wa uenyekiti wa Mbowe CHADEMA?

Yaani ni kama Wamarekani waseme ni kwa nini wajerumani wanaendelea kumchagua Angela Merkel kuwa Kansela wao. CCM kuhusu Mwenyekiti wa Taifa hakuna mahali kwenye katiba yao pamewekwa ukomo wa muda, bali wanabadilishana kwa kutegemea "Tamaduni" ya chama hicho na wala si kwa uchaguzi kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho hakuna kugombea nafasi ya mwenyekiti Taifa.

Sasa chama ambacho huwa hakifanyi kabisa uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa, kinakuwaje na nguvu ya kimaadili kuwaambia CHADEMA wabadilishe Mwenyekiti wao Taifa? Kwani kwenye Katiba ya CHADEMA kuna kipengele kinakataza mtu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa zaidi ya mara moja?
Angel Mikel alibadiri Katiba?
Udikteta ni kubadiri Katiba kuifanya iendane na Matakwa yako.
Kama chama kinatabia ya kubadirisha Katiba yake kikishika madaraka kitakua na Tabia hiyo hiyo ya hovyo.
Hoja kulikua na sababu gani ya kuondoa ukomo wa Mwenyeiti?
 
akifa na chadema inakufa, ha ha ha ha ha
Kweli eenh? Yaani kusema kwamba Barcelona wanamtegemea Messi kwenye ufungaji ndiyo inamaanisha kwamba Messi akistaafu kucheza mpira ndiyo Barcelona nayo itakuwa haifungi magoli kwa kuwa Messi kastaafu?

Kwa sasa Mbowe ndiye anayeifaa CHADEMA. Kwani na yeye mna lengo la kum- Pyu! Pyu?
 
Kama Chadema wanaona ni sawa kuongozwa na mwenyekiti huyohuyo miaka nenda rudi wanaonaje ajabu JPM akiongoza miaka saba saba.
Kuna tofauti kati ya utaratibu wa chama na katiba ya nchi, mwenyekiti wa chama na Rais wa nchi. Inawezekana tunachanganya kwa bahati mbaya au kutokujua ila ukivichanganya tu ndio mwanzo wa kuharibu/kuharibikiwa.
 
Hao miaka yote wako ivo, kwa sasa wanajidai kumpenda Dr.slaa na Lipumba. Hiv toka lini Panya akasifia uzuri wa Paka!!?
 
Ccm wenyewe wanahitaji kuwa na uoinzani imara wenye hoja ili hata siku wakiachia ngazi waache kwenye mikono salama.
Sasa wanashangaa wanapoona Mbowe anabeba makapi ya ccm kama Lowasa, Sumaye na Nyalandu alafu anawafanya kuwa top leader!

Hapo lazima wamuone Mbowe hajielewi,
 
Walionza kuuchoka uwenye kiti wa mbowe ni akina zito kabwe wakiwa ndani ya chadema lakini yakawakuta ya kuwakuta
 
Kwa rekodi alizoweka kama mwenyekiti wa CHADEMA tangu aliposhika hiyo nafasi hata ningekuwa mimi ndio kada wa CCM lazima ningeshabikia jamaa atoke. Maana gap la kura baina ya chama chake na CCM linazidi kupungua kila uchaguzi.
 
Ungewauliza kwanza Chadema na Mbowe wenu ambao kila siku hakuchi bila kuisema CCM utadhani wao ni wanachama wa CCM
Ccm lazima isemwe, kwani kazi ya upinzani ni nini??
Utakuwa huna kitu kichwani wewe, siyo bure!
 
Kwa sababu wameshindwa kupenyeza vikaragosi vyao ndani ya Chadema hilo linawakosesha sana usingizi. Mbowe ni shujaa kwa kweli.

Hili jambo huwa silielewi kabisa. Kweli Mbowe kama binadamu ana madhaifu yake, lakini inakuwaje ni CCM ndiyo wanataka kuweka ukomo wa uenyekiti wa Mbowe CHADEMA?

Yaani ni kama Wamarekani waseme ni kwa nini wajerumani wanaendelea kumchagua Angela Merkel kuwa Kansela wao. CCM kuhusu Mwenyekiti wa Taifa hakuna mahali kwenye katiba yao pamewekwa ukomo wa muda, bali wanabadilishana kwa kutegemea "Tamaduni" ya chama hicho na wala si kwa uchaguzi kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho hakuna kugombea nafasi ya mwenyekiti Taifa.

Sasa chama ambacho huwa hakifanyi kabisa uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa, kinakuwaje na nguvu ya kimaadili kuwaambia CHADEMA wabadilishe Mwenyekiti wao Taifa? Kwani kwenye Katiba ya CHADEMA kuna kipengele kinakataza mtu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa zaidi ya mara moja?
 
Lumumba huwa mnachekesha sana yaani Lumumba akili zao walishazijamba chooni. Ulishaona wapi adui anakushauri aina ya siraha na mbinu za kutumia wakati wa vita?
 
Lengo la CCM na serikali ni kuona Chadema ikipata mwenyekiti dhaifu dizaini ya kina Lipumba, Cheyo, Mrema na mama Mgwhira ili wapate chance ya kukisambaratisha.

Mbowe ana msimamo, ni mpinzani halisi, kimsimamo hana tofauti na Seif. Ana hekima, ana busara hakurupuki anajua nini chama chake na wafuasi wake wanataka, hana jaziba wala visasi kama mwenyekiti wa upande wa pili. Kuongezea hapo Mbowe hana njaa za kijinga ana biashara zake, hanunuliki. Wamejaribu kuharibu mali zake wakafikiri atalegeza msimamo, TRA wamembambikia kodi kalipa, NHC wamebomoa Bilicanas wakafikiri ndiyo biashara yake pekee.

Mbowe sio Mrema wa kudanganywa kwa cheo mbuzi, kwa Mbowe CCM watakesha sana na naomba wajumbe wa mkutano mkuu wa Chadema uchaguzi utakapofika wamchague tena kwa kura zaidi ya alizopata tuwashangaze mahasimu wake.
Na juzi kawaambia kwenye kampeni ya udiwani kuwa Chadema haiwezi kufa yeye akiwa hai eitha ni mwenyekiti au sio mwenyekiti. Hiyo ni kauli ya jabali
 
Back
Top Bottom