Bulamba
JF-Expert Member
- Sep 17, 2011
- 13,645
- 12,935
Hoja kubwa uliyojenga ni kuwa hatuna uwezo wa kujitegemea na mazungumzo mengi yafanyike baina ya wahisani , CUF na CCM ili kunusuru dhahama.Mkuu analysis yako ni nzuri lakini ujue kuwa mikwara wanayoweza kutuwekea Marekani (MCC) sio tu msaada wao au ushawishi wao mkubwa kwa nchi za magharibi kuondoa misaada yao, la hasha. Hata kama tungekuwa na budget surplus - yaani matumizi yetu ni trilion 22 na mapato yetu (TRA tu) ni trillion 50 - lakini Marekani wakitaka kutuzamisha wanaweza. Wanaweza kusema
Ona walichofanya/wanachofanya URUSI, IRAN, N. KOREA, IRAQ (enzi za Saddam), LIBYA (enzi za QADDAFI).
- tusitumie soko lao la US-Dollar, au
- tusitumie mtandao wao wa malipo wa SWIFT, au wakasema
- mabenki yetu yasifanye biashara zao na mabenki makubwa (wanayoyamiliki) ya dunia.
Wamarekani ni jeuri, wana kiburi, na hawapendi kudharauliwa hata kama wao ndio wenye makosa (na mara nyingi ndio hivyo). Kwa hapa Magufuli anapaswa kutumia diplomasia zaidi kuliko ubabe. Akitumia ubabe atakwenda na maji.
SASA TUFANYEJE?
1. Sheria za mitandao: Hapa ndipo pa rahisi pa kujikwamulia napo. Hii sheria inaweza ikabadilishwa bila kuathiri usalama wa nchi. Ilifanya kazi yake vizuri kuwadhibiti waliotaka kuchezea uchaguzi wa 2015 na sasa serikali ya Magufuli inaweza kukaa mezani na wafadhili, na kwa kupitia bunge, kutafuta muafaka. Hapa Tanzania itaonekana inawajibika (kama mnyonge) kwa mataifa huru duniani. Marekani watajisikia wameshinda, (save face) na kuwa wamesikilizwa. Hii ni muhimu sana. Safari ya maendeleo ya Tanzania ni ndefu sana. Tusianze kuchoma madaraja. Wapeni sheria ya mitandao kama kafara ili tung'ang'ane na mazito yajayo.
2. Uchaguzi wa marudio Zanzibar: Tanzania lazima iwatanabaishe wadau wa nchi za nje kuhusu red-lines zake. Kulikuwa na mtafaruku kati ya ZEC na CUF katika uchaguzi wa nchi ya Zanzibar Oktoba 2015. ZEC (tume huru ya uchaguzi Zanzibar) ingeweza kumtangaza mshindi kipindi kile (kati ya Maalim au Dr. Shein). Chochote kati ya hivi viwili kingefanyika ZEC ingelaumiwa na upande mwengine kuwa DEMOKRASIA imekiukwa. Walichofanya ZEC ni kusema kuwa haitampendelea yeyote yule bali kurudia uchaguzi. Hiki kilichofanywa na ZEC ndio kitendo cha DEMOKRASIA. Waliamua kurudi kwa wananchi watoe uamuzi wao bila ya mauzauza yale ya Oktoba, 2015. CUF waliamua kutoshiriki huu uchaguzi (ambacho pia ni kitendo cha DEMOKRASIA) na uchaguzi ukaendelea. Kwa sasa Zanzibar inasubiri 2020 kufanya tena maamuzi yao ya kidemokrasia. Kuibatilisha serikali mpya ya Zanzibar kwa shinikizo la mtu yeyote yule ni ukiukwaji wa misingi ya kidemokrasia.
Kama kususia uchaguzi kwa CUF kutailazimisha Zanzibar ipangue serikali yake mpya basi hii italeta precedence mbaya kuwa chama chochote kile cha siasa kikiona hakina muelekeo wa kushinda, basi kitasusia uchaguzi halafu baada ya uchaguzi wataiangalia Marekani iingilie kati. Hii haitakuwa demokrasia tena bali kero tu.
Uchaguzi wa Machi 20 umekwisha na Zanzibar ina serikali kamili kwa mujibu wa sheria za nchi ya Zanzibar. Kilichobaki sasa ni:
- Upinzani wajipange upya kwa uchaguzi wa 2020
- Katiba ya Zanzibar (na ya muungano pia) irekebishwe kudhibiti mapungifu (ikiwa ni pamoja na tume huru ya uchaguzi - ZEC).
- Maalim na vigogo wa vyama vya upinzani wapatiwe nafasi za maamuzi katika serikali ya Dr. Shein ili maoni ya wafuasi wao yashughulikiwe na serikali katika kipindi hiki mpaka 2020 (rai).