Ikiwa mtu hayuko pensionable, haya mashirika ya hifadhi ya jamii yanakuwa na uhalali gani wa kushikiria hela za mwanachama?

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,919
2,199
Tuliambiwa kuwa mashirika ya hifadhi ya jamii yataunganishwa lakini mpaka sasa Jambo Hilo halijafanyika.kila shirika linajiendesha kivyake. Jambo hili mimi naona limeleta usumbufu mkubwa. Ili mtu aweze kupata mafao ya kustaff anatakiwa awe amechangia miaka 15 .

Tangia 2019 tuliambiwa kuwa mashirika hayo yataunganishwa .Hivyo watu wengi michango yao ikaanza kupelekwa NSSF. Kwa mfano Michango ya mtu ilikuwa ikipelekwa PPF na mtu amechangia Miaka mitano tu ( i e is not pensionable) baada ya 2019 michango yake sasa inapelekwa NSSF ambapo kama atafikisha miaka kumi na mitano hapo ndipo atapata pensheni yake.

Mtu huyu akienda PPF ambao iko chini ya PSSSF kuomba michango yake ihamishiwe NSSF wanakataa,ukiwaambia nipeni basi hela zangu Nako wanakataa.sasa sijajua Wana uhalali gani kisheria kukaa na michango ya mtu wakati hatakuja kupata pension kutoka kwao!! Naombeni mnisidie kuelewa.
 
Back
Top Bottom