Idd Amin Dada

f44f1257806bddcebca76f046fd231a7.jpg

Huyu jamaa alikuwa jasiri kwa kweli alingekuwa hadi leo mambo yangelikwenda vizuri.
But shuleni alipewa majina mabaya sana while katenda mambo mazuri sana hakuna mfano wake.
Wazungu wanamsemo wao wanasema"If you want to kill a dog just give a bad name'
Ndo walivyofanya kwa mtu makini na mwema (IDD AMINI DADA)
 
nmecheka sana utadhan mstaafu wetu yule alikuwa naye yupo kwa vyeo prof..dr..mtukufu.......
usifananishe watu wetu na huyo iddi amini, acha matusi ya nguoni

sisi wa kwetu tittle zote alizonazo kapewa, kazipata kwa njia zinazoeleweka, na hayo maneno kama mtukufu, hicho si cheo ni neno tu la heshima ambalo baadhi ya watu hulitumia, nalo hakujipachika mwenyewe ni watu wenyewe kwa matakwa yao walimuita iwe kwa unafiki, heshima ama shobo walizokuwa nazo juu yake

so please stop disrespecting
 
aah,hiyo hapo juu,huyo alieitoa angejua nilihenyeka kuipata?
Watu tunaweka kumbukumbu sawa,wengine wanaingiza ukereketwa wa imani humu
hasaaa wakati kupitia aina ya maisha aliyoishi yeye na familia yake kama ioneshavywo kwenye dokumentari zake huyu amini huyu hakuwa mtu aliefuata saana imani yake
 
wao ndo walimweka baada ya kumsaidia silaha na kutrain kikosi kilichompindua obote,walikuja kukosana baada ya amin kuwaomba israel fighter jet ili kuishambulia Tanzania kwani amin alisikia obote anaanda majeshi ya kumpiga kutokea Tanzania,waisrael wakawa wanakuwa wazito kumpa,ghadaf akaona chance ya kuvunja urafiki kati ya idd amin na israel kwani lengo la waisrael ilikuwa kupitisha silaha uganda kwenda sudan kulikokuwa na waasi wa anyanya wakipigana na waarabu wa sudan.
Ghadaf akawa kakubali kumpa amin ndege za kijeshi,hapohapo amin akageukia kusupport wapalestina na akawa adui wa israel
uwe unaweka source ya taarifa zako, maana zinavutiakuaminika, tatizo usije aminisha vitu visivyowahi kujiri kwa mlolongo unaouelezea
 
Ivi,ile movie ya idi amini yale matukio yote yalirekodiwa au kuna mtu ambae ameicheza kama id amin?
 
Huyu jamaa alikuwa na tabia za kushangaza sana eti alikuwa mchangamfu lakini mwenye kuweza kukasirika kwa ghafla sana. Inashangaza sana:rolleyes::rolleyes:
 
Alivyojiita...

His Excellency President for Life Field Marshal Al Hadj Doctor Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Sea and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular...

Operation yake ya kuwafukuza Wahindi na kuwagawia washikaji wake biashara, majumba na mali zao ilijulikana kama Operation Mafuta Mingi, OMM!
Mimi ninachoelewa ni kwamba hiyo Operation Mafuta Mingi haikuhusu kuwafukuza wahindi Uganda ila operation iliyoitwa kwa jina hilo ilikuwa ni ya kumpindua kijeshi Idd Amin mwaka 1977 na iliongozwa na Maj. somebody Kimumwe.
 
Huyu jamaa alikuwa na tabia za kushangaza sana eti alikuwa mchangamfu lakini mwenye kuweza kukasirika kwa ghafla sana. Inashangaza sana:rolleyes::rolleyes:
Alikua na uwezo wa kukuchekea na kukuua katika mida wa dakika 60
 
Mimi ninachoelewa ni kwamba hiyo Operation Mafuta Mingi haikuhusu kuwafukuza wahindi Uganda ila operation iliyoitwa kwa jina hilo ilikuwa ni ya kumpindua kijeshi Idd Amin mwaka 1977 na iliongozwa na Maj. somebody Kimumwe.
Hapana, si kweli, umekosea...operation mafuta mingi ilikuwa ni matokeo ya vita ya kiuchumi iliyoondoa uchumi mikononi mwa Waasia na kuuweka mikononi mwa Waganda, hebu soma hapa chini...

Transferring businesses from Asians to Ugandans created a new class of wealthy Ugandans known as the Mafuta Mingi (literally translated as “too much fat”). These are people who rose from rags to riches. They were mostly Muslims who had been recipients of departed Asians’ properties.

They lived within their acquired shops while some - as they made more money - had a chain of women in different homes. Besides a few Baganda, the majority were either Nubians or Kakwa’s.

Nadhani utakuwa umenielewa Nyaka-One!
 
Nimekuelewa kiongozi. Basi kama ndiyo hivyo serikali au wananchi waliita huo mchakato wa kuwatajirisha waganda wachache kwa mali ambayo hawakuitolea jasho kwa jina la Operation Mafuta Mingi lakini pia muda mfupi baada ya hao waganda kumilikishwa biashara hizo na wanajeshi nao wakiongozwa na Maj. Kamumwe wakawa na mpango wao wa siri wa kumpindua kijeshi Idd Amin ambao waliupa jina hilo hilo.
 
Bila shaka unamuongelea Maj. Patrick Malati Kimumwe na kweli alijaribu kuongoza maasi dhidi ya Idi Amin mwaka 1977 ambayo hayakufanikiwa na wakakamatwa ila nakiri sina hakika kama hiyo operation iliitwa mafuta mingi. Pamoja na hilo vita ya kiuchumi aliyoianzisha Idi Amin alipoamua kuwafukuza Waasia Uganda ilikuja kujulikana kama Operation Mafuta Mingi!

Nyakati hizo watu walivamia tu maduka ya Wahindi na kudai wapewe funguo za duka, wengine walisimamisha magari na kudai wapewe funguo na wengine walivamia makazi na kuwatimua walioishi humo...ole wako ukatae. Waasia wengi waliishia kukimbilia Airport ya Entebbe na huko walipiga kambi wakisubiri ndege za kuwatoa nchini Uganda. Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwao kwani wapo waliolala hapo hata mwezi mzima.
 
Back
Top Bottom