Huu mradi wa maji unaofanyika katika mji wa Arusha imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi.

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
2,091
3,746
Hapo vip!!
Kwanza ni kiri yakwamba mradi kama wa maji ni alama ya maendeleo katika jamii na hakuna asiyependa maendelelo

Lakini pale ule mradi unapogeuka kuwa kero na kizuizi cha maendeleo mengine hilo linakuwa mradi wenye maendeleo lakini wenye maadhara hasi kwa jamii inayoizunguka mradi huo.

Moja kwa moja ipo hivi..huu mradi waji kutoka katika wilaya ya Arumeru mashariki kwa namna moja au nyingine imegeuka kuwa kero kubwa kwa wananchi kwa namna hii:-

Kwanza wamekuwa na tabia ya kuchimba mashimo na motaro mikuwa katika eneo la Ngulelo Arusha.

Ipo hivi uchimbaji wa haya mashimo haifanyiki kwa mara moja ila wanaweza kuchimba na kufukia mashimo na mitaro na baada ya wiki moja wanarudi na kuchimba tena...zoezi hili linaweza kufanyika zaidi ya mara saba katika eneo husika pasipo kujali wananchi wa maeneo hayo wanaumia kichumi kiasi gani..

Kero ambazo zinawakabili wananchi ni kufungwa kwa barabara zaidi ya week mojo..sasa imagine warudie hilo zoezi zaidi ya mara saba kuchimba pale pale.

Wananchi kuangukia kwenye yalebmashimo mara kwa mara na kuvunjika miguu.

Wananchi waliopo pembezoni mwa mradi ule kufunga maduka na kushindwa kufanya biashara.

Swali la kujiuliza je hawa wachina wanopewa hizi tenda ni wanafunzi wa kichina wanaokuja kujifunza huku kwetu au kuna maslahi katika ucheleweshaji wa mradi huu.
 
Back
Top Bottom