Hotuba ya Tundu Lissu kwa Taifa yasubiriwa kwa hamu kubwa na Wananchi, Matumaini yatawala, Wachache waingiwa hofu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
127,959
244,559
Kwa mara ya Kwanza tangu Uhuru wa Tanganyika, Nimeshuhudia watu wengi wakihangaika huku na kule ili kukamilisha kazi zao mapema kwa lengo la kuwahi Hotuba ya kiongozi wa Upinzani.

Maofisi ya Serikali ndio yanayoongoza kuhangaika huku baadhi ya Wafanyakazi wakipanga kutoroka ili kuwahi Hotuba hiyo inayotajwa kutoa Mwongozo na Dira ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania.

Pamoja na Msisimko huo lakini lipo kundi dogo miongoni mwa Wananchi lililojawa hofu na wasiwasi kuhusiana na kitakachozungumzwa, Uchunguzi wetu umebaini kwamba kundi hilo dogo ni pamoja na familia za viongozi wakiwemo na Mashemeji zao walioko mkabala na Chawa wao, Bali haijajulikana hofu yao hiyo inatokana na nini.

Ngoja Tusubiri saa 10 jioni kwa saa za Nchini Tanzania.

 
Ataunguruma kupitia redio gani mkuu?
 
Nishaanza kupata hofu na mimi. Maana inavuma sana
 
Saa 10 kamili nitaacha kazi zangu zote za Matunguli Nimsikilizw Rais wa JMT nje ya Ikulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…