Hoteli ya JB Belmont yafungwa rasmi kutokana na ukata

HATA MAX BAR ILIYOPO ILALA BUNGONI / IMEFUNGWA RASMI/ REASON / HAKUNA BIASHARA / MAMLAKA ZA SEREKALI KUTOTAMBUA KUSHUKA KWA BIASHARA.
**natabiri BIASHARA nyingi zaidi kufungwa.
 
Weka picha na wewe!!!!

slide01.jpg
 
Nilipita pale nikakuta kikaratasi kikionyesha kuwa imefungwa. Ndugu zanguni mikutano mingi likyokuwa inafanywa kwenye hizi hoteli kubwa ilikuwa ya taasisi, idara, miradi na programu za serikali. Rais alipotamka kuwa hakuna mikutano kufanyika kwenye mahoteli na badala yake ifanyike kwenye premises za serikali hali ya biashara ya hotel nyingi iligeuka ghafla kuwa mbaya. Si hii tu bali kuna uwezekano wa hoteli nyingi kubwa zikakosa mapato zikabakia na mapato ya accommodation tu.
Hii ina repercursion kwenye mapato ya TRA ingawaje serikali haijagundua hilo. Matamko ya rais yataendelea kuleta negative impact kwenye mambo mengi kwa sababu utafiti haukufanywa kabla ya kutoa matamko
Kichwa maji! Hivi walikuwa hawana mbinu nyingine ya kupata wateja mpaka wategemee mikutano ya watumishi wa serikali? Yani serikali iendelee kuteketeza pesa kisa kulinda hotel za watu?
Wacha wazifunge!
 
iko hivi, pesa za kuendeshea mikutano na semina zilikua zinatokana na kodi iliyotokana na makusanyo mbalimbali yakiwemo maduhuli, matumizi hayo yalisababisha bajeti ya uendeeshaji iwe kubwa kuliko ya maendeleo, serikali imeamua kubana matumizi hayo ili kusaidia upatikanaji wa bajeti ya maendeleo ambayo itafikia asilimia 40% ......bajeti tegemezi si jambo zuri hivyo nadhani tuunge mkono nia njema ya serikali ya kubana matumizi katika bajeti ya uendeshaji ama matumizi ya kawaida ili kusaidi kwenye bajeti ya maendeleo ambayo itainua sekta kuu za uchumi ikiwemo miundo mbinu .si vyema kushadadia kila jambo bila uchambuzi yakinifu
 
Alivyofariki Mzee Justus Baguma Jb usimamizi haukua mzuri na waliokua karibu yake ki ofisi wakapiga pesa ndefu lwa maana ni wao tu walibaki na siri ya pesa familia ya marehemu waliishi London ambako marehem alipokua ame base kwa miaka mingi baada ya kukimbia uganda,kwa faida ya wengi na ieleweke mzee aliwahi kua mmoja w walinzi wa idd amin dada,mzee alichomoka uganda kabla ya vita.
 
Wewe ndio umeona leo hii hotel kitambo sana imefungwa sema wewe umekuja leo kutoka kijijini kwenu na umekuja umekariri
 
JB Belmont iliyokuwa Benjamin Mkapa tower ilifungwa tokea 2015.
Nafikiri baada ya mmiliki kufa biashara ziliyumba. Sisi si Wahindi, sisi ni
Waswahili (japo alikuwa Mganda) biashara zetu "magumashi" na usiri mwingi. Ukifa na biashara inayumba.

Nawasifu Wahindi kwa ku-keep legacy za Wazazi wao hata kama kwenye biashara zao kuna uchafu.
Unakakuta kabinti ka kihindi chini ya maika 20 dukani, namna anavyoongea na Mteja kwa wale
Wakware wanafikiri kamawezimikia kumbe ni sales strategy.

Hawa wa kwetu "mshua" akiwa na pesa wanazunguka na bastola kwenye ma-club ya usiku na uzungu mwingii.
"Mshua" akifa ni hekaheka.
Ni kweli mkuu. Wahindi kwa hili wako vizuri. Nimesikiliza clip ya Mo Dewji akieleza namna alivyokuwa mdogo alikuwa hatanui kama watoto wengine. baba yake alimtaka awe ofisini pamoja naye. Alivyomuuliza kwa nini haendi na wenzie jibu la baba lilikuwa hao baba zao ni mawaziri, wabunge, au wenye nafasi kubwa serikalini lakini wewe baba yako ni mfanya biashara. Akamwuliza mbona sasa sifanyi kitu, akamwambia kaa tu uangalie. Sasa hivi Mo ameipaisha sana kampuni iliyokuwa ya baba yake kwa sababu kuhusishwa nayo tokea utoto. Isitoshe baba alimpeleka kwenye best schools, nadhani Harvard. Tatizo sisi waswahili kwanza watoto hawako interested na tunachofanya na sisi hatuwashurutishi kujifunza. Elimu ndiyo usiseme. Watoto wetu ndiyo hao vilaza aliowasema raisi wetu. So when we die the business dies too. Inabidi kwa hili tujifunze toka kwa wahindi. Tuwe wakali kwa watoto waache kutanua waumie na sisi.
 
WAcha wafunge tu, kwa maana hamna namna. Kama kasi ya kufungwa kwa biashara ikiwa hivi, sijui watakusanyaje Kodi?

Na hizo ajira ndo kwaheri.

Suppliers wote wanaopeleka vitu kwenye mahoteli nao watafunga biashara zao. Familia zao sijui zitakula wapi?

Hii ni MULTIPLIER EFFECT.
 
Back
Top Bottom