Hivi unakumbuka kwanini P Funk aliwahi mchapa vibao Afande Sele?

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,940
10,757
VISA na MIKASA
SIKU P FUNK alipomchapa Makofi AFANDE SELE…

1712604316251.jpg
Turudi nyuma kidogo,

Miaka zaidi ya 18 iliyopita na Ilikuwa ni kipindi kifupi tangu P funk aanze kufanya kazi na Afande. P anasema miezi kama miwili nyuma ya siku hiyo ya tukio alikuwa na Sele, alimpatia wimbo mmoja na sele akaahidi pesa ya wimbo huo angepeleka kesho lkn kesho yk Sele akajikataa kwao mji kasoro akimwacha P funk kaduwaa!!
Ikawa usiku ikawa mchana, hatimaye Afande akaibuka tena kwa P, safari hii alifata ngoma yk ingine akisema kwamba kesho yk alitaka aipeleke redio.

P akamwambia ngoma haijakamilika na asingeweza kuikamilisha kwa muda mfupi hivyo. afande akasema hiyo ngoma inabidi ima faima, P kuona hivyo akamwambia afande kavp ujaribu kesho lkn afande hakutaka kuelewa na akaanza kung’aka, “Brother ingekuwa nature hapo ungeshamrekebishia ila mimi ntazamie tena kesho, inakuwaje hii”. Ndiyo kilichotokea hapo siku hiyo na hatimaye Afande akaondoka na kuahidi angekuja tena kesho kufata kazi yake.

Keshoye sasa, baada ya uchovu wa kufanya kazi usiku P akiwa amejipumzisha, akasikia majibizano ya secretary wake kwa nje..baada ya kusikia kelele zinazidi ikabidi P aamke kwenda kuangalia kuna nini, ile kufungua mlango tu chumba kizima puyapuya, mimoshi ya bange hadi watu hawaonani,
P akauliza “Afande unafanya nini sasa? Hauoni tangazo hapo juu??

Afande akasema hii moshi ya dawa ya mbu braza(afande alikuwa amewasha dawa ya mbu kukata harufu) P akamaind sana ikambidi amfate afande na bila kutegemea akamnasa kofi moja la nguvu! maumivu ya kofi ukiongezea na stimu za bange afande akabaki anaona nyota nyota tu

P anasema ilikuwa ni tabia ya afande, akifika hapo studio kitu cha kwanza ni kugawa dawa kila mtu anaemkuta mjengoni hata ikabidi sasa waandike tangazo la kupiga stop uvutaji bange hapo na wakaweka kabisa Picha ya mfanano wa afande kuonesha msisitizo!!tangu siku hiyo afande akaacha tabia ya kwenda na dawa studio…anasema P funk.
 
P-Funk huwa hapendi upumbavu. Uzi mzuri huu, sasa tupe kisa cha Dudu baya kumtandika Mr. Nice, kisha ukitoka hicho utupe kisa cha Madee kutandikwa na wana HipHop
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom