Hivi ni kweli kuna baadhi ya wanawake wana nuksi?

Nimewahi kusikia kuhusu bunadamu wenye nuksi. Yaani ukijihusisha nao tu muda, you're ill fated iwe kibiashara, career, ama kimaisha.

Mfano mzuri ni Sean 'Diddy' Combs. Jamaa ukijihusisha nae kimuziki kwa muda, you're ill fated. Wengi wa wasanii waliowahi kuwa Bad Boyz(kama sio wote) ama kuwa karibu na Bad Boyz leo hii hawasomeki, aidha kimaisha, kibiashara au katika careers zao za muziki. Craig Mack (last I heard, Dude joined a cult). Biggie Smallz inajulikana kilimkuta kipi. Mase kajaribu 'ulokole', ila bado hajielewi. Loon, dah! Black Rob mpaka huruma. G-Dep yale yale. Kina Faith, Mario Winans, na wengine kibao wamezimika tu kiaina.

So yeah, inawezekana kuna binadamu wana mikosi ukijihusisha nao.
 
Sheikhe yahaya angekuwepo ningekuambia uwende lakini akija alibika kitu Nenda kwa ma shekhe ubwabwa kule zanziberi au tanga watakupa jibu na roho itapenda lakini humu watakuzinguwa !wallahi watakusahidia
 
Hili suala lina kiukweli

Nadhani kuna haja ya kuyafafanua kiundani mno...

Kama nuksi ni bahati mbaya inabidi tujiulize why lakini pia tuangalie kuwa hiyo bahati mbaya ina lengo gani .. Tuchukue hio nuksi kama namba ya mawasiliano ambayo yanatufahamisha kuwa uliye naye siye kama utagundua kuwa kikwazo ni pale ukijihusisha naye.

Na solutions ni kuachana naye tafuta mwingine kama hilo halifai na mshaingia kwenye ndoa basi jaribu kukutana na kiongozi wako wa dini na mwombe ushauri kuhusu hilo
 
inasemekana kila binadamu ana nyota, sasa nyota zenu zaweza kukinzana ama kuendana.
zinapokinzana tunaita nuksi hapa kila jambo litakwenda mrama,
kama nyota zikiendana inaitwa bahati kila utakachofanya kitafanikiwa.
siyo lazima mpenzi hata ndugu na marafiki pia.
kuna mtu ukiamka asubuhi ukakutana nae wa kwanza siku yaweza kuwa mbaya ajabu.
 
Wengine akiwa MTU wa kwanza kusalimu asubuhi, nuksi siku nzima.

Si lazima awe mkeo, hata Kama ni mpangaji JIRANI.

Hata wazee zamani, walijua kabisa Kati ya watoto wao, yupo mwenye bahati na nuksi.

Ndiyo maama alfajiri baba/mama huwaamsha watoto kwa kuita jina la mtoto Fulani kila siku na si mwingine.

Huyo anayeitwa, Ana bahati, kama ni wakike akija kuolewa baadae, mafanikio kibao.
 
Wapo wanawake/wanaume ukiwa naye faragha utapigiwa simu either taarifaya ugonjwa, msiba, ajali, wizi, ttatizo kazini Kama kufukuzwa.

Baada ya fargha, Watumia computer, unaweza ingiza data vibaya, bank tellers ukazimzidishia mteja fedha
 
Binadamu hazaliwi na Nuksi, ila anazipata akiwa mkubwa na kujihusisha labda kwa mahusiano na wanawake / wanaume tofauti tofauti (uzinzi), na hao anaoshirikiana nao kingono, wana roho zao walizonazo zaweza kuwa za mikosi, balaa, mafanikio, uimara wa kila jambo, n.k.

Na ikumbukwe hizo roho siyo nuksi. Sasa mchanganyiko unapokuwa umezidi (wa kimahusiano na wanaume ama wanawake tofautix2) ndizo huzaa hasa hasa Nuksi.

Mungu anachukia sana zinaa, kumbuka kuifuta dhambi ya uzinzi siyo jambo dogo, wanasema kusamehewa dhambi hiyo inawezekana, ila matokeo ya dhambi hiyo hubaki pale pale. Mfano, unaweza kutubu na kuungama, ukaamini dhambi yako imefutika, ila matokeo ya hiyo dhambi, ni yapo pale pale, na ndiyo maana kuna kutubu, kuungama, kuondolewa dhambi, na kusamehewa dhambi.

Hoja hapa, ni idadi ipi ya mahusiano uliyoyapitia, yaweza kuwa ni mmoja, ila huyo mmoja alipitia wapi, ama kazaliwa kutokea mzizi gani (soma vema hapo juu).

Tumche Mungu, siku zote na haswa kuzitii Sheria zake. Zaidi fuatilia vitabu vitakatifu vya Dini yako.

Baadhi ya Maandiko hapo chini,

Ezekieli 24:13-14
Yeremia 16:1-4, 11-12

Ahsante!
 
Nimesikia mara kadhaa kuwa kuna baadhi ya wanawake ukiwa na mahusiano nao kimapenzi unaweza kuandamwa na mabalaa mbalimbali kama kufilisika,kufukuzwa kazi,kufungwa nk. Je kuna ukweli wowote katika hili?
MADEREVA WALIOKUWA WANAPITA KANDA YA KATI ENZI YA NJIA DUME WATAKUBALIANA NA HILI......KUNA MADEMU FULANI MAENEO YA MISIGIRI,ULIKUWA UKIWAGONGA TU....SAFARI INAKUWA MZITO NA MARA KADHAA WATU WALIPATA AJALI NA HATA VIFO.
 
Ni jambo la kusikitisha vijana wa siku hizi hawajui hili. Hata wakielezwa, wanapuuza.
Nawapa na hili, mwanamke mwenye mguu usio na uvungu kwenye unyayo was mguu ni hatari!

Kama umeshamwoa, mkabidhi kwa Mungu kwa kuomba Sana!

Ukiwa naye, hutaona mafanikio, kazi utafukuzwa, akili itafubaa utaishishia kubangaiza.

Hujawahi kujiuliza, hata jeshi haliwataki hao.
 
Nyota, nuksi na balaa ni zao la imani. Km mtu aliweka imani yake kwa ushirikina lazima hayo mambo yatamwandama. Mume km akitoka ktk familia inayoamini ushirikina, familia hiyo haitakubali kijana wao aoe binti wa familia inayomwamini Mungu, kwa sababu ucha Mungu huendana na mkondo wa imani yao kuwa huwezi fungiwa nira na asie amini.
Na upande wa washirikina nako ni hivo hutaweza kumwoa asie amin ushirikina coz ataharibu ule ushirikina hivyo hapo ndo huzuka hayo mambo kuwa mke Huyu hana nyota, ana nuksi, ana balaa nk. Ukibisha wanakupa adhabu ya kishirikina coz ulishakuwa kwenye mkondo huo ili uamini kweli mke ana nuksi. Ukweli ni kuwa hana nuksi isipokuwa mke huyo hayupo ktk mkondo waliotaka wazee, wao walikataa mkorogano ndo maana wakakuadhibu kiaina bila we kujua afu wanakujia kukumbusha " unaona ? Tulikuambia..."
Hivyo km unampenda mke huyo kwanza itakubidi ubadili imani kati ya nuru ama giza, ndo umrudie au la sivyo uoe mke watakayemkubali hao wazee wako.
 
Nimesikia mara kadhaa kuwa kuna baadhi ya wanawake ukiwa na mahusiano nao kimapenzi unaweza kuandamwa na mabalaa mbalimbali kama kufilisika,kufukuzwa kazi,kufungwa nk. Je kuna ukweli wowote katika hili?
so interesting. Kwanini unafikiri wanawake tu ndio wana nuksi? haiwezekani kuwa mwanaume ndio mwenye nuksi labda
 
Wapi nimemtaja mke wa Lowassa?
Mbona unakua na IQ ya kuku wewe?
Acha kutafasiri kitu usicho na ushahidi nacho,hivi leo mzee Moyani Ilembu wa Monduli juu ndiye mume wa Regina Lowassa?
ha ha ha,regina hana mkosi,mkosi alijiletea lowasa mwenyewe alipopanga mapinduzi dhidi ya mwenyekiti wa chama
 
Ni jambo la kusikitisha vijana wa siku hizi hawajui hili. Hata wakielezwa, wanapuuza.
Nawapa na hili, mwanamke mwenye mguu usio na uvungu kwenye unyayo was mguu ni hatari!

Kama umeshamwoa, mkabidhi kwa Mungu kwa kuomba Sana!

Ukiwa naye, hutaona mafanikio, kazi utafukuzwa, akili itafubaa utaishishia kubangaiza.

Hujawahi kujiuliza, hata jeshi haliwataki hao.
hebu weka picha ya huo mguu wenye uvungu,sijawahi ona wala kusikia
 
sasa kama kifanywa kinatumika kila siku na watu mbalimbali lazima atakuwa na nuksi
 
Back
Top Bottom