Hivi ni kwanini siku hizi watu hawapigani mitaani kama miaka ya 1980s?

zile zilikua zinanaitwa enzi za ujinga,leo mtu anasifiwa pesa sio mabavu tena.nakumbuka hata mitaani kwetu walikua wanavuma zana wenye kupiga kumi na mabavu sana ila sasa watu tumeelimika maendeleo kwanza ndoo heshima hata kama mtoto utaitwa mzee,kitu mpungaaa.
 
Mleta mada unanikumbusha mbali sana 1981 ama 1982 kama sijakosea kuna dogo flan aliingia anga zangu kijijin huko mbarali kwa kumtongoza mchepuko wangu. Nilitembeza vitasa kijiji kizima kwa madogo wote wenye umri kama wake. Maumiv makal sana niliwakabiz kwa kosa la mtu mmoja. Yan nilikuwa na bwaka nikiibuka 10 ardhin nikizama nikichomoza 20 wengine chali. Nikamchukua dogo mwengine mwembamba hiv nikamtumia kama fimbo kwa kuwacharaza. Ila kwasasa nimejikita zaid kusaka hela uzee nao ndio huo. Ila miaka iyo ya themanini nilikuwa mtemi sana
heeeeee, boss hapo kuanguka na 10 kuzimama na 20 umekaanga mbuyu,,,,,hahahahaaaaa
 
Zamani Elimu haikua ya kutosha....wapumbavu walikua wengi kuliko wastaarabu...
Kadri siku zinavyokwenda wapumbavu wanakufa, wanapungua au wana badilika na kuwa werevu...ndio maana hamna kupigana pigana

Elimu muhimu Sana.
 
Nakumbuka miaka ya 80-90 ilikuwa jambo la kawaida kukuta jamaa wanapigana mitaani halafu watu wanashangilia sana.

Yaani ukiwa mtemi au gangwe basi unaonekana wa maana sana. Hata baadhi ya disco ilikuwa lazima ziishe kwa ngumi.

Kwa wale wa Iringa mtawakumbuka kina cool 9, shedadi, Ray nk
zamani watu walikuwa hawapelekani kwenye vyombo vya sheria kama sasa hv. Mambo yalikuwa yanaishia uwanja wa mapambano. Kwasasa utamtajirisha mtu bure. Halafu ustaarabu umeongezeka kwa watu wengi.
 
Back
Top Bottom