Hivi kuna taratibu zozote za kujianzishia kabila lako jipya na ukalitungia jina?

Ndiyo unaweza kabisa, na ndivyo Wazungu walivyofanya hapa kwetu, haya yote mnayoyaita Makabila, Wazungu ndiyo walioyaanzisha, kwa maana ya kuchukuwa Makundi mbali mbali yaliyokuwepo tangu mwanzo kuyaweka pmj, kuchora mpaka wa Kijiografia na kuyapa jina kama Wachaga, Wahaya, Wasukuma, au sijui Wagogo!
Rejea kusoma historia hasa za mababu zetu, kabla ya kuja kwa "wageni", naamini wazungu walitenga nchi na kuweka mipaka na sio kutengeneza/kutenga makabila
 
Rejea kusoma historia hasa za mababu zetu, kabla ya kuja kwa "wageni", naamini wazungu walitenga nchi na kuweka mipaka na sio kutengeneza/kutenga makabila

Haya leo unayoyaita Makabila kama Wachaga, Wasukuma, Wahaya, Wamakuwa&Co. hayakuwepo kilichokuwepo ni Makundi ya jamii mbali mbali waliokuwa wanaishi pmj na wenye Utamaduni mmoja au unaofanana, Wazungu walipokuja wakayaunganisha haya Makundi na kuyaita Kabila fulani, na ndiyo maana kwa mfano hakuna lugha ya Kichaga kwa maana Mchaga wa Marangu hawezi kuwasiliana na Mchaga wa Kibosho vivyo hivyo wanaoitwa Wahaya au Wasukuma wengi wa ktk maeneo mbalimbali ya Usukumani au Uhayani wanawasiliana kwa Kiswahili ingawaje wanaitwa ni Kabila moja!
 
Ni lini ulisikia Muingereza, Mchina au hata Binadamu mwingine yoyote yule ukiacha Mwafrika akitumia neno Kabila kujitambulisha? Unafikiri kwa nini Muingereza hasemi Scottish tribe, au Irish tribe?

Ukweli ni kwamba hayo Makabila yenu yalianzishwa na Mzungu, hata wewe unaweza kuanzisha Kabila, nchini Kenya Raisi Moi alifnya sana kama vile Wakoloni, alianzisha Makabila mapya kuyapa majina ili kupata kura nyingi na kama ulikuwa haufahamu neno Kabila (tribe) ni neno negative, na Wazungu hulitumia kwa Waafrika tu wakimaanisha watu ambao hawajastaarabika bado!
uko vizuri mno mkuu. Hapo umenifumbua macho baadhi ya mambo.
Ni risk kubwa sana kuishi kwenye nchi au kuwa raia wa nchi ambayo hujui historia ya nyma ikoje.
Leo mchaga anaweza kujiona mbora, Au mtu wa mjini akajiona bora na kumuita wa kijijini mshamba kumbe ni mabaki ya ukoloni
 
Mi nadhani au nakushauri kabila utakalo anzisha muongee kikoromije mtatawala dunia
 
Ushauri wangu tembeza umboro kwa kila mwanamke anayekatiza mbele yako hakikisha anabeba mimba wakati huo unaedit lugha mbalimbali ili utohoe lugha kwa ajili ya kabila lako kisa kusanya vifaranga vyako vyote anza kuvitandika na lugha yako mpya vitakua nayo na kabila lako utalisajili
 
Huwez asilani... Jaribu kuongea lugha mpya ambayo hata wewe usiojua uone balaa lake
 
Ni lini ulisikia Muingereza, Mchina au hata Binadamu mwingine yoyote yule ukiacha Mwafrika akitumia neno Kabila kujitambulisha? Unafikiri kwa nini Muingereza hasemi Scottish tribe, au Irish tribe?

Ukweli ni kwamba hayo Makabila yenu yalianzishwa na Mzungu, hata wewe unaweza kuanzisha Kabila, nchini Kenya Raisi Moi alifnya sana kama vile Wakoloni, alianzisha Makabila mapya kuyapa majina ili kupata kura nyingi na kama ulikuwa haufahamu neno Kabila (tribe) ni neno negative, na Wazungu hulitumia kwa Waafrika tu wakimaanisha watu ambao hawajastaarabika bado!
Rubbish!..
 
Hii itawasaidia wale wasiojua lugha ya kikabila ya Baba na Mama...Wale wa mjini wanaojua kiswahili tu
 
kama mwl,wazanaki yaani umekuja na nini,ulikuwa ukirudi toka safari ukifika kwilembo unaulizwa umetuetea nini au umeleta nini? yaani wazanaki? Alipokufa akazikwa eneo linaloitwa "Mwitongo" yaani bustani ya wafu.Rejea nchi za Burundi na Rwanda.
 
Sidhani kama kwa maisha ya sasa unaweza kunzisha kabila, sababu kabila lina eneo, mila, lugha na taratibu mbalimbali ambazo zinawajumisha wanakabila na kuwatofautisha na wengine. zamani ilikua familia ikihama na kukutana familia za makabila mengine katika maeneo mapya ya mbali kunatokea mchanganyiko na kabila mpya inaweza kutokea sababu wanakua wamejitenga kabisa na kabila lao la asili. lakini sasa ulimwengi ni mdogo kwa sababu ya mawasiliano kwa hiyo siku zote uko na mawasiliano na jamma zako.
 
Back
Top Bottom