Hivi Jeshi la Tanzania lina Special Forces?

Ingekuwa duniani wanajeshi wanapigana na matofali na fimbo za mbao, basi tungekuwa na jeshi bora sana.
Mbona hata China na Korea wanafanya hivyo vitu. Ni kawaida ktk mafunzo ya kupambana pasipo silaha, na ukifikia level ya ukomando unapaswa kuwa fit kweli kweli.
 
Actually when comes to a powerful standing army, we can run the continent. Jeshi letu si la mchezo mchezo naungana nawe. Vijana wako well trained, well equipped I know this not from story za kijiweni.
Tuweke unazi pembeni, acha uhalisia uongee. Mkuu, vita vya sasa ni teknolojia na vifaa na Pesa, Period!

Labda tupambane na Afrika Mashariki na Kati ila sio kusema Bara zima. Unazijua nchi kama Algeria, S.Afrika, Misri n.k jinsi walivyopiga hatua ktk uboreshaji wa majeshi yao?
 
Acha zako bwana, mbona unaishi kizamani mkuu?
Hivyo vya nchi zingine ukitafuta taarifa zake unazipata, hata ukitaka kuangalia jinsi wanavyofanya mazoezi unaweza ni bando lako tu.

Wewe unakuja hapa kutoa hekaya za uongo kama hivi, hebu zunguka online kwanza ndiyo uanze kulalamika.

ELEWA HIVYO INATOSHA
 
Lazima wapo ila jina wanalotumia ndo shida ukisikia usalama wa taifa nimiongoni mwa special force even in specific issues broo
 
Tuweke unazi pembeni, acha uhalisia uongee. Mkuu, vita vya sasa ni teknolojia na vifaa na Pesa, Period!

Labda tupambane na Afrika Mashariki na Kati ila sio kusema Bara zima. Unazijua nchi kama Algeria, S.Afrika, Misri n.k jinsi walivyopiga hatua ktk uboreshaji wa majeshi yao?
Umesahau kitu kimoja ni morali na nidhamu ya wanajeshi(Utayari wa kupambana kwenye medani). Kikikosekana hiki hata kama mna tech na pesa kubwa kiasi gani haitosaidia chochote.

JWTZ ni jeshi imara kiasi chake lina nidhamu kubwa lakini tech bado ni duni naeza kushauri zaidi ya hapo.
 
maxresdefault.jpg
 
Sidhan kama Tanzania tunazo special forces zinazofanya Kazi Kama za nje,
Sidhan Kama Tanzania tunahitaji kua na special forces kwa sababu hatuna operation za siri dhidi ya nchi nyingine
Unajuaje?
 
special force ipo ila hautaijua mpaka cku nchi ichokonolewe na wazembe wazembe ndipo utajua kuwa lile karandinga ilikuwa ni show tu ila uhalisia upo saa wazee wakiwa kazini.
kwa maelezo zaidi,TEMBELEA KAMBI ZA JESHI.
 
Kuna jamaa mmoja amepitia mafunzo ya kukaanga kokoto kwa mkono wake kama mwiko, kukimbia kivuli chake na kukiacha umbali wa mita 1, kukata umeme nchi nzima kwa kupuliza 'puuuuu', ngoja nimuulize yuko kikosi gani kama si special force
Babu wewe sio mzima........ha ha ha ha.
 
Babu wewe sio mzima........ha ha ha ha.
Unaweza dhani utani ila kwa kuwa siko hapa kuweka kila kitu wazi ngoja niachie ila waliopita kule wanaelewa hicho kitu, achana na wapiga show check wale jamaa wenye uwezo wa kubadili sura na kuwa na mabaka kama uso wa zitto. Mcheki yule jamaa anayetembea na bwana yule ndo utajua ile sura si ya mchezomchezo imepitia kukaanga chips kwa mkono, etc
 
Umesahau kitu kimoja ni morali na nidhamu ya wanajeshi(Utayari wa kupambana kwenye medani). Kikikosekana hiki hata kama mna tech na pesa kubwa kiasi gani haitosaidia chochote.

JWTZ ni jeshi imara kiasi chake lina nidhamu kubwa lakini tech bado ni duni naeza kushauri zaidi ya hapo.
Nashkuru kwa kuzungumzia Nidhamu ya Kijeshi, ni kweli kabisa Mkuu nidhamu ya kijeshi ni muhimu sana ndani ya Jeshi.

Na nakupa hongera kwa kutokuwa mnafki, jeshi letu kwenye teknolojia bado sana.
 
Mie sio mjuzi sana wa mambo ya majeshi lakini ninavyodhani;kila jeshi huwa na watu wenye mafunzo ya kipekee.Hivyo, kukitokea jambo la dharura au kutekeleza jambo Fulani la kipekee huwa wanachaguliwa watu kadhaa kutoka katika kundi hilo ili kutekeleza mpango/jambo husika.Hapo sasa kundi hilo ndilo special force na linawezekana likawa na jina lake la kudumu au linaweza kupewa jina malum kutokana na tukio.
 
Tuweke unazi pembeni, acha uhalisia uongee. Mkuu, vita vya sasa ni teknolojia na vifaa na Pesa, Period!

Labda tupambane na Afrika Mashariki na Kati ila sio kusema Bara zima. Unazijua nchi kama Algeria, S.Afrika, Misri n.k jinsi walivyopiga hatua ktk uboreshaji wa majeshi yao?
Mkuu Ni kweli kabisa....jeshi km misri lenye heshma zake,jeshi km Algeria lenye fighter jets za kisasa km f-16 Na wako Na mpango wa kunua s-400 toka urusi halafu unaaminishwa eti tumewazidi...
 
Back
Top Bottom