Majigoro
JF-Expert Member
- Jan 5, 2017
- 301
- 551
Kikosi cha makomandoo ni kikosi kama vimosi vya ardhini, anga, maji nk isipokuwa wao wamepewa mafunzo ya ziada kukabiliana na mazingira tatanishi... Ikifika kwenye special force watachaguliwa makomandoo wachache wa fani mbalimbali mf snippers, daktari, mtaalam wa milipuko na inawezekana kumchukua hata raia endapo kuna utaalamu wa ziada unahitajika ambao wameshindwa kumpata mtu ndani ya jeshi hapo kinaundwa kikosi maalum na wanapewa mafunzo ya ziada yanayoendana na mazingira wanayoenda kukabiliana nayo... Inasemekana kabla ya kwenda kumuua osama wale jamaa walijengewa jengo linalofanana na makazi ya osama na wakaanza kufanyia mazoezi kwa miezi mitatu. Tanzania tuna makomandoo na kila nchi ina makomandoo ila katika hao makomandoo ndio vinaundwa vikosi maalum. Naendelea kutolea mf Marekani wanapokuwa na mission tata huwa wanatumia Navy Seals ila wanapokuwana mission zisizo hitaji kusubiri wala kupoteza muda wanatumia Delta Force.Then JWTZ wana Special Forces. Kumbuka JWTZ wana kikosi cha Makomandoo. Sasa hawa Makomandoo hawafundishwi kuwa Makomandoo ili wakapigane kama infantria.