Historia ya mlima Kilimanjaro

Dec 21, 2023
80
158
Mlima Kilimanjaro
Kilimanjaro ni jina la mlima mrefu kuliko yote barani Afrika. Mlima huo uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa mita 5,895 (futi 19,340).

Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi ya mlima tu, ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hiyo mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja, hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima.

Kijiolojia Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko mnamo mwaka 1730.

Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru. Mtu wa kwanza kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kwa Kijerumani: Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

Kibo ina theluji na barafuto ndogo kadhaa.

Sasa leo nakupa urahisi wa kuutembelea mlima kilimanjaro kwa safari ya kutwa yaani (Day Trip) kutoka marangu gate mpaka mandara hut.

Pata fursa ya kutembelea mlima Kilimanjaro kwa gharama nafuu zaidi zilizoandikwa kwenye tangazo letu hapo chini 👇🏾
 
Attachments

  • Green Black Bold Hiking Trip Poster_20241207_071330_0000.png
    Green Black Bold Hiking Trip Poster_20241207_071330_0000.png
    1.6 MB · Views: 3
😌

Hii ni Historia ya Mlima Kilimanjaro ama Tangazo la Biashara?

Manake nilipata shauku kubwa tu, nikajisomea mpaka nilipo fik hapa👇🏿
Sasa leo nakupa urahisi wa kuutembelea mlima kilimanjaro kwa safari ya kutwa yaani (Day Trip) kutoka marangu gate mpaka mandara hut.

Pata fursa ya kutembelea mlima Kilimanjaro kwa gharama nafuu zaidi zilizoandikwa kwenye tangazo letu hapo chini
Nimenyoosha mikono....Ila

In all fairness, this is a misleading advertisment.

Tuheshimu Nyara zetu za Taifa
 
Mlima Kilimanjaro ni mlima uliopo nchini Tanzania na ni mlima mrefu zaidi barani Afrika. Mlima huu ni volkano inayokumbwa na theluji kileleni, licha ya kuwa karibu na ikweta. Kilimanjaro ina urefu wa mita 5,895 kutoka usawa wa bahari hadi kileleni.

Historia ya mlima Kilimanjaro imejaa hadithi na maajabu. Mlima huu ni kitovu cha utamaduni wa Kiafrika na kisiwa cha biolojia tofauti. Mawe yanayopatikana kwenye mlima huu yamewashawishi wachimbaji kwa karne nyingi, na eneo hili linathaminiwa kama tapo la utamaduni na historia.

Mtu wa kwanza kurekodiwa kupanda mlima huu ni Hans Meyer kutoka Ujerumani mwaka 1889 akiwa na wapagazi Waafrika na mtaalamu wa jiolojia Ludwig Purtscheller. Waligundua mabadiliko ya hali ya hewa kutoka kwa misitu ya chini hadi kilele cha theluji, pamoja na maisha ya mimea na wanyama katika maeneo mbalimbali ya mlima.

Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ni moja ya maeneo ya hifadhi muhimu zaidi nchini Tanzania na ina aina mbalimbali za wanyama kama vile nyati, nyani, na fisadi. Pia, hifadhi hii ina mimea adimu na mandhari ya kipekee ambayo huwavutia watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Kwa kifupi, mlima Kilimanjaro ni hazina ya historia, utamaduni, na mazingira ya kipekee ambayo inastahili kutembelewa na kuenziwa.
 
😌

Hii ni Historia ya Mlima Kilimanjaro ama Tangazo la Biashara?

Manake nilipata shauku kubwa tu, nikajisomea mpaka nilipo fik hapa👇🏿

Nimenyoosha mikono....Ila

In all fairness, this is a misleading advertisment.

Tuheshimu Nyara zetu za Taifa
Hili ni tangazo
 
Mlima Kilimanjaro
Kilimanjaro ni jina la mlima mrefu kuliko yote barani Afrika. Mlima huo uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa mita 5,895 (futi 19,340).

Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi ya mlima tu, ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hiyo mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja, hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima.

Kijiolojia Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko mnamo mwaka 1730.

Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru. Mtu wa kwanza kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kwa Kijerumani: Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

Kibo ina theluji na barafuto ndogo kadhaa.

Sasa leo nakupa urahisi wa kuutembelea mlima kilimanjaro kwa safari ya kutwa yaani (Day Trip) kutoka marangu gate mpaka mandara hut.

Pata fursa ya kutembelea mlima Kilimanjaro kwa gharama nafuu zaidi zilizoandikwa kwenye tangazo letu hapo chini 👇🏾
Historia yenyewe iko wapi? Hvyo vijimistari viwili vitatu ndiyo vinakushawishi kuwa unaweza kutushawishi kuita historia? Kama hujui kitu si uache tu.
 
Historia haijakamilika bila kuelezea maana au asili ya jina Kilimanjaro
 
Hiyo master yako hainihusu. Hata ungekuwa na PhD kama mimi, kama utaleta utopolo unaambiwa tu mwanangu.
 
Back
Top Bottom