Hii picha ya Dr Dau msalabani inathibitisha nini?

Status
Not open for further replies.
Unamchukia mtu mpaka unajisahau na kunamfananisha na unaeamini ni Mungu wako? Duh hii kali ya weekend!
 
Haihitaji rocket science kugundua kuwa hii haiko sawa katika nchi ambayo ni secular state kama Tanzania.

Ila napata shida kudhani kuwa gazeti hili litapewa adhabu yoyote ile maana mmiriki wake alikuwa kiungo muhimu kwenye harakati za uchaguzi 2015.
 
Yaani wapo akina Kitylia na wengine wengi wagalatia lakini hawajathubutu kuwekwa hivi wezi wote wa escrow,rada,richmond nk hawajawai kuandikwa hivi ila kwa bwana Dau tu anapaswa kutundikwa msalabani.
 
Pamoja na ukweli kwa huyu Dau ni Fisadi kuu lenye udini..lakini mwandishi wa gazeti hili ni punguani
 
Shigongo katika ubora wake, nna mashaka na huyu jamaa anatumia njia nyingi za kufedhehesha wengine ili kujinufaisha yeye
 
Dau Kumpa msalaba ni kupotoka sana..
Mbona kwa Pilato bado hajafikishwa..?
 
''Watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa"
Hapa kuna harufu ya uchochezi inayofanywa na upande fulani wa Imani kwenda kwa Imani nyingine kwa njia ya uchonganishi.Ukiangalia kwa haraka haraka na mihemko ya kidini, unaweza kuona hiyo picha ya kwenye gazeti kama inadhalilisha Imani fulani lakini tujiulize swali moja tu,Je;msalaba ulitumika kumsulubisha Yesu(Nabii Issa) peke yake au kwa kila aliyetuhumiwa au kudhaniwa ni mhalifu?

Hakuna jambo baya kama kuchochea mambo ya ki-imani.Ni kama moto unavyosambaa kwenye nyasi kavu.Tumzungumzie mtu na makosa yake lakini tusiiguse imani yake maana kumbuka kwa kufanya hivyo unagusa wengi.
 
Yaani wapo akina Kitylia na wengine wengi wagalatia lakini hawajathubutu kuwekwa hivi wezi wote wa escrow,rada,richmond nk hawajawai kuandikwa hivi ila kwa bwana Dau tu anapaswa kutundikwa msalabani. .

Hawa wanajulikana chuki yao ni Uislam hawana zaidi.
 
Tunafahamu kuwa Waziri wa kazi Jenista Mhagama, Katibu Mkuu wizara ya Kazi Eric Shitindi, Waziri wa mambo ya Ndani, Charles Kitwanga ,Mkurugenzi wa Operations NSSF Crescentius Magori na Director wa Public Relations NSSF Eunice Chiume wanafanya kazi ya ziada kumchafua Dr magazetini lakini kwa nini wahariri wanakubali kutumika kupandikiza mbegu ya chuki na udini?

Kwa nini huu uchochezi unanyamaziwa na vyombo vya dola?

Sasa ile habari kuwa Magufuli alipewa taarifa za uwongo juu ya Dr Dau na watu wake (akina Sefue, Shitindi,Kitwanga na Mhagama) hazikukuwa na ukweli wowote ule na hii jitihada yenye harufu ya duni inayotumika sasa imedhihiri wazi kuwa hii vita dhidi ya Dr Dau ni Udini na sidhanii kama Mheshimiwa Magufuli anafurahia haya mambo.

Kwanza Magazeti ya MTANZANIA na DIRA na JAMBO LEO yalimchafua Dr Dau kwakutumia ripoti feki ya CAG.

Sasa naona RISASI wamekuja na hii. Hatujui kesho na wiki ijayo magazeti yakuja na nini lakini sidhani kama wakoaji wakubwa wa Dr Dau watapendezwa na hili.

Pia cha kushangaza kwa nini Dr Dau hajayashitaki haya magazeti yanayomchafua? Ni wazi waziri wa Habari Nape anafurahia haya mambo ya kuchafuana magazetini.

20160409_045728.jpg
Wanaopaswa kulalamika hapa ni sisi wakristu kwa kudharirishwa kwa msalaba ambayo ni nembo yetu. Naamini mngekuwa upande ule tayari mngekuwa barabarani. Sijapenda kutumia msalaba kwa mtu mwenye kashifa kama Dau harafu utumie msalaba kufikisha ujumbe wako. Dau si Yesu na kwa kweli wametutukana vya kutosha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom