Hii kero ni kwa shule hii Tu au huko kwengine yapo haya?

hamna cha urefu sema walimu wanafanya favour tu,mfano mitihani inayotakiwa kufanyika ni midterm,terminal na annual ila unakuta walimu wanatoa test za mara kwa mara na kufundisha mda wa ziada ila malalamiko yako pale
Unafikiri hizo test zinasaidia au hazisaidii?
 
80 ndogo sana, kumbuka wako pale miaka 2 wanapita tuu, hakuna muda wa kupoteza,mimi ningelipa tuu aongeze chance ya kufaulu
 
Nadhani kaelewa
Hawezi kuelewa hata kwa kugongwa makwenzi kichwani. Anawezaje kuhoji issue ya maamuzi ya kikao cha wazazi kuchangia hela kuwamotisha walimu (hususani wanaojitolea) ili kuboresha taaluma ya mtoto aliyemzaa yeye mwenyewe kwa hiyari yake!?

Ikiwa anaona elimu ni ghali basi ajaribu ujinga. BTW sidhani kama amelazimishwa kuchangia.
 
80 ndogo sana, kumbuka wako pale miaka 2 wanapita tuu, hakuna muda wa kupoteza,mimi ningelipa tuu aongeze chance ya kufaulu
Mkuu unajipa uhakika gani kwa kutoa hiyo 80 Mtoto atafanya vizuri? Suala sio pesa. Ni utayari waalimu wetu wa kujitoa kwa ajili ya majukumu yao.
 
Huwaliza sana hili swala la tuition kwa wanafunzi, sijawahi kupata majibu sahihi. Hivi ni kwa nini hao walimu wasitie nguvu ya tuition kwenye vipindi vya kawaida?
 
Hawezi kuelewa hata kwa kugongwa makwenzi kichwani. Anawezaje kuhoji issue ya maamuzi ya kikao cha wazazi kuchangia hela kuwamotisha walimu (hususani wanaojitolea) ili kuboresha taaluma ya mtoto aliyemzaa yeye mwenyewe kwa hiyari yake!?

Ikiwa anaona elimu ni ghali basi ajaribu ujinga. BTW sidhani kama amelazimishwa kuchangia.
Mkuu,elewa kuwa sipingi maamuzi ya wazazi. Ninachokiongelea ni kitendo cha waalimu kuona wao si sehemu ya tatizo na kuja na hoja kuwa mzazi ajiongeze ili Mtoto wako apambaniwe. Kama mwalimu umefikia hatuwa hii ni wazi kabisa majukumu yako ya uwalimu yamekushinda na hutoshi kwa hiyo nafasi.
 
Ana mdomo huyo🙌
 
Umeshaongea tayari kwamba walimu wanajali masilahi yao
 
Mkuu mbona simple saana kama unaona walimu watafaidi hizo pesa zako muhamishe mwanao.
Hivi kweli wazazi waazimie kikao afu lawama uwatupie walimu?
Unajua maana ya motisha?
Ushawahi kujiuliza ni kwanini kunakuwa na tuzo mbali mbali zinazotolewa kwa wanaofanga vizuri wakati ni wajibu wao kufanya hivyo? Nyie ndio wale wazazi ambao wakishaskia elimu bure basi kazi ni kufyatua tu watoto bila kujali kama watapata huduma muhimu kutoka kwa wazazi.
Wenzenu wa private kuna hadi michango ya majaribio ya kila wiki ila hawalalamiki.
Mkuu tafuta hela ukiwa na hela hata ROHO YA KICHAWI KAMA HII YAKO HAIPO.
 
Mkuu,elewa kuwa sipingi maamuzi ya wazazi. Ninachokiongelea ni kitendo cha waalimu kuona wao si sehemu ya tatizo na kuja na hoja kuwa mzazi ajiongeze ili Mtoto wako apambaniwe. Kama mwalimu umefikia hatuwa hii ni wazi kabisa majukumu yako ya uwalimu yamekushinda na hutoshi kwa hiyo nafasi.
Ujamaa uliondoka na mwalimu Nyerere ndugu yangu. Mlipie mwanao apambaniwe afanye vema kwa masomo yake kwa faida ya maisha yake
 
Mkuu mbona simple saana kama unaona walimu watafaidi hizo pesa zako muhamishe mwanao.
Hivi kweli wazazi waazimie kikao afu lawama uwatupie walimu?
Unajua maana ya motisha?
Ushawahi kujiuliza ni kwanini kunakuwa na tuzo mbali mbali zinazotolewa kwa wanaofanga vizuri wakati ni wajibu wao kufanya hivyo? Nyie ndio wale wazazi ambao wakishaskia elimu bure basi kazi ni kufyatua tu watoto bila kujali kama watapata huduma muhimu kutoka kwa wazazi.
Wenzenu wa private kuna hadi michango ya majaribio ya kila wiki ila hawalalamiki.
Mkuu tafuta hela ukiwa na hela hata ROHO YA KICHAWI KAMA HII YAKO HAIPO.
Mkuu nashukuru kwa mawazo yako. Wazazi si walio- arrange hicho kikao. Ni waalimu baada ya kufanya setup ya mipango yao. Wazazi walipitishwa tu kwenye hoja ambayo waalimu waliona kwao ina mashiko kisha wao wakajitoa kama kwamba wao si waratibu wa hicho kikao.

Lengo la wao kufanya hivyo,ionekane maamuzi yoyote yaliyotolewa pale ni ya wazazi si wao. Mtazamo huu ulikuwa mzuri kama sehemu ya wazazi,wangekuwa na malalamiko ya watoto wao kutofanya vizuri hivyo kuitisha kikao cha wazazi na kuangalia namna ya ku- deal nalo.

Hivyo maamuzi ya hapa kama ingeamuliwa na wazazi wenyewe kuwa tuwape motisha waalimu, sioni kama kungekuwa na tatizo. Shida kuwa wao tayari walishafanyiwa setup na waalimu.

Hakuna mzazi asiyemtakia mambo mazuri Mtoto wake endapo kila kitu kitaenda katika njia mzuri. Bado nasisitiza waalimu wasikwepe majukumu yao kwa kisingizio cha motisha ili WAWAPAMBANIE WATOTO WETU. Hakuna roho ya kichawi hapa. Wao wajibu wao kufundisha,motisha itakuja pale juhudi yako inapoonekana. Motisha Kwanza bila jitihada hiyo ni hongo.
 
Kama wazazi wameridhia hiyo Elfu themanini hakuna shida kama ingekuwa tatizo basi wazazi wangekataa kutoa ndugu yangu. Kikubwa ni maridhiano baina ya wazazi na walimu
 
Ujamaa uliondoka na mwalimu Nyerere ndugu yangu. Mlipie mwanao apambaniwe afanye vema kwa masomo yake kwa faida ya maisha yake
Mkuu bahati mzuri sina Mtoto anaesoma huko. Nimeumizwa na mzazi aliyekuja kunipa ABC ya hili. Tena amefika mbali amedai ikitokea mwanae kufeli basi atafelishwa kwa kutomtolea hiyo gharama.
 
Elimu gharama sana
 
Miaka ya nyuma hiyo elfu 80 tulikuwa tunalipia tuition tena topic mbili za somo moja tu. Na Mwalimu aliyekuwa anafundisha tuition ni wa hapo hapo shuleni.
 
Anayepokea sifa kila siku ndiyo apokee na lawama sasa ingawa hamna tatizo ikiwa walikubaliana, hata kama unajaribu kusema Walimu walichokoza agenda wazazi wakaingia kwenye mfumo, maisha ni makubaliano tu.🤣🤣
 
Kwa nn unampeleka mtoto tuition?
Ila kumpa mwalimu motisha ya 80k roho inakuuma
Haya si malalamiko waalimu wengi wanakosa uwajibikaji kichaka kinakuwa hiki. Mwanafunzi unamfundisha, kama mwalimu wewe ni mtu wa Kwanza kufahamu changamoto za mwanafunzi wako. Ikitokea anafanya vibaya na wewe unaona suluhu kumuambia mzazi ajiongeze ili mwanae apambaniwe ina maana mwalimu kashindwa kutekeleza majukumu yake kifupi hatoshi.
 
Back
Top Bottom