Kitabu cha 8=Darasa la sita. Humo ndio utakuta wimbo wa Tanzania, tanzania nakupenda kwa moyo wote... na shairi la Tuipende Tanzania.. hapa naweka verse mbili, tatu:
Sina budi kuisifu, nchi yetu Tanzania
Kwa shairi maarufu, na vina kupangiia,
Nipange na kusanifu, shairi kuwaimbia
Tuipende Tanzania,nchi tuliyozaliwa.
Kuna mlima mrefu, kwa sifa twajivunia
Ukiwekwa kwenye safu, urefu kukadiria,
Hapawi ulinganifu, Afrika yote pia,
Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa.
Hapawi w kulingana, wala kuukaribia
Hawaupati wa Ghana, Uganda wala Zambia
Milima kila namna, yote haitofikia
Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa.
Una vilele viwili, majina nawatajia
Mawenzi ni cha awali, hapa nawahesabia
Kibo kilele cha pili, jamani nawaambia,
Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa.
Naacha mlima ule, na vilele vyake pia
kusudi nisongembele, kwenye mbuga kuingia
nifike hapa na pale, nichungue kila njia
tuipende tanzania nchi tuliyo zaliwa
Nifikapo Serengeti, au Mikumi kwa nia
Kwa jitihada na dhati, wanyama kuangalia
kuna makundi ya nyati, nyumbu na pundamilia
Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa.
Mbuga na misitu hii, na nisivyowatajia,
Huvutia watalii, kila mwaka kutujia,
Nao hawavumilii, wanyama kuwasifia,
Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa...