Haya ndiyo maandishi ya kwenye Sanamu la Askari

Mnara wa Askari Kwa kiwango chochote huwezi kufananisha na diamond

mjerumani ameficha maboxi ya madini.hipo siku watakuja kununua au kuingia ubia ili wachimbue hapo.maana ni mjerumani ndie aliweka hizo kumbukumbu.

swissme

huyo mbunge ndo kazihirisha kuwa sisi wabongo kweli IQ yetu ni 72.

aje aweke kwenye sanam la moshi walivo wachaga.hawampendi hahaha sijui ingekuaje

Wanachadema wanjua at ile ni sanamu ya wapigania uhuru wa tanganyika na wengine hudhani kuwa ile ni sanamu ya mayunga . Hili ni kosa kubwa hapa kwetu tunacho kizazi cha nyumbu kinacho haribu taifa letu

kama kiongozi wa vyama alipata division zero unategemea wafuasi wawe na akili gani ni suala la kupita pale na kuliangalia na kusoma:

ishu ya huyu diamond mtoboa pua mm siiungi mkono

Sanamu ni sanamu tu. Hapo yabadilishwe maneno tu yaliyoandikwa hapo. na kama tunadhani kuwa sanamu hiyo haituwakilishi kwa sababu hatukuwa na bunduki enzi hizo, basi ichongwe sanamu ya askari mwenye mkuki, na ngao au upinde na ngao...na maneno mahsusi, Basi! Habari ya Diamond, wamchongee Sanamu Tandale na Ulanga!

Dimond ndo uchafu gani??
 
Macos,
Ahsante sana kwa kunitaja katika hii mada ya Picha ya Bismini na kuniomba
nichangie

Wakati wa Vita ya Pili ya Dunia (1914 - 1918) Tanganyika ilikuwa chini ya
utawala wa Wajerumani.

Sanamu hii ya Bismini ni kwa ajili ya kuwakumbuka askari wa waliopigana
upande wa Muingereza dhidi ya Mjerumani.

Hii ni kumbukumbu ya babu zetu askari na wapagazi Waafrika ndani ya jeshi
la Muingereza.

Kama ulivyosema ni kuwa awali ilikuwapo picha ya Herman Von Wissman.

Wissman ndiye aliyeongoza vita dhidi ya wananchi wa Tanganyika kwa kuleta
askari mamluki Wanubi kutoka Sudan na Wazulu kutoka Mozambique.

Katika hawa Wanubi maarufu katika askari hawa katika mji wa Dar es Salaam
ni Mzee Hamisi baba yake Ibrahim Hamisi mmoja wa waasisi wa African
Association pale ilipoanzishwa mwaka wa 1929.

Mtoto wa Ibrahim Hamisi, Abdallah Ibrahim ni mmoja wa watu niliozungumza
nao katika kujifunza historia ya mji wa Dar es Salaam.

Askari wengine walitoka Congo na mmoja wapo ni babu yangu mkuu Samitungo
Mwekapopo
aliyekuwa katika Boma la Wajerumani Shirati, Musoma.

Katika Wazulu walioingia Tanganyika pamoja na Wissman ambao taarifa zao ziliweza
kuhifadhiwa ni Sykes Mbuwane baba yake Kleist Sykes, baba yao Abduwahid,
Ally
na Abbas Sykes.

Hawa askari wote mamluki walikuwa katika kikosi kilichojulikana baadae kama ''Germany
Constabulary,'' na mkuu wa jeshi hili alikuwa Affande Plantan baba yao Mwalimu
Thomas Saudtz Plantan,
Schneider Abdilllah Plantan, na Ramadhani Mashado
Plantan.

Wakati wa Vita Vya Pili Mwalimu Thomas Plantan ndiye alikuwa rais wa African Association.

Inasemekana huyu Affande Plantan alikuwa ndiye chifu wa Wazulu Mozambique
na ndiye aliyewekeana mkataba na Wissman kuja na jeshi la Wazulu kuiteka Tanganyika.

Katika mswada wa kitabu alichoandika Kleist Sykes (1894 - 1949) kuhusu maisha yake,
Kleist anaeleza kuwa mkataba ulikuwa Wazulu na Wajerumani kuitawala Tanganyika
kwa ushirika.

Wazulu na ujuzi wao katika medani ya vita uliwawezesha Wajerumani kuwashinda
Abushiri bin Salim na Chifu Mkwawa.

Wajerumani ndiyo katika kuonesha shukurani yao kwa Wazulu walimfanya Affande
Plantan
kuwa mkuu wa majeshi yao na wakaliita jeshi hilo ''Germany Constabulary.''

Haya kaeleza Kleist katika mswada wake.

Vilevile waliwajengea shule watoto wa wanajeshi wao ambayo ilikuwa ilipo sasa Ocean
Raod Hospital ambako Kleist alisoma hapo hadi darasa la sita na alipomaliza akaingizwa
katika jeshi pamoja na Schneider.

Wakati wote wa utawala wa Wajerumani Waafrika hawa wakiishi ndani ya kambi ili
kuwatenganisha na wazalendo wa Tanganyika.

Kwa hali hii ya kutoa elimu kwa watoto wa askari katika jeshi la Wajerumani, hawa
wakoloni walifanikiwa kuwanyanyua juu Wazulu na Wanubi kiasi kuwa waliposhindwa
Vita Kuu ya Pili na Waingereza kuja sasa kuitawala Tanganyika, walioweza kupata kazi
za maana katika utawala mpya walikuwa hawa Wazulu na Wanubi ingawa katika vita
ile walipigana dhidi ya Muingereza katika jeshi la Wajerumani.

Watoto wa hawa Wazulu walioingia Tanganyika na Wissman ambao walipigana dhidi ya
Waingereza ambao kumbukumbu zao zimehifadhiwa na akina Sykes na Plantan.

Katika Vita ya Kwanza ya Dunia watoto wa hawa Wazulu walipigana chini ya uongozi wa
Von Lettow Vorbeck aliyekuwa wakati ule ndiye mkuu wa majeshi ya Ujerumani Tanganyika.

Kleist ndiye alikuwa Aide de Camp wa Vorbeck.

Vorbeck alipoona kazidiwa nguvu na majeshi ya Waingereza akishambuliwa na General
Smuts
kutoka Afrika ya Kusini alivuka mpaka akakimbilia Mozambique na baadhi ya askari wake wa Kizulu.

Kleist alikamatwa mateka na akawekwa kambi ya askari mateka Dodoma.

Kitu cha kuangalia ni kuwa hawa watoto wa Wazulu na Wanubi ambao walipigana dhidi
ya Waingereza ndiyo waliokuja kufanya mabadiliko makubwa katika siasa za Tanganyika
katika kudai uhuru kutoka kwa Waingereza, uhuru ambao ni wa nchi ambayo ilikuwa yao
kwa kuhamia na wengine kwa kuzaliwa.

Mathalan Mwalimu Thomas Plantan na nduguze wote hawakuzaliwa Tanganyika walikuja baada ya baba yao kuwa keshajiweka vizuri nchini.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Mashado Plantan alikuja Tanganyika mwaka wa 1905.

Hawa vijana wote wa Kizulu walikuwa katika African Association, Kleist akiwa muasisi khasa na Schneider akiwa mwanaharakati wa kupigiwa mfano kwani aliwataabisha sana Waingereza khasa wakati wa Vita ya Pili ya Dunia (1938 - 1945) kiasi cha Waingereza kuamua kumkamata na kumuweka kizuizini Mwanza alikofungwa hadi mwisho wa vita.

Mashado
yeye alianzisha gazeti, ''Zuhra,'' na ndiyo ilikuwa sauti ya Mtanganyika wakati wa ukoloni.

Kleist ingawa alikuwa karibu sana na Waingereza yeye alijiingiza katika siasa za kuwapinga Waingereza kichinichini na alipounda African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) chama alichokiasisi mwaka wa 1933 na rafiki yake wa Kimanyema, Mzee bin Sudi.

Hawa vijana wa Kizulu katika Tanganyika ile ya 1930 wao wakijiona bado ni askari katika jeshi la Kijerumani na zaidi kwa kuwa wote walikuwa wakikisema Kijerumani kama maji.

Hili jambo bila shaka likiwakera sana Waingereza.

Sidhani kama hawa Wazulu na Wanubi walikuwa wakikerwa na ile sanamu ya kamanda wa baba zao Hermann von Wissman.

Lakini Vita ya Pili ya Dunia ilipoingia Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally walivaa sare za majeshi ya King's African Rifles (KAR) kupigana na Wajerumani ambao walikuwa washirika wa babu na baba yao.

Abdul na Ally walikwenda kupigana Burma dhidi ya Wajapani na wote wawili walipewa medali ya ''BurmaStar,'' na Waingereza baada ya kwisha vita mwaka wa 1945.

Hizi ndizo athari za ukoloni.
Kumbukumbu hizi tuzichukulie kama kumbukumbu katika historia ya Tanganyika.

Soko la Kariakoo ambako ndipo Waingereza walipokuwa wakiwaandika kazi za upagazi babu zetu wakati wa vita bado lipo hali kadhalika Bismini na bunduki yake sanamu ile bado tunayo.

Mimi binafsi vyote hivi havinitaabishi hata chembe navitazama kama zilivyo - historia yetu ambayo hatuwezi kuikimbia hata kama tutataka.

Kuhusu Diamond...

Kwa kawaida mwanamuziki akifanya makubwa huwa anawekwa kwenye ''Hall of Fame,'' au sanamu yake inawekwa pale alipokuwa akifanyia muziki wake.

Liverpool ipo sanamu ya The Beatles.
Mephis ipo sanamu ya Elvis Presley.

JS78039909.jpg

images

Nashukuru sana Brother Mohamed Said umetufafanulia vizuri sana kuhusu hili na kuonesha namna gani ile vita ya kwanza Watanganyika walishiriki.
na namna askari hawa Kina Plantam na Kleist Sykes walivo shikiana na Ujerumani dhidi ya Muingereza.
Lakini hii "change of heart" ilivokua inageuka kutokana na hali ya siasa za wakati huo ni jambo lenye mafunzo makubwa ndani yake bila ya shaka kwa wenye kutambua.
  • tumejifunza Wazee hawa vita ya Kwanza walipagana upande wa Ujerumani...

  • Watoto wao vita ya pili walijiandikisha kuwa askari wa Uingereza dhidi ya Mjerumani.

  • Na walipo rudi nyumbani baada ya vita wakawa chachu ya kutaka Muingereza sasa aondoke Tanganyika

Ahsante kwa ufafanuzi huu na haya si ajabu kwa vijana wa mjini walosoma kuwa na free mind..kwani walitarajiwa baada ya kurudi wawe watiifu wa Muingereza lakini ikawa kinyume na wao ndio wakawa mwiba.
wengine wengi walopatiwa fursa za elimu na Muingereza inajulikana walikua upande gani katika harakati hizi za kudai uhuru.

Kuna jambo nilitaka kufahamu ingawa hapa sio mada yake lakini hawa Babu wa Maunda Plantam na kina Abbas Syskes Kleist hawa ni wazulu na askaari watiifu wa Mjerumani bila ya shaka walingia hapa ama wakiwa ni vijana wakikristo au hawana dini....suala langu waliufikaje Uislam ? maana baadae wao na watoto wao walikua watetezi wakuu wa waislam kwa ujumla.
ningependa kufahamu hili hapa au kama utatufungulia mada nyengine na uni tag
 
Sykes Mbuwane
alikuwa ni shemeji yake Affande Plantan.
Hawa walikuwa wameoleana toka huko walikotoka.

Sykes Mbuwane alikuja Tanganyika akiwa na ndugu yake
akiitwa Ally Kattini.

Huyu Ally Kattini alikuwa kipofu.
Ally Kattini baadae alirejea Mozambique.

Kleist alipomzaa mwanae wa pili akampa jina la baba yake
huyu mdogo Ally Kattini.

Ramadhani Mashado Plantan aliingia Tanganyika kutoka
Mozambique kunfuata baba yake Affande Plantan akijulikana
kwa majina hayo.

Halikadhalika kaka yake Abdillah Schneider Plantan siku zote
akijulikana kwa majina hayo.

Wajerumani walikuwa ana kawaida ya wao kutoa majina na kufanya
tasjila ya watoto wa askari wao na wakiwapa majina ya Kijerumani
kama unavyoona Kleist, Schneider, Sykes nk.

Baba zao hawakuyataka majina yale na kama ilivyo ada katika Uislam
wa kutoa majina mazuri ya Kiislam wakawa wanawapa majina kama
Uislam ulivyoelekeza.

Ndiyo unaona Mashado jina lake Ramadhani, Kleist jina lake Abdallah,
Schneider jina lake Abdillah.

Sijapata ushahidi wowote hata wa kusikia kwa wazee wa Dar es Salaam
kuwa hawa Wazulu walioingia na Wissman walisilimishwa.

Akina Said Kastiko, Hassan Machakaumo ambao hawa baba zao
walikuja na Wissiman siku zote katika maisha yao walikuwa wakijulikana
kama Waislam.

Kilichowafanya watu kidogo wasiowajua wawashangae ni kuwa takriban
hawa Wazulu wote walikuwa na majina ya Kikristo na sababu yake nimeeleza.

Kubwa ni kuwa Wazulu hawa walitoa mchango mkubwa katika dini ya Kiislam.

Kleist aliasisi Ali Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika na kujenga shule kusomesha
watoto wa Kiislam na Schneider alikuwa katibu wa Daawati Islamiyya (Muslim
Call) chini ya uenyekiti wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir.
 
kosa la huyu mbunge ni hajaweza kuyaorganize mawazo yake, alikuwa na point ila kabugi kwenye mfano, kwa dimond hapana.
 
Nimegundua akili yako inahitaji kueleweshwa au kuwekewa mambo mengi ili angalau uonekene umekuwa mtu wa miaka 18.
Madini mengi hupatikana ardhini sijui mantiki ya hao watu wanaochimba madini kisha kuyachenjua halafu wanayafukia chini? Kama hawakuwa na uwezo wa kuondoka nayo wasingeyachimba bali wangeweka alama ya eneo ambapo madini hayo hupatikana.
Napenda kuwalaumu watu wote wameoshiriki kukuongoza katika kuchangia mada huku mpangilio wako wa mawazo haujakaa sawa na kushindwa kukurekebisha. Kufanya kosa ni sehemu ya kujifunza iwapo utarekebishwa. Endelea kuwa mdadisi kidogokidogo utafanana na wenzio.
wewe ndio unatakiwa kuelewesha na povu jingi unalotoa.alama walioweka ili watanzania wasijue nini Kinaendelea.wewe vipi povu sijui jiki.

Alama waliweka baadhi ya maeneo, lakini si hizi unazosema wewe. Halafu hii mada iliyokuwa ikijadiliwa na haya unayojibu unafikiri upo sawa?
 
Mnara wa Askari Kwa kiwango chochote huwezi kufananisha na diamond

Historia haitunzwi kwa sababu tu inaeleza mambo mazuri, bali inatunzwa kwa sababu inaeleza matukio muhimu ambayo vizazi vijavyo vinatakiwa kujua ili kuepuka au kuboresha mambo fulani kwa ustawi mzuri wa jamii.

Tanganyika ilishiriki vita vya dunia na baadhi ya washiriki walipoteza maisha. Hata kama kipindi hicho nchi ilikuwa chini ya ukoloni haiondoi ukweli kuwa wapo watu walipoteza maisha wakiwalisha mchango wa Tanganyika katika vita hiyo.

Leo hii mtu anapofananisha uzito wa sanamu na hiyo na Diamond ni wazi kama Taifa tuna tatizo.

Kama wanaona Diamond kafanya makubwa sana nashauri wamjengee sanamu Tandale.
 
Hoja hizii Nizakupoteza Muda..

Mnamjadili/jadili hoja Mfuu za Kilaza wa komban.i
Huyu ni wakumpuuza..na siku zote wanasema mpumbafu hupuuzwa..
 
Wanachadema wanjua at ile ni sanamu ya wapigania uhuru wa tanganyika na wengine hudhani kuwa ile ni sanamu ya mayunga . Hili ni kosa kubwa hapa kwetu tunacho kizazi cha nyumbu kinacho haribu taifa letu

kama kiongozi wa vyama alipata division zero unategemea wafuasi wawe na akili gani ni suala la kupita pale na kuliangalia na kusoma:

ishu ya huyu diamond mtoboa pua mm siiungi mkono
sasa na wewe hapo ndio umetoa wazo gani?
umecomment nini sasa hiv umekisoma kwanza ulichokiandika kabla ya kukiruhusu??

nonsense
 
Aisee,

Inawezekana ikawa hivyo, nadhani uchunguzi wapaswa kufanyika.
mjerumani ameficha maboxi ya madini.hipo siku watakuja kununua au kuingia ubia ili wachimbue hapo.maana ni mjerumani ndie aliweka hizo kumbukumbu.

swissme
 
Historia haitunzwi kwa sababu tu inaeleza mambo mazuri, bali inatunzwa kwa sababu inaeleza matukio muhimu ambayo vizazi vijavyo vinatakiwa kujua ili kuepuka au kuboresha mambo fulani kwa ustawi mzuri wa jamii.

Tanganyika ilishiriki vita vya dunia na baadhi ya washiriki walipoteza maisha. Hata kama kipindi hicho nchi ilikuwa chini ya ukoloni haiondoi ukweli kuwa wapo watu walipoteza maisha wakiwalisha mchango wa Tanganyika katika vita hiyo.

Leo hii mtu anapofananisha uzito wa sanamu na hiyo na Diamond ni wazi kama Taifa tuna tatizo.

Kama wanaona Diamond kafanya makubwa sana nashauri wamjengee sanamu Tandale.
ukweli kaka tuna tatizo kubwa sana kama taifa, yaani ni aibu ya kiwango cha juu sio tu kwa huyo mbunge bali hata wanainchi anao wawakilisha, kauli yake inadhiirisha kwamba watanzania wanaongozwa na watu wasiojua hata historia ya matukio nadra ya nchi yao pamoja na umuhimu wa kutunza kumbu kumbu ya matukio hayo, kwa maana hiyo ina generize hata hao anawaongoza ni mabongo lala..

sidhani hata ukinda BRONX utakuta kuna sanamu ya JAY Z inayotambulika kma alama moja wapo ya kiserikali pamoja na yote alioufanyia mziki.
 
Macos,
Ahsante sana kwa kunitaja katika hii mada ya Picha ya Bismini na kuniomba
nichangie

Wakati wa Vita ya Pili ya Dunia (1914 - 1918) Tanganyika ilikuwa chini ya
utawala wa Wajerumani.

Sanamu hii ya Bismini ni kwa ajili ya kuwakumbuka askari wa waliopigana
upande wa Muingereza dhidi ya Mjerumani.

Hii ni kumbukumbu ya babu zetu askari na wapagazi Waafrika ndani ya jeshi
la Muingereza.

Kama ulivyosema ni kuwa awali ilikuwapo picha ya Herman Von Wissman.

Wissman ndiye aliyeongoza vita dhidi ya wananchi wa Tanganyika kwa kuleta
askari mamluki Wanubi kutoka Sudan na Wazulu kutoka Mozambique.

Katika hawa Wanubi maarufu katika askari hawa katika mji wa Dar es Salaam
ni Mzee Hamisi baba yake Ibrahim Hamisi mmoja wa waasisi wa African
Association pale ilipoanzishwa mwaka wa 1929.

Mtoto wa Ibrahim Hamisi, Abdallah Ibrahim ni mmoja wa watu niliozungumza
nao katika kujifunza historia ya mji wa Dar es Salaam.

Askari wengine walitoka Congo na mmoja wapo ni babu yangu mkuu Samitungo
Mwekapopo
aliyekuwa katika Boma la Wajerumani Shirati, Musoma.

Katika Wazulu walioingia Tanganyika pamoja na Wissman ambao taarifa zao ziliweza
kuhifadhiwa ni Sykes Mbuwane baba yake Kleist Sykes, baba yao Abduwahid,
Ally
na Abbas Sykes.

Hawa askari wote mamluki walikuwa katika kikosi kilichojulikana baadae kama ''Germany
Constabulary,'' na mkuu wa jeshi hili alikuwa Affande Plantan baba yao Mwalimu
Thomas Saudtz Plantan,
Schneider Abdilllah Plantan, na Ramadhani Mashado
Plantan.

Wakati wa Vita Vya Pili Mwalimu Thomas Plantan ndiye alikuwa rais wa African Association.

Inasemekana huyu Affande Plantan alikuwa ndiye chifu wa Wazulu Mozambique
na ndiye aliyewekeana mkataba na Wissman kuja na jeshi la Wazulu kuiteka Tanganyika.

Katika mswada wa kitabu alichoandika Kleist Sykes (1894 - 1949) kuhusu maisha yake,
Kleist anaeleza kuwa mkataba ulikuwa Wazulu na Wajerumani kuitawala Tanganyika
kwa ushirika.

Wazulu na ujuzi wao katika medani ya vita uliwawezesha Wajerumani kuwashinda
Abushiri bin Salim na Chifu Mkwawa.

Wajerumani ndiyo katika kuonesha shukurani yao kwa Wazulu walimfanya Affande
Plantan
kuwa mkuu wa majeshi yao na wakaliita jeshi hilo ''Germany Constabulary.''

Haya kaeleza Kleist katika mswada wake.

Vilevile waliwajengea shule watoto wa wanajeshi wao ambayo ilikuwa ilipo sasa Ocean
Raod Hospital ambako Kleist alisoma hapo hadi darasa la sita na alipomaliza akaingizwa
katika jeshi pamoja na Schneider.

Wakati wote wa utawala wa Wajerumani Waafrika hawa wakiishi ndani ya kambi ili
kuwatenganisha na wazalendo wa Tanganyika.

Kwa hali hii ya kutoa elimu kwa watoto wa askari katika jeshi la Wajerumani, hawa
wakoloni walifanikiwa kuwanyanyua juu Wazulu na Wanubi kiasi kuwa waliposhindwa
Vita Kuu ya Pili na Waingereza kuja sasa kuitawala Tanganyika, walioweza kupata kazi
za maana katika utawala mpya walikuwa hawa Wazulu na Wanubi ingawa katika vita
ile walipigana dhidi ya Muingereza katika jeshi la Wajerumani.

Watoto wa hawa Wazulu walioingia Tanganyika na Wissman ambao walipigana dhidi ya
Waingereza ambao kumbukumbu zao zimehifadhiwa na akina Sykes na Plantan.

Katika Vita ya Kwanza ya Dunia watoto wa hawa Wazulu walipigana chini ya uongozi wa
Von Lettow Vorbeck aliyekuwa wakati ule ndiye mkuu wa majeshi ya Ujerumani Tanganyika.

Kleist ndiye alikuwa Aide de Camp wa Vorbeck.

Vorbeck alipoona kazidiwa nguvu na majeshi ya Waingereza akishambuliwa na General
Smuts
kutoka Afrika ya Kusini alivuka mpaka akakimbilia Mozambique na baadhi ya askari wake wa Kizulu.

Kleist alikamatwa mateka na akawekwa kambi ya askari mateka Dodoma.

Kitu cha kuangalia ni kuwa hawa watoto wa Wazulu na Wanubi ambao walipigana dhidi
ya Waingereza ndiyo waliokuja kufanya mabadiliko makubwa katika siasa za Tanganyika
katika kudai uhuru kutoka kwa Waingereza, uhuru ambao ni wa nchi ambayo ilikuwa yao
kwa kuhamia na wengine kwa kuzaliwa.

Mathalan Mwalimu Thomas Plantan na nduguze wote hawakuzaliwa Tanganyika walikuja baada ya baba yao kuwa keshajiweka vizuri nchini.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Mashado Plantan alikuja Tanganyika mwaka wa 1905.

Hawa vijana wote wa Kizulu walikuwa katika African Association, Kleist akiwa muasisi khasa na Schneider akiwa mwanaharakati wa kupigiwa mfano kwani aliwataabisha sana Waingereza khasa wakati wa Vita ya Pili ya Dunia (1938 - 1945) kiasi cha Waingereza kuamua kumkamata na kumuweka kizuizini Mwanza alikofungwa hadi mwisho wa vita.

Mashado
yeye alianzisha gazeti, ''Zuhra,'' na ndiyo ilikuwa sauti ya Mtanganyika wakati wa ukoloni.

Kleist ingawa alikuwa karibu sana na Waingereza yeye alijiingiza katika siasa za kuwapinga Waingereza kichinichini na alipounda African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) chama alichokiasisi mwaka wa 1933 na rafiki yake wa Kimanyema, Mzee bin Sudi.

Hawa vijana wa Kizulu katika Tanganyika ile ya 1930 wao wakijiona bado ni askari katika jeshi la Kijerumani na zaidi kwa kuwa wote walikuwa wakikisema Kijerumani kama maji.

Hili jambo bila shaka likiwakera sana Waingereza.

Sidhani kama hawa Wazulu na Wanubi walikuwa wakikerwa na ile sanamu ya kamanda wa baba zao Hermann von Wissman.

Lakini Vita ya Pili ya Dunia ilipoingia Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally walivaa sare za majeshi ya King's African Rifles (KAR) kupigana na Wajerumani ambao walikuwa washirika wa babu na baba yao.

Abdul na Ally walikwenda kupigana Burma dhidi ya Wajapani na wote wawili walipewa medali ya ''BurmaStar,'' na Waingereza baada ya kwisha vita mwaka wa 1945.

Hizi ndizo athari za ukoloni.
Kumbukumbu hizi tuzichukulie kama kumbukumbu katika historia ya Tanganyika.

Soko la Kariakoo ambako ndipo Waingereza walipokuwa wakiwaandika kazi za upagazi babu zetu wakati wa vita bado lipo hali kadhalika Bismini na bunduki yake sanamu ile bado tunayo.

Mimi binafsi vyote hivi havinitaabishi hata chembe navitazama kama zilivyo - historia yetu ambayo hatuwezi kuikimbia hata kama tutataka.

Kuhusu Diamond...

Kwa kawaida mwanamuziki akifanya makubwa huwa anawekwa kwenye ''Hall of Fame,'' au sanamu yake inawekwa pale alipokuwa akifanyia muziki wake.

Liverpool ipo sanamu ya The Beatles.
Mephis ipo sanamu ya Elvis Presley.

JS78039909.jpg

images
nakushukuru sana kaka..... barikiwa mnoo
 
Lizarazu,
Amin kwa sote.
ukweli kaka tuna tatizo kubwa sana kama taifa, yaani ni aibu ya kiwango cha juu sio tu kwa huyo mbunge bali hata wanainchi anao wawakilisha, kauli yake inadhiirisha kwamba watanzania wanaongozwa na watu wasiojua hata historia ya matukio nadra ya nchi yao pamoja na umuhimu wa kutunza kumbu kumbu ya matukio hayo, kwa maana hiyo ina generize hata hao anawaongoza ni mabongo lala..

sidhani hata ukinda BRONX utakuta kuna sanamu ya JAY Z inayotambulika kma alama moja wapo ya kiserikali pamoja na yote alioufanyia mziki.
Lizararazu,
Kumbukumbu kwa za wanamuziki zinakwenda na uzito wa huyo msanii.

Na hizi kumbukumbu si kuwa zinawekwa tu ni lazima iwepo sababu ya
kufanya hivyo.

Kumbukumbu haiwekwi mwenyewe akiwa bado anaishi huwekwa baada
ya kifo chake.

Kama ulivyosema viongozi wetu wengine wana upeo mdogo wa kuelewa
mambo.

Umetaja Bronx na Jay Z.

Ipo kumbukumbu ya John Lennon aliyekuwa mmoja wa Beatles New York,
Manhattan Central Park.

Kumbukumbu hii iliwekwa na mkewe Yoko Ono baada ya kifo cha mumewe.
Hapo chini ni Lennon Memorial na kumbukumbu yake imeandikwa, ''Imagine,''
moja ya nyimbo zake maarufu.

V_gcid4vIR8JwieVTZ-Xw9Yntp1nhGhF6yR4mb5oAbFMtVhO6d9rRcibASFidXXVdsYClFKE2XP3GUBCbfnTSWfoNh4T61WUGYllr9sAmH7esWT0cE8uZ9Vma8KCxj2hQNG0UHnZhvnNe8ozLnGzmSxwvW92Qye9nIfKtm5ebIgZluGSj76eugxMc_5OdrRkdELYcZLH-FFFfhBFYWd0xjUKDQeiwDG-I7TZ5hWEfqpUABKid6h_MnVqd73lRojf5-EVjHKQyod7BCdk9thtycUimhlhKrwHveW2bRncA9xFWu5cx9FIaHmiQ6PJUwLefa6eYj8FUEI2hyE5uxFEPKyeFvRcy_1lgn0gLJSVEibhRdtwWM_4OOE0psFAEH8jrr5t2KO8V1jJYEWAYaWJsVb1q-WeLY1zUaJBf5Y96WVp_AXDaseNqNhR1ETwIXISfmpbpEmT8jyiAy4fUJcUWaifFfStdca6gok9Xi4UdqM6TOQIM1TJUlnvwf66_IOEhRNhNBKuQ9x6aRM892R8k7ZZVugmN0bcBsQKgZKBdVRF7kdExB8IWC7tP_ioScef1S16nQ=w480-h360-no
 
walitumia bunduki

soma history

Sanamu ni sanamu tu. Hapo yabadilishwe maneno tu yaliyoandikwa hapo. na kama tunadhani kuwa sanamu hiyo haituwakilishi kwa sababu hatukuwa na bunduki enzi hizo, basi ichongwe sanamu ya askari mwenye mkuki, na ngao au upinde na ngao...na maneno mahsusi, Basi! Habari ya Diamond, wamchongee Sanamu Tandale na Ulanga!
 
I enjoyed to read your post

captivating and educative
Macos,
Ahsante sana kwa kunitaja katika hii mada ya Picha ya Bismini na kuniomba
nichangie

Wakati wa Vita ya Pili ya Dunia (1914 - 1918) Tanganyika ilikuwa chini ya
utawala wa Wajerumani.

Sanamu hii ya Bismini ni kwa ajili ya kuwakumbuka askari wa waliopigana
upande wa Muingereza dhidi ya Mjerumani.

Hii ni kumbukumbu ya babu zetu askari na wapagazi Waafrika ndani ya jeshi
la Muingereza.

Kama ulivyosema ni kuwa awali ilikuwapo picha ya Herman Von Wissman.

Wissman ndiye aliyeongoza vita dhidi ya wananchi wa Tanganyika kwa kuleta
askari mamluki Wanubi kutoka Sudan na Wazulu kutoka Mozambique.

Katika hawa Wanubi maarufu katika askari hawa katika mji wa Dar es Salaam
ni Mzee Hamisi baba yake Ibrahim Hamisi mmoja wa waasisi wa African
Association pale ilipoanzishwa mwaka wa 1929.

Mtoto wa Ibrahim Hamisi, Abdallah Ibrahim ni mmoja wa watu niliozungumza
nao katika kujifunza historia ya mji wa Dar es Salaam.

Askari wengine walitoka Congo na mmoja wapo ni babu yangu mkuu Samitungo
Mwekapopo
aliyekuwa katika Boma la Wajerumani Shirati, Musoma.

Katika Wazulu walioingia Tanganyika pamoja na Wissman ambao taarifa zao ziliweza
kuhifadhiwa ni Sykes Mbuwane baba yake Kleist Sykes, baba yao Abduwahid,
Ally
na Abbas Sykes.

Hawa askari wote mamluki walikuwa katika kikosi kilichojulikana baadae kama ''Germany
Constabulary,'' na mkuu wa jeshi hili alikuwa Affande Plantan baba yao Mwalimu
Thomas Saudtz Plantan,
Schneider Abdilllah Plantan, na Ramadhani Mashado
Plantan.

Wakati wa Vita Vya Pili Mwalimu Thomas Plantan ndiye alikuwa rais wa African Association.

Inasemekana huyu Affande Plantan alikuwa ndiye chifu wa Wazulu Mozambique
na ndiye aliyewekeana mkataba na Wissman kuja na jeshi la Wazulu kuiteka Tanganyika.

Katika mswada wa kitabu alichoandika Kleist Sykes (1894 - 1949) kuhusu maisha yake,
Kleist anaeleza kuwa mkataba ulikuwa Wazulu na Wajerumani kuitawala Tanganyika
kwa ushirika.

Wazulu na ujuzi wao katika medani ya vita uliwawezesha Wajerumani kuwashinda
Abushiri bin Salim na Chifu Mkwawa.

Wajerumani ndiyo katika kuonesha shukurani yao kwa Wazulu walimfanya Affande
Plantan
kuwa mkuu wa majeshi yao na wakaliita jeshi hilo ''Germany Constabulary.''

Haya kaeleza Kleist katika mswada wake.

Vilevile waliwajengea shule watoto wa wanajeshi wao ambayo ilikuwa ilipo sasa Ocean
Raod Hospital ambako Kleist alisoma hapo hadi darasa la sita na alipomaliza akaingizwa
katika jeshi pamoja na Schneider.

Wakati wote wa utawala wa Wajerumani Waafrika hawa wakiishi ndani ya kambi ili
kuwatenganisha na wazalendo wa Tanganyika.

Kwa hali hii ya kutoa elimu kwa watoto wa askari katika jeshi la Wajerumani, hawa
wakoloni walifanikiwa kuwanyanyua juu Wazulu na Wanubi kiasi kuwa waliposhindwa
Vita Kuu ya Pili na Waingereza kuja sasa kuitawala Tanganyika, walioweza kupata kazi
za maana katika utawala mpya walikuwa hawa Wazulu na Wanubi ingawa katika vita
ile walipigana dhidi ya Muingereza katika jeshi la Wajerumani.

Watoto wa hawa Wazulu walioingia Tanganyika na Wissman ambao walipigana dhidi ya
Waingereza ambao kumbukumbu zao zimehifadhiwa na akina Sykes na Plantan.

Katika Vita ya Kwanza ya Dunia watoto wa hawa Wazulu walipigana chini ya uongozi wa
Von Lettow Vorbeck aliyekuwa wakati ule ndiye mkuu wa majeshi ya Ujerumani Tanganyika.

Kleist ndiye alikuwa Aide de Camp wa Vorbeck.

Vorbeck alipoona kazidiwa nguvu na majeshi ya Waingereza akishambuliwa na General
Smuts
kutoka Afrika ya Kusini alivuka mpaka akakimbilia Mozambique na baadhi ya askari wake wa Kizulu.

Kleist alikamatwa mateka na akawekwa kambi ya askari mateka Dodoma.

Kitu cha kuangalia ni kuwa hawa watoto wa Wazulu na Wanubi ambao walipigana dhidi
ya Waingereza ndiyo waliokuja kufanya mabadiliko makubwa katika siasa za Tanganyika
katika kudai uhuru kutoka kwa Waingereza, uhuru ambao ni wa nchi ambayo ilikuwa yao
kwa kuhamia na wengine kwa kuzaliwa.

Mathalan Mwalimu Thomas Plantan na nduguze wote hawakuzaliwa Tanganyika walikuja baada ya baba yao kuwa keshajiweka vizuri nchini.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Mashado Plantan alikuja Tanganyika mwaka wa 1905.

Hawa vijana wote wa Kizulu walikuwa katika African Association, Kleist akiwa muasisi khasa na Schneider akiwa mwanaharakati wa kupigiwa mfano kwani aliwataabisha sana Waingereza khasa wakati wa Vita ya Pili ya Dunia (1938 - 1945) kiasi cha Waingereza kuamua kumkamata na kumuweka kizuizini Mwanza alikofungwa hadi mwisho wa vita.

Mashado
yeye alianzisha gazeti, ''Zuhra,'' na ndiyo ilikuwa sauti ya Mtanganyika wakati wa ukoloni.

Kleist ingawa alikuwa karibu sana na Waingereza yeye alijiingiza katika siasa za kuwapinga Waingereza kichinichini na alipounda African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) chama alichokiasisi mwaka wa 1933 na rafiki yake wa Kimanyema, Mzee bin Sudi.

Hawa vijana wa Kizulu katika Tanganyika ile ya 1930 wao wakijiona bado ni askari katika jeshi la Kijerumani na zaidi kwa kuwa wote walikuwa wakikisema Kijerumani kama maji.

Hili jambo bila shaka likiwakera sana Waingereza.

Sidhani kama hawa Wazulu na Wanubi walikuwa wakikerwa na ile sanamu ya kamanda wa baba zao Hermann von Wissman.

Lakini Vita ya Pili ya Dunia ilipoingia Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally walivaa sare za majeshi ya King's African Rifles (KAR) kupigana na Wajerumani ambao walikuwa washirika wa babu na baba yao.

Abdul na Ally walikwenda kupigana Burma dhidi ya Wajapani na wote wawili walipewa medali ya ''BurmaStar,'' na Waingereza baada ya kwisha vita mwaka wa 1945.

Hizi ndizo athari za ukoloni.
Kumbukumbu hizi tuzichukulie kama kumbukumbu katika historia ya Tanganyika.

Soko la Kariakoo ambako ndipo Waingereza walipokuwa wakiwaandika kazi za upagazi babu zetu wakati wa vita bado lipo hali kadhalika Bismini na bunduki yake sanamu ile bado tunayo.

Mimi binafsi vyote hivi havinitaabishi hata chembe navitazama kama zilivyo - historia yetu ambayo hatuwezi kuikimbia hata kama tutataka.

Kuhusu Diamond...

Kwa kawaida mwanamuziki akifanya makubwa huwa anawekwa kwenye ''Hall of Fame,'' au sanamu yake inawekwa pale alipokuwa akifanyia muziki wake.

Liverpool ipo sanamu ya The Beatles.
Mephis ipo sanamu ya Elvis Presley.

JS78039909.jpg

images
 
View attachment 348239

Wandugu huyu Mbunge ameonekana kituko.kituko kwa kutaka Diamond awekwe badala ya Picha ya askari nadhani ni utoto zaidi..Ila mimi nimeona hoja yake inaibua mjadala mpana kuhusu picha ile na Tanganyika.
Jee sanamu ile ni ya nini ?

Huyu mbunge ametufunua wengi kuhusu ile sanamu. Ni sanamu ya askari wa malkia wa UK alopigana kumuondoa mzungu mwenzie wa Kijerumani. Yule ni mwafrika , mwafrika alotumiwa na wakoloni hivyo nawwza kumwita alikua upande wa wakoloni wapo askari wabeba miziko au wapagazi walo andikwa katika placard ya pale. Lakini hawa sio mashujaa wa Tanganyika hata kama ni waafrika...hawa walipigana upande wa mkoloni muingereza dhidi ya mkoloni mjerumani hawa ni puppets sio wazalendo.

Naibua mjadala huu kwa makusudi na mbunge yule amechokonoa hoja ya msingi kabisa japo yeye kaleta uchepe.

Wafrika wa nchi hii walopambana na wakoloni ni Kinjekitile, Chief Mkwawa, Bushiri. Hawa walipoteza maisha yao kuilinda Tanganyika dhidi ya Ukoloni hawa wanastahiki kabisa stutue zao kusima pale tena za dhahabu ...na mtag ndugu yangu Mwanahistoria Mohamed Said aje nae atie mchango wake kuhusu hili

Wakoloni walitufanya wanaserere hata historia zetu tukazitia kwenye kapu na kutukuza za kwao.

Mwanzo ilikua picha ya askari wa kijerumani Major Hermann von Wissmann Waingereza waliindoa pamoja na Ya Bismack na Karls Peter

Sanamu Hii ya sasa , Ilizinduliwa Rasmi Dar es salaam hapo ilipo Mwaka 1927. Sanamu Hii imetengenezwa kwa shaba na imechongwa na James Alexander Stevenson.

Kabla haija letwa Dar es salaam iliwekwa kwa maonesho katika Royal Academy , London.

Tujaribu kusoma historia , kama hujui historia ya sanamu ile unakua saw ana huyo Mbunge . Hapa tunatakiwa kuijadili ile sanamu kama jee ibaki kama ilivo ambapo askari Puppet alo pigana upande wa Mfalme wa Uingereza dhidi ya Kals Peter wa Ujerumani ina maana yoyote Kwetu.

Jee si wakati mzuri wa kuwaenzi Kinjekitile, Abushiri na Mkwawa walopigana dhidi ya Ukoloni ? Hii ni hoja moto

Hii ni mada moto , hard talk kila mtu ajadili hili .

View attachment 348240

**USHAURI WANGU WA BURE KUHUSU PUBLIC SPEAKING**
mimi binafsi naonelea ni vema kama wabunge wangekuwa na utaratibu wa kupewa kozi ama mafunzo maalum ya muda mfupi (ikiwezekana yawe endelevu) na ikiwezekana pia iwe kwa viongozi wote wa ngazi za juu wa serikali kwenye suala zima la public speaking.

hawa watu wakubwa ila bado hawapo vizuri sana katika mbinu ya kuwasiliana mbele ya kadamnasi ya watu kupitia matamshi yao hata body language. ukishakuwa kiongozi wa umma, wewe ni mtu wa kutazamwa muda wote. unakuta mtu ni kiongozi wa ngazi za juu, lakini bado anaongea mambo kwa mazoea tu bila kujua watu na jamii wanamuangalia muda wote. kosa dogo tu, unatengeneza vichwa vya habari, na ukizingatia karne hii ya sayansi na teknolojia dunia nzima inatutazama.

bado wanasisa na viongozi wengi wanazungumza kwa sauti na lugha ya mwili za mitaani tu kwa mazoea sana hapa tanzania tuna wataalamu wengi sana wenye hii taaluma ambao wanaweza kutoa msaada sana kwa hili.
**NINAWASILISHA**
 
Back
Top Bottom