Hatua ya kumpata mchumba wa ndoa ni ngumu

Hakuna cha mvumilivu kula mbivu. Anakupumzikia huyo.
Nakushauri kabla hujaoa atleast uwe na wasichana kama watatu au wanne pembeni ili ufanye uchaguzi sahihi.
Ukiwa na mmoja huyohuyo unakuwa myopic. Mapenzi yanakufunga macho huoni upande wake wa pili.
Ushauri mbovu huu
 
Dah ,,,kuna watu wanapendwa kweli wanazingua ...jamani mim kila wakati nimelia zaidi ya mara mbili kwa kuumizwa then nikaamua kumove on ...nataman hata kupata wakunifuta machozi lakin bado ni wasanii halafu huyo anapendwa lakin anazingua naumia ,,,khaaaa natamani ningependwa mim ...kweli ngombe wa maskini hazai
kwenye miti hakuna wajenzi
 
Mwanamke akishakwambia anamtu, uwe makini,kwani huenda namsururu,na anatengeneza mazingira ya, ikiwa utamkuta na yeyote hata kitandani, akwambie "nilishakwambia nna mtu", vinginevyo akutajie kabisa ni nani.

Pia wa hivyo anasubiri ada-mpiwe ndo aje kwako.
 
Habari wana MMU,

Siku zote huwa naamini katika kumuandaa mwanamke wa ndoa na maisha. Umri wangu ulipofika napaswa niishi na mke sasa, maana kama maisha pakuanzia papo. Siku za nyuma nikiwa shule mabinti nilishawahi kuwa nao wote niliotengeneza mazingira yakuwaandaa leo hii wameolewa kwani mimi nilikuwa sisomi sina kazi hivo hata waliponiitaji nitamke neno nilikuwa kimya maana nikawa sioni lini maisha nitatoboa. Na wengine nilipendwa ila nikakwepa kwakutumia kigezo cha kazi kwani hata sikuwapenda kivile.

Ila nimeingia kazini sasa, kuna binti ambaye nimempenda na natamani nimuweke ndani lakini, amekuwa ni mgumu kufanya maamuzi, akidai ana mtu ila matamanio yakuolewa anayo sina mapenzi ya kisanii, ila nimekuwa mkweli kwake muda wote na uwezo wakukomaa nikapata mtu mwingine ila kwakulazimisha nafsi sana. Nawaza moyoni, nimeongea naye karibia mara tatu kwa muda tofauti na sasa nimemaliza mwaka mmoja toka nianze kuwasiliana naye je kuna siku atabadili msimamo wake nakuja kwangu? Au ni sawa nakusubiri mvua kipindi ambacho nikiangazi?

Ni mtu ambaye tunashirikishana maswala mengi yakimaisha nakusaidiana kwa kiasi chake. Namuheshimu na ananiaheshimu pia, ila when it comes to that point dah! Maumivu ni kwangu kama kuna wenye mfano na matukio kama haya basi tupeane uzoefu labda nikichuja utanisogeza kama huna la kuongea soma upite tu, kejeli mwiko hapa.
Ukinipa sababu ya kumpenda Huyo msichana nitakupa ushauri
 
Mbali na kumuomba Mungu, ninachoamini mimi ni kuwa mwanamke au mume haandaliwi kama inavyotafsirika na watu ukiondoa utamaduni wa zamani wa wazazi wetu, mwanamke au mume huja accidentally ingawaje kumpata aliye na maadili mema itategemea na malezi aliyoyapata kutoka kwa wazazi/walezi wake, kama ukikosa mwenye maadili mema basi hilo litakuwa ni jukumu lako wew kama mwanaume au mwanamke kumfanya mwenzako awe mwenye maadili mema kama msemo usemavyo usione vyaelea vimeundwa.
Kama kweli wewe una nia ya dhati, mwambie huyo mwanamke heri elfu moja aliyonayo kuliko laki moja ya ahadi, mapenzi haya hayatabiriki anayemtegemea awe naye makini sana, kama unamtaka kweli mwambie unataka kupeleka mahari kwao kwisha habari!!
 
Suala gumu sana hili.Wengi wamekata tamaa nikiwepo mie,sijui kama nitaoa.Imebidi nikae tu sasa.
 
Back
Top Bottom