Hatimaye Assad na familia yake wamewasili Moscow, Urusi

Assad na familia yake wamefika salama Moscow. Serikali ya Urusi yawapa hifadhi kuishi humo kwa muda wote.

===

Syria’s Bashar al-Assad and his family have arrived in Moscow and have been granted asylum by the Russian authorities, Russian news agencies report, citing a Kremlin source.

The Interfax news agency quotes the unnamed source as saying: “President Assad of Syria has arrived in Moscow. Russia has granted them (him and his family) asylum on humanitarian grounds."

Times of Israel
Wakiwachoka watawakabidhi kunakohusika
 
Russia wanafiki sana au Hawana Nguvu waliyokua wanatuambia Wanayo!!! Kila mahala Russia kavurugwa na hana msaada nchi zote ally wake zimechakazwa sanaa..Anzia Libya, Iraq,Syria, LEBANON imebakia Iran tu na Korea ambao naamini Wanazilia timing wazipige ....Ili Wamtese wamemweka yeye mwenyewe kati na kibaraka anaitwa Zelensky hivi kweli Russia wala KGB wameshindwa kumalizana na mtu kenge kama Zele??? Anaruka ruka pale wameshindwa kummaliza???
Naamini hata Iran na Hizbollah wameanguka kabisa kijeshi
Russia ukiona anapigana sehemu basi jua anapiga na umoja wote wa Nato na vibaraka wote wa marekani kwahiyo sio kazi ndogo. Na kama angekua dhaifu Ruassia ingelikua imeshafutwa kwenye uso wa dunia hivyo kumbuka hilo mkuu.
 
Ila wewe jamaa yetu hua huna misimamo kabisa.
Hivi unajua Assad amekuwepo madarakani kwa karibu miaka 30 kwa msaada wa ulinzi wa Urusi na Iran.
Utawala wa Obama ukitaka kumtoa Urusi wakamkingia kifua,utawala wa Trump wakajaribu kumtoa wakashindwa na Sasa mwishoni kabisa utawala wa Biden wameweza.
Hivi unadhani Urusi wangeweza kupigana vita ngapi dhidi ya Mataifa mangapi?
Asada amepinduliwa kwa muungano wa USA ,France,UK, Turkey,Israel,saud Arabia na Some Arabs,vikundi vitatu vya waasi na hata baadhi ya wanajeshi wake hawakutaka kupigana safari hii Kwa moyo wote.sasa Urusi na Iran wanawezaje kukabiliana ana umoja wote huo wakati Urusi nae ana vita nyumbani kwake?
Nakuambia hivi,Hali hii hata Marekani asingeweza.
Urusi na Iran wamemlinda sana Assad sema basi TU.
Hata hivyo waliomuondoq wamevizia Urusi akiwa bize na vita yake.kabla ya hapo Assad alikua sana madarakani.
Watu wanatanguliza hisia kuliko fact,sehemu yoyote anapopigana urusi jua anapigana na mataifa yote ya NATO na viabaraka wa marekani. Russia kama angekua dhaifu leo pengine ingelikua imefutwa kwenye uso wa dunia.
 
Inamuathirije kisaikolojia? Unafikiri Assad ataishi maisha ya kikimbizi makambini na kula chakula cha UNHCR? Jiulize kwa nini ameenda Russia? Assets zake nyingi na vibunda vyake vipo Russia na Hong Kong
Hakuna mkimbizi ambaye huwa ana amani kwa kuishi uhamishoni kwa nguvu. Ni sawa upelekwe gerezani, upewe chakula kizuri na mahali pa kulala vizuri, halafu eti useme kuwa utakuwa na amani.
 
Assad na familia yake wamefika salama Moscow. Serikali ya Urusi yawapa hifadhi kuishi humo kwa muda wote.

===

Syria’s Bashar al-Assad and his family have arrived in Moscow and have been granted asylum by the Russian authorities, Russian news agencies report, citing a Kremlin source.

The Interfax news agency quotes the unnamed source as saying: “President Assad of Syria has arrived in Moscow. Russia has granted them (him and his family) asylum on humanitarian grounds."

Times of Israel
Kumbe taarifa ya ndege yake kupigwa kombora was misleading kwa adui zake
 
Russia ukiona anapigana sehemu basi jua anapiga na umoja wote wa Nato na vibaraka wote wa marekani kwahiyo sio kazi ndogo. Na kama angekua dhaifu Ruassia ingelikua imeshafutwa kwenye uso wa dunia hivyo kumbuka hilo mkuu.
Hakuna nchi mwanachama wa NATO iliyowahi kupigana na Russia. Mataifa ya Magharibi huwa wanaipiga Russia kwa akili siyo maguvu.

Ni kama kwa sasa wanavyoisaidia Ukraine. Ukraine inachangiwa gharama za vita na mataifa mengi, huku Urusi ikilazimika kugharamia vita pekee yake. In long run, Russia inaathirika kwa kiwango kikubwa maana wakati mataifa ya Ulaya Magharibi yanaendelea na mipangio ya maendeleo ya mataifa yao, Urusi muda wote inahangaika na vita pekee.

Kwa namna hiyo, mataifa ya Ulaya yalifanikiwa kuisambaratisha iliyokuwa USSR, kiasi cha Urusi kulazimika mpaka kuomba msaada wa kifedha ili kujinusuru na kufilisika kabisa. Ni mataifa ya Magharibi ndiyo yaliyoisaidia Urusi lakini masharti yalikuwa magumu, na mwisho muungano wa Soviet ukafa, na leo zilizokuwa states za USSR zimekuwa mataifa adui dhidi ya Urusi. Na karibia mataifa hayo yote yanataka kuwa sehemu ya mataifa ya Magharibi.

Hakuna taifa la Magharibi linalojihangaisha eti na kulifuta Taifa lolote Duniani, achilia mbali hiyo Russia. Hizo fikra za kufuta Taifa huwa zipo kwa wale magaidi punguani wa mashariki ya kati na nchi ya Iran, wanaosema kuwa kuna siku Israel wataifuta kwenye uso wa Dunia. Nchi za Magjaribi zingrkuwa na dhamira ya kuyafuta baadhi ya mataifa si zingefanya hivyo enzi za ukoloni? Ni nchi gani walizifuta?
 
Waasi wanashidaje bila kuwa na ndege, na silaha bora? Assad ana kila kitu toka Urusi na Irani na bado kashindwa!!! 😏
 
Hakuna mkimbizi ambaye huwa ana amani kwa kuishi uhamishoni kwa nguvu. Ni sawa upelekwe gerezani, upewe chakula kizuri na mahali pa kulala vizuri, halafu eti useme kuwa utakuwa na amani.
Nani alikwambia Assad mkimbizi?

Yuko zake Moscow na mkewe watoto wanasoma China

Huyo mtu utamuita mkimbizi?
 
Urusi alikuwa na maslahi gani katika vita vya Syria?
 
Back
Top Bottom