Hapa Makongoro Nyerere kaamua kusema ukweli mbele ya Rais bila kupepesa macho

..Warioba alishiriki kampeni za Ccm 2015 na 2020.

..alishuhudia kwa macho yake kampeni za matusi, ubaguzi, na ukabila, zilizokuwa zikifanywa na Ccm.

..angekuwa na msimamo wa dhati angejiweka mbali na Ccm, lakini yeye aliendelea kuwa nao karibu.

..hata sasa hivi ukimsikiliza Mzee Warioba hayuko tayari " kumvika paka kengele ,"na kueleza bayana unyama waliofanyiwa wapinzani.

..kwao Mzee Warioba, mkoa wa Mara, ni moja ya eneo ambako wapinzani wamefanyiwa mambo mabaya kupitiliza, lakini Mzee badala ya kuwatetea wananchi ananyenyekea na kuwasitiri watawala.
Mzee Butiku namkubali ni straight forward. Hamunghunyi maneno au kuogopa.
 
Jamani! Jamani! Jamani!

Yaani Mzee Warioba ajitoe mhanga namna hii kweli, kwa lipi? Mbona mnamtwisha zigo mzee wa watu!

Kwanza ni kwa uwezo gani ambao pengine mnadhani anao?

Huo uwenyekiti wa tume si alipewa tu, kama ambavyo anaweza kupewa mtu mwingine leo…. au alishinda tenda kwa uwezo maalumu!

Pengine mimi simfahamu vizuri, mbali na kuwa Jaji na Waziri Mkuu mstaafu…. ana uspesho gani wa kutingisha mhimili?

Yuko pale kwa maslahi yake na familia, watoto wake wapo kwenye system…. anatuchora tu.

Mwacheni amalizie uzee wake kwa utulivu, hajasahau yaliyowakuta wanzake kina Lowassa na Sumaye.
Mzee Warioba sawa tu kunyamaza aliishapata shubiri ya akina Makonda kipindi kile kwenye kongamano! Mtu mwenye ujasiri kidogo ni Prof Shivji
 
Mzee Butiku namkubali ni straight forward. Hamunghunyi maneno au kuogopa.
..wakati Magufuli yuko hai Warioba na Butiku walikuwa wameuchuna huku wapinzani wakiteswa na kubaguliwa waziwazi.

..Mimi nawasifu Sheikh Ponda na Askofu Mwamakula kwa kutetea haki when Magufuli was alive and it was risky to do so.

..Mwingine ni Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samata yeye alisema mbele ya Magufuli kwamba utawala wa sheria hauzingatiwi na wateule wa Raisi.
 
..Watawala wetu wanajua kwamba Watanzania tunamheshimu na kumpenda Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

..Kwa hiyo watawala wameamua kumteua Makongoro ili kujiweka karibu na jina na heshima ya Mwalimu Nyerere.

..Pia miradi mbalimbali imepewa jina la Mwalimu kwa kisingizio cha kumuenzi na hiyo ni mbinu ya kuzuia wananchi kuhoji tija, au uhalali, wa miradi hiyo.

..Kwa mfano, yeyote atakayehoji lolote kuhusu ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere yuko ktk hatari ya kuzushiwa kwamba anapinga fikra / ndoto za Mwalimu, au hataki Mwalimu aenziwe.

..Kwa ujumla kinachoendelea ni mkakati wa watawala kutufanya wananchi wa kawaida MAZUZU.

Cc Kalamu1
 
Hawa watoto wa Nyerere sio chawa, hawajipendekezi kwa viongozi ili wapewe chakula, baba yao alishawakomaza waishi kibishi toka miaka hiyo. Kwa sasa watawala wanawapa madaraka ili kuficha aibu ya watoto wao au wa marafiki zao wanaowabeba.

Tatizo ni watoto wa hiki kizazi kipya, kilichozoeshwa kuwepo serikalini karibia awamu zote wakiulizwa waoneshe walichowahi kufanya hakuna, na wengi wao wamezoea kubebwa mpaka wanamkasirikia anapokuja asiewabeba, hawaoni aibu.

Wataanza kumchora kwa vikatuni twitter kama vile hii nchi ni ya baba yao, wanajiona wao tu, hawajui kuna watanzania wengine wengi wenye sifa na weledi wa kutosha kushika nafasi walizopo na waka deliver zaidi yao.

Kubebwa kumewapofusha akili zao hawaoni mbele tena, hata wakioneshwa udhaifu wao kiutendaji wanajibu tatizo ni uwaziri wao, ulafi wao umejaa mpaka kwenye akili zao sasa wanadhani kila mkosoaji wao anataka nafasi zao huku "wakiuota" urais.
 
Attachments

  • VID-20220411-WA0005.mp4
    6 MB

Ngoja nikurudishe nyuma kidogo na kukumbusha: Makongoro mwenyewe, si aliwahi (2015)? kuutaka u-Rais, lakini hakufurukuta akakatwa ngazi ya chini kabisa ndani ya mchujo wa chama, unakumbuka?

Kiujumla wetu, waTanzania ni MAZUZU sana. Tusingekuwa mazuzu tusingevumilia tawala hizi za siku hizi ambazo hazieleweki na wala hazijui wanachofanya.

Kumuenzi Mwalimu ni kukataa UZUZU.
 
Mkuu Kalamu1,
Wacha tu nirukie...itifaki imezingatiwa

Ndio nashawishi mjadala makini juu ya 'wanasiasa' kama Jaji Warioba-Mh.Makamu wa kwanza wa Raisi na Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkuu 'SYLLOGIST', unashawishi sana pawe na mjadala makini juu ya watu aina ya Warioba.
Ndio.
Nimekusoma kwa uangalifu sana, lakini nikiri kabisa bado sijakuelewa barabara.
Kwa kutoweza kunielewea "barabara" kwa maoni yangu, hakumaanishi wala kusababisha wewe ni baradhuli-haujabisha ushwawishi wangu uliouona wewe.
Kweli kuna sababu nyingi tu za kuwa na umakini katika kujadili 'wanasiasa' kama Jaji J.S Warioba. Wangalau tunaafikiana hapo.
Hoja yako imejikita kwenye mhtasari wa mstari huo hapo juu, na hasa kwenye haya maneno "...Heshima ya nchi yake na heshima Chama." (?)
Nikusahihishe "...Heshima ya nchi yake na heshima ya chama"
Haswa, kwa maono yangu, amekuwa mstari wa mbele kwakuwa ni nyota wa heshima ya nchi na Chama chake CCM-sidhani utalipinga hili- mfano kumekuwa na mitiririko ya Viongozi wa juu, wa Vyama na Serikali wa nchi hii 'kwenda kwake' kwa sababu wanazozijua wao. Kwa maoni yangu, ni kwasababu ya tunu ya heshima ya nchi aliyokuwa nayo na unguli wa Kisiasa nje na ndani ya Chama chake cha CCM, pamoja na kuonekana utofauti wa mihimili na misimamo ya sasa ya CCM, Mzee Warioba, again, bado ni mmoja wa wengi mwenye mhimili na msimamo wa Kale wa CCM wa kujikomboa na fikra za kiafrika.
Kuhimiza uwepo wa Katiba Mpya ni kupingana na 'Heshima ya nchi'?
Hapo juu Mkuu Kalamu1 sijakuelewa, unauliza rhetorically? Je ni wewe unayohimiza au ni Jaji Warioba?-Au yeye Warioba kuhimiza katiba 'kwa mantiki ya "woga" wake-atakuwa anankinzana na utunzaji wa... Heshima yake ya Nchi na ya CCM? Sijui, lakini nafikiri unaweza kunielewesha.
CCM kama chama, baada ya yote kilichokwishapitia chama hicho toka enzi za Mwinyi hadi leo hii, bado Mzee Warioba na wazee wengine, kweli bado wanaona kuna "Heshima" ndani ya chama hicho, inayowafanya wasiseme lolote juu yake, kweli?
Kwangu mimi naona swali hili litanilengesha kujibu nisoyoyajua. Siwezi kukujibu-nafikiri ulielekeze kwa hao wazee-lakini inajulikana wapo wazee wengi tu amabao wanasema mengi(lolote) kuhusu 'Heshima' ya CCM
Mkuu inawezekana sijaelewa vyema na kuzoea jinsi ya muwasilisho wako wa hoja, ndiyo sababu ninashindwa kukuelewa vizuri unachoandika hapa.
Lakini ninaheshimu sana ulivyowasilisha hoja zako. Natamani tu kama ningeelewa maana hasa ya unachonuia kueleza.
Kutonielewa 'vyema' na muwasilisho wa "hoja" haukufanyi wewe ni baradhuli, kwani sio kawaida ya mijadala mitandaoni kuwasilisha hoja kwa mpangilio au kuwa na hitimisho linalofuata mantiki. Nilikurupuka.
Kwa bahati nzuri, umemtaja pia Salim katika andiko lako, na kwa bahati nzuri, huyo pia nilisha mtaja pia ndani ya mijadala humu JF katika maudhui kama haya haya tunayoyajadili hapa leo.

Bado kabisa ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kwamba watu wenye hadhi kama ya Warioba, hawana chochote cha kupoteza, ila wana kila kitu cha kuwapa heshima kubwa ndani ya Taifa hili, kama wangesimamia na kueleza wanachokiamini juu ya maslahi ya nchi hii.

Sielewi maana ya kuwa "Nguli wa Siasa za nyakati" zinavyosaidia chochote kwa ukimwa wake.
Sawa.
"Strategic", kwa vipi? Hapa nadhani umeniuzia tu maneno bila ya kujali nitaelewa au la!
Ha ha naona ni kweli nilifanya bila ya kuzingatia, lakini sio kwa kusudi la kuuza neno au maneno. "Werevu' that is the word!🤔

Kalamu1 tukitumia kichwa cha bandiko na maudhui ya mleta mada-tuko nje. Tukubaliane hapo.

Kilicho kuwepo kwenye maudhui, kwa maoni yangu, ni tofauti na mjadala wetu hapa. (Kuhusu aina ya Wanasiasa kama Warioba)
Kitu tunaweza kuafiki ni kuwepo mjadala makini kuhusu "aina" ya watu au wanasiasa kama Warioba?

Naomba nikiri pia-Nilikurupuka na kuingilia swali uliloelekeza kwa JokaKuu bila ya kujijua-nilikurupuka! Sikuwa nimenuia hivyo, kuingilia hoja mlizoziibua kati yako na mzee JokaKuu. Kumradhi

Ukifika wakati muafaka niko tayari tukajadiliana, nje ya mada hii.
Ahsante
 
Hawa watoto wa Nyerere sio chawa, hawajipendekezi kwa viongozi ili wapewe chakula, baba yao alishawakomaza waishi kibishi toka miaka hiyo. Kwa sasa watawala wanawapa madaraka ili kuficha aibu ya watoto wao au wa marafiki zao wanaowabeba.

Tatizo ni watoto wa hiki kizazi kipya, kilichozoeshwa kuwepo serikalini karibia awamu zote wakiulizwa waoneshe walichowahi kufanya hakuna, na wengi wao wamezoea kubebwa mpaka wanamkasirikia anapokuja asiewabeba, hawaoni aibu.

Wataanza kumchora kwa vikatuni twitter kama vile hii nchi ni ya baba yao, wanajiona wao tu, hawajui kuna watanzania wengine wengi wenye sifa na weledi wa kutosha kushika nafasi walizopo na waka deliver zaidi yao.

Kubebwa kumewapofusha akili zao hawaoni mbele tena, hata wakioneshwa udhaifu wao kiutendaji wanajibu tatizo ni uwaziri wao, ulafi wao umejaa mpaka kwenye akili zao sasa wanadhani kila mkosoaji wao anataka nafasi zao huku "wakiuota" urais.
Yule mwingine mlevi yuko wapi siku hizi?

Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom