Hapa Makongoro Nyerere kaamua kusema ukweli mbele ya Rais bila kupepesa macho

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,924
4,484
Hii kauli ni kubwa sana. Kuwa watoto wa viongozi wanapata nafasi si kwa sababu wamewahi fanya matendo makubwa ila ni sababu tu ya majina ya watoto wao.

Nadhani alikuwa anamaanisha yeye, Ridhwani Kikwete, Januari Makamba, Nape Nnauye n.k

Anasema wao wapo hapo ukisema utafute walichofanya mpaka kuwepo hapo utatafuta mpaka ukome. Ila ndo wapo sababu ya wazazi wao.

Sisi tunaokesha JF kuipigania CCM ni lini tutafika huko? Angalau nasi mtukumbuke jamani MNAPOLAMBA ASALI. KWA SASA MAKAMBA ANASEMA NI KULAMBA ASALI TU KWA KWENDA MBELE.


Screenshot_20220409-165129~3.png
 
Makongoro akiwa anapiga speech live on a national television inahitaji ujasiri maana street language za kutosha.

Jamaa kitaa sana na anaweza kutoa boko any moment.

Kuna maneno kayasema ni deep street am sure hata rais hakuyaelewa...

The man is funny and free soul creature with a bottle of hennessee in his hand.
 
Hawa watoto wa Nyerere sio chawa, hawajipendekezi kwa viongozi ili wapewe chakula, baba yao alishawakomaza waishi kibishi toka miaka hiyo. Kwa sasa watawala wanawapa madaraka ili kuficha aibu ya watoto wao au wa marafiki zao wanaowabeba.

Tatizo ni watoto wa hiki kizazi kipya, kilichozoeshwa kuwepo serikalini karibia awamu zote wakiulizwa waoneshe walichowahi kufanya hakuna, na wengi wao wamezoea kubebwa mpaka wanamkasirikia anapokuja asiewabeba, hawaoni aibu.

Wataanza kumchora kwa vikatuni twitter kama vile hii nchi ni ya baba yao, wanajiona wao tu, hawajui kuna watanzania wengine wengi wenye sifa na weledi wa kutosha kushika nafasi walizopo na waka deliver zaidi yao.

Kubebwa kumewapofusha akili zao hawaoni mbele tena, hata wakioneshwa udhaifu wao kiutendaji wanajibu tatizo ni uwaziri wao, ulafi wao umejaa mpaka kwenye akili zao sasa wanadhani kila mkosoaji wao anataka nafasi zao huku "wakiuota" urais.
 
Hii kauli ni kubwa sana. Kuwa watoto wa Viongozi wanapata Nafasi si kwa sababu wamewahi fanya matendo makubwa. Ila ni sababu tu ya Majina ya Watoto wao.

Nadhani alikuwa anamaanisha yeye, riziwani kikwete,januari makamba...

Huyu jamaa ni mlevi-mlevi tu anabugia mshahara kwa kodi za Watanzania kwa sababu ni mtoto wa Nyerere.

Ndio maana KATIBA MPYA ni muhimu ili wananchi wasiendelee kubeba mizigo kama hii.
 
Tusubiri tuone Wabunge wetu wa Bunge la JMT watakavyojadili suala la maboresho na uchafu wa TANESCO na gharama yake ya 4Tiii.
 
Kaongea tu, lakini Makongoro ni mpambanaji sana tena bila hata kutegemea jina la baba yake.

Alikuwa Jeshini. Akaenda vitani Uganda.

Aligombea Ubunge Arusha kupitia NCCR Mageuzi 1995 baba yake akiwa hai na akashinda.

Na siku zote amekuwa yeye kama yeye kifikra na Mambo yake.
 
Makongoro akiwa anapiga speech live on a national yelevision inahitaji ujasiri maana street language za kutosha
Jamaa kitaa sana na anaweza kutoa boko any moment
Kuna maneno kayasema ni deep street am sure hata rais hakuyaelewa...
The man is funny and free soul creature with a bottle of hennessee in his hand.
Kwamba "ukome" mama haijui?
 
Back
Top Bottom