Hali ni Mbaya Sana, Tembo Wanazagaa Vijijini na Kuhatarisha Usalama wa Wananchi wa Mbarali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,038
974

MBUNGE BAHATI NDINGO Afikisha Hoja ya Dharura Bungeni - Hali ni Mbaya Sana, Tembo Wanazagaa Vijijini na Kuhatarisha Usalama wa Wananchi wa Mbarali

Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Mhe. BAHATI KENNETH NDINGO leo tarehe 30 Aprili, 2024 amefikisha Hoja ya Dharura Bungeni mbele ya Spika kutokana na Tembo kuingia kwenye makazi ya watu na kusababisha shughuli za kiuchumi na kijamii kusimama kwa zaidi ya miezi mitatu sasa.

"Tunayo Dharura kubwa ambayo imeendelea kudumu kwa muda mrefu lakini sasa hali imezidi kuwa mbaya ndani ya Wilaya ya Mbarali Kata ya Igava kwenye Vijiji Vinne hali ya kuzagaa kwa Tembo imekuwa ni ngumu na takribani miezi mitatu nimesharipoti kwa Waziri wa Maliasili na Utalii lakini bado hatua stahiki hazijachukuliwa" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Usiku wa tarehe 29 na 30 Aprili 2024 Wananchi wa Kata ya Igava wameshindwa kurudi majumbani mwao wakiongozwa na Diwani kwa Tembo kuzagaa na mbaya zaidi Tembo wamekuwa wakizagaa mpaka kwenye maeneo ya shule, watoto wa Shule ya Igava hawaendi mashuleni" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Vijiji vya Igunda, Ikanutwa, Igava na Iwalanje mazao yote ya Mahindi yameshaliwa na Tembo, Wananchi hawana chakula na sasa wamehamia kula Mpunga ambao umekauka . Hali ya wasiwasi kwa wananchi ni ngumu na hawafanyi kazi yoyote zaidi ya Kujilinda na familia zao kwaajili ya Tembo" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Tunahitaji kuona Serikali inachukua jambo hili kwa Dharura kwa Wananchi wa Igava. Suala la Tembo maeneo mengi ni changamoto kubwa. Kwa udharura wa jambo hili naomba Waheshimiwa wabunge wenzangu waniunge mkono kwenye jambo hili ili tuweze kulijadili kwa udharura wake" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali
 

Attachments

  • BUNGE 30 APRIL 2024 HOJA YA DHARURA.mp4
    39.6 MB
Serikali imekuwa ikiuhujum mkoa wa Mbeya bila sababu za msingi.

Kila mara inaongeza maeneo ya hifadhi ndani ya Mbarali ilihali inafahamika ardhi ya Mbarali inafaa Sana Kwa kilimo.

Leo hii uhaba wa mashamba Mbarali ni mkubwa mno ilihali maeneo yanayofaa Kwa kilimo NI hifadhi.
 
Back
Top Bottom