Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 26,434
- 63,725
HAKUNA UJANA TENA. HAKUNA KUSUBIRI TENA.
Kwa mkono wa, Robert Heriel
Yule Mtibeli
Andiko hili, linamfaa kila mtu, ingawaje nimeyaandika haya ili yasomwe na wanangu, hao watakakuja baada yangu. Haya usiwe mvivu wa kujifunza usijeukshindwa wakati wa majaribu.
Ulipokuwa mtoto ulisema kuwa ukiwa mkubwa utakuwa na kazi nzuri, utaoa mke mzuri au kuolewa na mume mzuri kabisa mwenye wadhifa na heshima ndani ya jamii. Unakumbuka ulifikiri kuwa ukiwa mtu mzima utasaidia sana watu masikini, Yatima na wajane pamoja na wote waliowahitaji, Unakumbuka? Pengine umesahau, vipi kuhusu kusafiri nchi za mbali duniani kuuona uzuri wa Ulimwengu, hayo yote na mengine yalikuwa matamanio yako. Vipi nini kimetokea?
Mwanangu, sina lengo la kutonesha hisia zako na kukufanya uhuzunike, haikuwa dhamira yangu kukukumbusha mambo haya ili uumie na kuyaona maisha kama mchezo mbaya usiotamanika. Isipokuwa nimekuandikia haya kusudi ujirudi na kuzirudia ndoto zako.
Niliwahi kukuambia kuwa MAISHA YANAOGOPESHA ILA WEWE USIOGOPE, leo nakuandikia tena; HAKUNA UJANA TENA, HAKUNA KUSUBIRI.
Ule ujana uliokuwa unasimuliwa ukiwa mtoto mdogo ndio huo mwanangu, usije ukadhani kuna ujana mwingine, Hakuna!
Zile ndoto ulizokuwa ukiziota ukiwa mtoto ukisema ukiwa mkubwa, "ukubwa" ndio huu sasa mwanangu. Hakuna ukubwa mwingine tna, Usije ukajidanganya, ujana ndio huo.
Huu ndio umri wa kujaribu na kufanya kila akili na nguvu zako liwezalo.
Ulipokuwa mdogo walikuambia ACHA! Ulipokuwa mtoto walikuwa USISHIKE! Ulipokuwa mdogo walikuambia USIFANYE! tena wakakuambia USISEME! kwani wewe bado ni mtoto, subiri ukiwa mkubwa.
Sasa ushakuwa mkubwa mwanangu, usisubiri KUAMBIWA, usisubiri KUSHIKIWA, Usisubiri KUFANYIWA wala usisubiri KUSEMEWA.
Yote hayo fanya mwenyewe kwani huo ndio muda wako wala hapana muda mwingine.
Mwanangu utakapofikisha umri wa miaka 20 mpaka 40 pambana kufa na kupona.
Usiogope kujifunza kwa vitendo katika umri huo.
Usisubiri utafutiwe kazi, fanya Tafuta mwenyewe kazi yoyote unayoiweza na iliyombele yako. Wewe sio mtoto mdogo mpaka utafutiwe kazi. Usisubiri kama mtoto kutafutiwa pesa, usikubali kupimiwa pesa, tafuta mwenyewe pesa na kile utakachokipata usikidharau kwa sababu hiyo ndio heshima ya jasho lako. Ni kheri ujira mdogo wa jasho lako kuliko ujira mkubwa usio wa jasho lako.
Mwanangu nafahamu ungependa Mimi Baba yako ningekuandalia mazingira mazuri ili wewe Udeke na kuserereka kwenye utamu wa maisha lakini kwa bahati inaweza isiwe hivyo. Na kama itakuwa hivyo, usife moyo, tayari wewe ni kijana na umeshakuwa mkubwa, usifikiri kulaumu wengine, bali fikiri kupambana na kukabiliana na kila kigingi na kiunzi kilichombele yako.
Hakuna ujana tena, hakuna muda uliobakia mwingine wa KUOA Zaidi ya sasa mwanangu. Usikubali umri wa ujana ukakutupa mkono bila kuoa. Hakikisha piga ua garagaza, Oa ukiwa na miaka 24- 35, kwa maana hakuna raha kama kuoa ukiwa kijana.
Mwanangu Maisha hayatarajiwi isipokuwa maisha yanafanywa, ukiyatarajia maisha utaishi kwa kuugua na kuumia siku zote, wala hautayafurahia kwa maana yatakusaliti kila wakati. Hata kama bado mambo yako hayajawa vizuri OA hivyo hivyo, usiyaogope maisha bali yafanye maisha yakuogope, Yaambie Maisha kuwa ikifika mwaka fulani au nikifika umri fulani iwe isiwe lazima nitaoa mke wangu, niwe na pesa nisiwe na pesa lazima nitaoa, bila kujali matokeo.
Maisha usiyaambie kamwe kuwa; unasubiri itakavyokuwa. Nakuhakikishia utakwama.
Hakuna pesa huko mbele mwanangu, usisubirie ya mbele wakati wewe uko nyuma, kama ifuate pesa ya kesho ukiwa siku ya leo, lakini kamwe usisubiri pesa ya kesho ukiwa siku ya leo.
Ukiwa kijana ndio utaoa usisubiri uwe mtu mzima mpaka ushindwe kumfurahia mke wako kwa uzee wako ambao hauna maana yoyote kwake.
Ukiwa kijana ndio umri wa kuzaa watoto usisubiri ukazeeka ushindwe kuwafurahia watoto wako, na pia watoto wako washindwe kukufurahia kisa uzee wako usio na sababu za msingi. Maisha yanaogopesha ila wewe usiogope, hayo nilikuambia tangu siku zile za kwanza uliponijua mimi Baba yako. Mwanangu, ujana ndio huu, ishi kistaa, kula maisha kwa akili ukijua kabisa uzee unakuja kwa kasi. Hata hivyo uzee usikuogopeshe ukashindwa kula ujana wako vizuri, ingawaje Ujana nao usikuendeshe ukashindwa kupata utulivu uzeeni.
Kwa maana Ujana ni kwaajili ya kuvinjari na kuyafurahia maisha wakati uzee ni wakati wa kutulia ukiyatathmini yale yote uliyoyfanya tangu ukiwa mtoto mdogo. Uzee sio wakati wa kufanya, au kushika, au kusema, au starehe bali UZEE ni umri wa kukikabili kifo kwa ushindi mkuu baada ya kufanya vyema ujanani. Tena ujana ndio wakati wa kutenda MEMA kwa wema na Ubaya kwa sababu bado una nguvu.
Tena ndio wakati wa kutenda maovu kwa wakutendeao maovu wala usiogope kumlipa ubaya akutendeaye ubaya, kwa maana ikiwa utafanya hivyo basi hautatulia uzeeni. Walakini utende kwa hekima mambo haya, tena uwe na kiasi katika kutenda maovu usije ukafa kabla ya muda wako, ukaacha raha za Dunia.
Mwanangu, ikiwa wanawake hawatakupenda kwa sababu zao, pengine UFUKARA wako Au maumbile yako au pengine ni hadhi yako kuwa ya chini, hiyo isiwe sababu ya wewe kuwachukia hao wanawake, wala isiwe sababu ya kujichukia wewe mwenyewe, au kumchukia aliyekuumba.
Isipokuwa utafanya kazi kwa bidii yote, nawe ukusanye utajiri kidogo kidogo mpaka utakapokuwa nao, hata hivyo usijepoteza muda kukusanya utajiri mpaka muda wa KUOA ukapita, kwa maana utajiri hautakufaa kitu, nao huo huo ndio utakaokuua na huyo uliyemuoa ukiwa mzee ukamuingiza katika dhambi ya mauti.
Hakuna Ujana tena, wala hakuna muda wa kusafiri isipokuwa sasa. Tembea huku na huko, usiogope ya huko, wala usiwaze itakuwaje. Ukiwa kijana hupaswi kuwaza ya mbele bali ya mbele yakuwaze wewe. Usiogope kwenda mikoa ya mbali, nchi za mbali kwa kuhofia kufa au kuumbuka, kijana haumbiki. Umri wa kuumbuka ni uzeeni huko. Hakuna mwanafunzi anayeumbuka isipokuwa mwalimu.
Kila kijana aogopaye huishia kuwa masikini, kila kijana asiyehangaika huishia kudhalilika, kila kijana asiyesafiri huku na huku huishia kuwa mshamba na asiye na maarifa mengi. Basi ukiwa kijana, safiri huku na huko na usiogope lolote, isipokuwa usisahau kutumia akili kila hatua upigayo.
Usikubali akili yako ikuambie hauna chakufanya, wewe sio mzee wala sio marehemu. Wewe ni kijana damu changa. Fanya lolote hata kama sio chochote. Fanya! Fanya! Kamwe usikome kufanya. Ishike sana Akili kuliko hekima uwapo kijana, ili ukiwa mzee ushike Hekima kuliko Akili. Ujana ukitumia hekima sana kuliko akili utaishia kudhulumiwa, kuonewa, kutapeliwa na mwisho kabisa kuwa hohehahe. Ukiwa kijana tumia akili nyingi kisha nguvu nazo usiziache nyuma. Ili uwapo mzee utumie hekima na busara kwa maana hutakuwa na nguvu yoyote.
Ukiwa kijana usikubali kuachwa na rika lako, usizubae zubae kama kijana mpumbavu. Wakati wa kuwa na kazi tafuta kazi, usibadili badili kazi, ukishaamua kazi yako ni hii, labda ni Fundi cherehani basi jiimarishe mpaka utakapokuwa nguli wa kazi hiyo, lazima upate utajiri kwa maana kadiri unavyokuwa nguli ndivyo jina lako linavyokua, na kadiri jina linavyokua ndivyo utajiri wako unavyokua, hivyo ndivyo utakavyofanya. Usiruke ruke kama Ngedere. Usiwe na tamaa ya mambo makubwa, bali fanya yale madogo uliyonayo kuwa makubwa, hayo ndio huitwa MAFANIKIO.
Wakati wakuoa oa na kuzaa, usikubali kupitwa. Wala usiisubirie kesho ya MANYANI.
HAKUNA UJANA TENA, HAKUNA KUSUBIRI!
Mimi yule Baba yako.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Morogoro