Hakuna na hakutatokea ngoma Kali ya Hip Hop ya kushirikiana hapa Tanzania na Afrika Mashariki kuizidi MTAZAMO

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
2,311
6,825
Hii ngoma iliyokutanisha manguli wa muziki wa Rap hapa Tanzania Kwa miaka hiyo kiukweli ilipikwa,ikasukwa na ikasukika ki kwelikweli!

Kiukweli ninayo Jeuri kusema ya kwamba "Kama Kuna mtu anadhani Kuna ngoma Kali kuizidi hii naomba aiweke hapa na nitampatia Tsh 100,000/=

Hii ngoma iliachiwa rasmi ule mwaka wa 2004,hapa Kuna mtoto wa elfu mbili bila shaka alikuwa na miaka 4!

Ngoma hii ilitengenezwa pale Bongo Records chini ya Mdachi a.k.a Majani,Huwezi amini hii ngoma Hawa wasanii wote kila mmoja alienda studio Kwa muda wake na hawakurekodi wakiwa pamoja!.

Baada ya wasanii wote kuambiwa kuhusu hii project,kila mmoja alipania Ili kumfunika mwenzie na hatimaye mkamio wao ukazaa ngoma Kali ambayo Haito na haiwezi kufa Leo,zimekuwepo ngoma nyingi za Hip Hop za kushirikiana lakini hii inabaki kama THE BEST HIP HOP FEATURE SONG OF THE DECADES
 

Attachments

  • mtazamo_feat._solo_thang_+_prof._jay_aac_42235.m4a
    4.1 MB · Views: 12
Bwana Uone, nina mashaka hapo unaposema "na hakutatokea"

Ni kweli hiyo ngoma ni kali, lakini yajayo huwezi kuyatabiri mkuu, otherwise labda kama unaongelea nafsi yako, maana kila mtu na jinsi anavyouona uzuri!!

(๑•﹏•)
Kwa hizi nyimbo sijui tema mate iteleze mara chapatichapati kufikia ukali wa hio collabo bado na kama mambo yakiendelea hivi kile kizazi kitabaki kua golden generation ya mziki wa kizazi kipya bongo
 
Bwana Uone, nina mashaka hapo unaposema "na hakutatokea"

Ni kweli hiyo ngoma ni kali, lakini yajayo huwezi kuyatabiri mkuu, otherwise labda kama unaongelea nafsi yako, maana kila mtu na jinsi anavyouona uzuri!!

(๑•﹏•)
Mkuu Mtoto wa Jadu labda nikuulize una umri gani?,Je tangu uzaliwe wewe ngoma yako Bora ya Kushirikiana ya Hip hop ni ipi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom