Gwajima atumwa Ninawi, akimbilia Tarshishi, Kawe imtose Baharini

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
26,444
63,760
GWAJIMA ATUMWA NINAWI AKIMBILIA TARSHISHI, KAWE IMTOSE BAHARINI.

Na, Robert Heriel

Gwajima anafanana kwa kiasi kikubwa na Nabii Yona katika kipengele cha Kukimbia uso wa Mungu. Kwa Wasio Mjua Nabii Yona,
Yona ni moja ya Manabii wadogo katika kitabu cha Biblia, kwa waislam Yona anatambulika kama Nabii Yunus.

Umaarufu wa Nabii Yona unajitokeza pale alipomkimbia Mungu. Nabii Yona ndiye nabii wa Kwanza kukimbia uso wa Mungu. Pia Yona ndiye mwanadamu pekee tangu dunia kuumbwa aliyemezwa na samaki. Sijasoma historia yoyote inayoeleza kuwa kuna mwanadamu mbali na Yona aliyemezwa na Samaki. Kama yupo basi nitaomba wataalamu wanijulishe.

Mtu anayekimbia uso wa Mungu lazima amezwe na samaki. Mtu anayekimbia kazi ya Mungu lazima atoswe baharini.
Yona alitoswa baharini, kisha samaki akammeza.

Gwajima ni kama Yona tuu.

Gwajima amejipambanua kama Mtumishi wa mungu, amekuwa mara kadhaa akihutubia akisema yeye anamtumainia Mungu aliyehai, anamhubiri, na kazi yake ni kutangaza habari za Bwana.

Gwajima kama ni mtumishi wa Mungu ametumwa ninawi kuhubiri watu makosa yao. Kukemea uovu, kutangaza habari za ufalme wa Mungu. Lakini Gwajima amempiga chenga Mungu ati hataki kwenda Ninawi anataka kwenda Tarshishi.

Ninawi kwa zama za leo ni kanisani, mikutano ya dini, matamasha ya dini.
Tarshishi ni maeneo yasiyohusika na dini kabisa. Yaani huko ni kwenda kula bata, kufanya shughuli za kidunia.

Gwajima kapanda Merikebu Iendayo bungeni ambapo ni kama Tarshishi badala ya Kupanda merikebu iendayo Kanisani kuhubiri injili.

Mabaharia wa CCM wamempa tiketi ya kwenda tarshishi, wamempakiza mtu aliyekimbia uso wa Mungu, bora hata kipindi cha Yona wale Mabaharia hawakujua kuwa Yona anamkimbia Mungu huenda wangekataa, lakini mabaharia wa CCM wao wanajua fika waliyempakiza kwenye Merikebu ni mtoro aliyemtoroka Mungu.

Matokeo ya kumtoroka Mungu yanafahamika, wapende wasipende lazima merikebu itikisike, dhoruba ikipige chombo, na wakileta mzaha wote wanaweza kupoteza maisha. Sasa ni lazima Gwajima ashushwe kabla chombo hakijafika mbali. Na kama kimefika mbali basi sharti atoswe baharini.

Wananchi wa Kawe hawapotayari kuona wanapatwa na misukosuko kisa mtoro aliyekimbia uso wa Mungu. Wana KAWE Hawapo tayari kutupa mizigo yao baharini na kuhatarisha usalama wao kisa Gwajima aliyemkimbia Mungu.

Ikumbukwe kuwa Gwajima alishawahi kusema kuwa hawezi kugombea Urais, hawezi kugombea ubunge, sijui uwaziri kwani kazi yake ya utumishi wa Mungu ni zaidi ya mambo hayo.

Leo anagombea ubunge, hahaaha! Gwajimaaa! Umekimbia uso wa Mungu, ubunge ni zaidi ya uchungaji siyoo! Hahahha! Gwajimaa! Tarshishi ni zaidi ya Ninawi siyoo?

Bungeni ni zaidi ya Kanisania si ndio, ewe uliyekimbia uso wa Mungu?

Sasa subiri shughuli ya tufani utakayotumiwa na Mungu, huko Tarshishi hautafika, lazima utoswe baharini na Wana Kawe.

Uzuri ni kuwa ukitoswa baharini na wana KAWE Bado Mungu atakusubiria Ninawi naam ndio hekaluni ukaendelea na kazi aliyokuagiza. Nenda ukahubiri kanisani,

Unakimbia Kanisa unataka Mungu ndio akahubiri? Hahahha! Mwenzako Yona ati alivyopanda Merikebu akawa anawaza Moyoni akisema; Kwani Mungu hajaona watu wengine wa kwenda Ninawi mpaka anitume mimi. Hahahah! Yona Bhana,

Yona kakimbia kwenda Tarshishi ati Mungu akahubiri mwenyewe Ninawi. Thubutuu! Mungu akasema subiri utakiona kilichomnyima Mambo Ulimi.

Wana Kawe lazima wakutose Baharini, ili ujue kanisa ni zaidi ya Bunge. Nyumba za ibada ni zaidi ya Ikulu.


Gwajima ni YONA katika zama zetu. Ama kweli dunia matukio yanajirudia.

Gwajima ni YONA, Atoswe baharini.

Taikon Nimemaliza, baharia kwenye Merikebu ya Tarshishi

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Kwa hiyo unataka kusema waendao bungeni ni wala bata??!!

Sidhani kama Gwajima anashindwa kula bata akiwa kanisani tena bata isiyo under pressure.
 
Utumishi upo wa aina tofauti tofauti sawa na vyombo kabatini, hata kwenye Biblia walikuwepo walio mtumikia Mungu kwa upande wa Madhabahu na upande wa siasa, Daniel tena ktk nchi ya ugeni na alifanya vizuri.

Au labda Gwajima katangaza akiwa Mbunge hatakuwa mchungaji tena ila mla bata kama ulivyosema?!


Umetolea Mfano wa Yona ila Mimi nakupa mfano hai... Marehemu Mama Rwakatale aliacha huduma akaenda bungeni kula bata?! Je huduma ilisimama?!

Binafsi sioni tatizo kwa Gwajima ikiwa tu anajua anachokifanya kwani hayupo mtu duniani mwenye akili timamu aliyewekeza kwa hasara, hivyo tumpe muda wa kuona amejipanga vipi kutumikia nchi yake na ni mapema sana kuanza kumhukumu.
 
Yeye ni yona 😂😂 kwani kasema wapi kwamba anakimbia kanisa, embu tuliza mshono kidogo. Yajayo yanafurahishaaaa 🤧🤧
 
Wacha izzo.. Bunge, kozi ya MBA ni vitu vinavyohitaji people from all walks of life kwa kuwa bunge ni sehemu ya kujadili mambo yote yanayomhusu binadamu.
 
Wengine tuna Damu za Kunguni hata pale tu tukiwa tunashauri Jambo jema lenye Maslahi mapana ya Siasa na Demokrasia. Ngoja tujinyamazie tu.
 
Hakika watu wanaweweseka na Gwajima mpaka mnaanza kukoti vibaya neno la Mungu. Mpaka sasa msha0oteza Jimbo
 
Back
Top Bottom