Guys be like "Nina kazi nzuri, Gari, Nyumba, Pesa lakini sipati Mke"

Hapo hakuna mke
Tatizo ni kuwa wanawake wengi ni fake, na wana roho mbayaa. Mwanaume ukiwa na pesa, nyumba plus gari, wanawake weengi utakaotongoza wanaigiza kwamba wanakupenda kumbe wamekubali kwasababu ya hela..

For smart rich guys, golddiggers wanatambulika mapema tu. Utakuta mwanzoni mwa mahusiano, mdada anachoongea Kwako ni shida zake za kipesa tu, hajali kukufahamu zaidi wala nini, atakwambia mara hana hiki, mara hana kile, mara kakuomba mtaji, mara anakwambia mfungue biashara hii, na obviously mwanaume ndo mtoa hela, Ukimwambia let's go kwenye mgahawa huu, anasema she is busy, unajiuliza Je hii ni relationship au relationshit, yani its very sad.

Kwa mwendo huo kuna mke hapo kweli? Labda mwanaume uwe umekubali kupendewa hela Evelyn Salt Heaven Sent
 
Hakuna???? Kwani unaishi wapi ndugu yangu? Wanawake wa hivyo wapo wengi tu. Wengine wameanza maisha na wake zao wakiwa apeche alolo hafi wakaja wakafanikiwa; wengine wameoa wakiwa ready made, lakini walikuja wakatetereka kiuchumi na wake zao stood by their side, wangaoi wanaishi kwa kusaidiana kiuchumi na wake zao? Yes labda wanawake tumekengeuka sana; but they are still plenty of good women out there
Nimesoma comments Zote Lakini niseme tu..Hakuna Mwanamke wa caribre yako, hata wewe Bado siamini Kama uliyoandika unayaishi au utayaishi au umeyaishi
 
About the compliments.... Glory be to God.
My personal views sasa ooooh

Ni hivi; wanawake tuna uwezo wa kuiona future ya mwanaume miaka 10 ijayo; we can foresee that. Tuna uwezo wa kunusa mafanikio ndani ya mwanaume hata kama leo anaonekana ni kapuku. Na kama nilivyokwambia nguvu ya mwanaume includes both nguvu za kimaumbile na nguvu za kiuchumi. Mwanaume akiwa hana pesa, kumfuata tu mwanamke na kumtongoza ni mtihani; achana na mwanamke ambaye kwake anaonekana amemzidi kitu fulani; his inferiority will shut him down.

Mwanamke ambaye yupo educated sio rahisi sana kufall kwa broke, uneducated man; sio kwa sababu tu ya kutokuwa na hela kwa sababu mwingine anaweza akawa na hela lakini mkashindwana kwa kigezo cha yeye kutokuwa na elimu; hakuna kitu kinachohitaji hekima kubwa kama kuishi na mwanamke aliyekuzidi uelewa. Tunaamini kwamba shule inampa mtu exposure na inamuongezea uelewa na maarifa juu ya mambo mbalimbali. Level yako ya uelewa ni vyema imzidi mke ili uweze kumtawala na yeye a-submit kwako. Otherwise wanaume wengi wanakuwa inferior, as a result wanajikuta wanatumia mabavu kutaka heshima; ukimrekebisha tu kitu kidogo ashasema una mdharau kisa elimu yako. Tunahofia tusije tukaishia kuwa "doormats" ili tu tusijeambiwa tuna viburi kwa sababu tumesoma. Bora mwanaume akose hela ila asikose akili (IMO); maana hata neno linasema "Muishi na sisi kwa akili", sio kwa pesa (bado pesa ni ya muhimu though). Akili za kuzaliwa, za darasani, na za mtaani pia

Kuwa less educated kunaweza kusiwe a big deal as long as muhusika anajitahidi kujiongeza na kujitanua kimawazo (sio kila ambaye hakusoma aliamua tu, shit happens). Kuna aina nyingi za informal education ambazo haziwe certified maybe; lakini zinampa mtu exposure na uelewa fulani. Diamond ameishia form 4; lakini anajua kusoma na kuandika, ana-handle discussions vizuri tu na kiingereza juu, ana-reason logically; yaani uelewa wake ni mpana sana kwa sababu aliamua kujiongeza kutafuta maarifa. Mtu kutokusoma sio issue, ila je ndiyo ameridhika na hali yake au anajiongeza? Tunaweza tuka-communicate vizuri na kufanya decisions za za maisha yetu? Hawi intimidated na elimu yangu na haweki vizuizi pale ninapohitaji kujiendeleza academically?

Trust me kuna watu wamefika vyuo; lakini their way of understanding, how they reason; ni bora tu niongee na vitoto vyangu tunaelewana vizuri. Sometimes tunataka tu wasomi kwa sababu ya status, like najua mume wangu akinikuta na mashosti zangu, at least anaweza akachomekea Yes, No pale mambo yakaflow; though still kuna watu wamefika vyuo, na akitaka yu kutamka neno la kiingereza, lazima kigugumizi na kutetemeka kutokee ghafla,

Bado wapo wanawake wengi sana ambao wapo tayari kuanza na wanaume zao from scratch as long as wanaona hao wanaume wana akili za maisha; ila sasa wanaume wengi ndiyo wanageuka kuja kuwa wazinguaji wakishafanikiwa; wanawatelekeza wanawake walioanza nao. Wengi mnoo
Mtu anaweza akawa hajafanikiwa leo under certain circumstances, lakini unaona kabisa he is not lazy, he aspires for greatness; unaona kabisa huyu mtu anapambana. Ndiyo unakuta hata mwanamke anaamua kumshika mkono mwanaume wake, anamsaidia kutimiza ndoto zake ili watimize ndoto zao pamoja.

Hata humu, wanaume wengi wameoa/kuanzisha familia bado wakiwa wanabangaiza sio wakiwa stable financially tayari (wana ajira/biashara, uwezo wa kupanga nyumba, kuhudumia familia...kipato cha kawaida tu). Na wapo ambao hata hicho kipato hakieleweki kihivyo, ni ile uamke utoke ndiyo upate chakula cha siku na bado maisha yanaendelea; watoto wanakula, wanasoma, wanatibiwa, kibanda kinajengwa n.k. So ipo hivyo.

Kuhusu kuoa slay queens; tuwe tu honest, sio kila mwanamke anafake utakatifu ili aolewe. Kuna wanawake ambao wanaishi maisha ya juu kuliko uwezo wao, na hawajifichi na still wanaolewa. So wengine wanaamua tu kuoa "trophy wives"; ila huko mbeleni kikiumana ndiyo akili zinawakaa vizuri
Sammarise kidogo mkuu! Umeupiga mwingi
Muda wa kutyp...unautoa wap ..asee
 
-5458895986198951515_121.jpg
 
Back
Top Bottom