Guys be like "Nina kazi nzuri, Gari, Nyumba, Pesa lakini sipati Mke"

Heaven Sent, katika jiji la Daslam bado kuna wimbi kubwa tu la watu wanashobokea magari tena IST mfano Evelyn Salt humwambii kitu kuhusu magari wakati wa masika akiwa amevaa kitu chake cha high heels toka uturuki.
 
Jitafute wewe binafsi, jijenge vizuri then jikabidhi kwa Mungu akuongoze kwenye huo mchakato. Usichague kwa macho ya kibinadamu na akili tu za kawaida. Muombe Mungu akupe macho ya rohoni, utaona hadi na attributes zisizoonekana kwa macho ya kawaida. Hela ni za muhimu sana lakini sio kitu pekee kwenye mahusiano. I pray wote mnaotafuta wake mpate wake wema eeh, mtuletee testimonies nzuri nzuri jamani
Nisaidie mkuu, nawezaje kuangalia kwa macho ya rohoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake wengi yani most of them wanataka stability ila wanataka stability kutoka kwa wanaume...yan wengi wao wanajiconsider wako stable sababu wako attached kwa mtu ambaye yupo stable, yan kiuhalisia wao kama wao wanakuwa hawana cha kuoffer kwenye ralationship yao zaid ya the "cookie" and they cannot be stable by themselves (hii kitu wanawake inabid muiangalie sana). Ukimpata mwenye stability anataka equal rights kwenye kundesha hiyo relationship na hapa ndio matatizo yanapoanziaga. Anyways....

Alafu kitu kingine unaposema unataka mtu anaejitambua, what is kujitambua in broad terms ? Yan unajuaje huyu anajitambua ? ili mwanaume ajitambue inabid awaje ? what are the indicators ? je hizo indicator zina correlation yeyote na gari, nyumba, na pesa ?...

Kuna sababu ya msingi kabisa ya mwanaume kuanza kutafuta mwanamke akiwa anaweza kuishi vizuri na akiwa ameshaacomplish goals zake. Kwa mwanaume mwanamke ni kitu cha mwisho kukitafuta baada ya kuacomplish goals zako lakin hili ni tofauti kwa wanawake, na ndio maana mwaname anaweza akamwoa mwanamke yeyote(aliesoma, asiyesoma, mwenye pesa au asie na pesa), ilhali mwanaume ana hivyo vyote, ila mwanamke mwenye aliesoma na pesa na vitu vingne huwa anaona kuwa na mtu asiesoma na hana kitu ni kujikosea heshima na hata akiwa nae atamnyanyasa sana...Hii ndio sababu kuu inafanya wanaume washangae anakosaje mke na kashapata ulimbo wao ?..
Hii comment yako mkuu nai printi na kuwekea lamination na kuning'iniza chumbani
 
Kwa mwanamke, mwanaume wa maana ni yule mwenye

1. Fedha

2. Kazi nzuri

3. Gari

4. Nyumba

5. Degree

6. Pamba Kali

7. Muonekano mzuri

Ukikosa hivyo hutopata mke asilani abadani!!!.

Kama uko well established financially ni sawa na kusukuma mlevi tu.

Kama uko apeche alolo, mongwe au lumba aisee utaishia kununua wa buku

Kama uko kwenye process ya kuji establish nobody will give a fvck about u.

They only care about the results not the efforts u try to make !!

Simaanshi wanawake waolewe na wavivu

Ila mentality zibadilike from family level
 
Ukitaka mke wewe fanya mambo yako mtakutana mbele ya safari, mke sio mtu wakumtafuta ni mtu wakukutana naye kama marafiki tu.

Mnawezakakutana kwenye gambe, biashara, kazini, au ibadani ni wewe tu ukutane naye. Sio kumtafuta

Anatafutwa mtu aliyepotea tu, labda kama mmepotezana na mkeo hapo ruksa kumtafuta
 
Point yangu ilikuwa hivi; ndoa haihitaji tu utayari wa kifedha. Inahitaji utayari wa mwili, roho na akili. Zaidi ya yote, ukiondoa pesa na mali; ni vitu gani vingine unaweza kuoffer kwenye mahusiano yako ili yawe bora na kudumu ?
Kwenye wanawake 100,wenye mtizamo kama huo hawazidi watano.
 
90% ya wanawake wa Tz ni gold diggers tu... Na kamwe huwezi fananisha nyumba na mwanamke.. Kila mtu anaweza kumiliki mwanamke hata 10 akitaka ila sio kila mtu anaweza kumiliki nyumba..

All in All 98% ya wanawake wa JF ni gold diggers wanaopenda vitu vizuri vizuri.. Nishapiga zaidi ya 10 humu JF hawana lolote, maisha yao ni tofauti na haya wanayoandika humu..
Aisee
Unaposema 90% ya wanawake tz humo wapo family yako including your mum and sisters,
Anyway kazi iendelee
 
Upretend kwamba huna chochote kabisa au upretend kama umejaaliwa kidogo? Ukijifanya maskini sana, hata potential candidates wengine watakukimbia

Hakuna universal formula ya kumpata wife material zaidi ya kumuomba tu Mungu. Angalia aina ya mwanamke unayemuhitaji; sio unakimbilia wale slay queens ili tu uonekane na wewe una pisi kali, ilhali unajua zinahitaji high maintenance. Hata ukimpata mwanamke; be generous to her, but don't make her financially dependant on you. Wakati mwingine kabla ya kumpa hela, atoe maelezo ya kueleweka anahitaji hela ya nini; akupe mchanganuo kabisa. Sio mtu anakuja anakukamua tu kisa anataka maisha ya starehe. Hakikisha mwanamke uliyenaye atakusaidia kuongeza hizo mali ulizonazo kwa mawazo ayke na utulivu wake; na sio atazitapanya tu. Angalia mwanamke atakayeongeza thamani kwenye maisha yako.

Uwe na good attitude unapomfuata mwanamke, usijaribu kumuimpress mwanamke kwa pesa zako; siku ya kwanza tu ashajua kila unachomiliki (ingawa pia na sisi huwa tunamnusa mwanaume mwenye mafanikio mapema sana); na ushamjaza mapene. Mtaenda kwa mtindo huohuo wa kujazana mapene, huko mbeleni ndiyo utaelewa somo

Aisee, unatoa madini sana we mdada, how old are you?....uandishi mzuri, mpangilio mzuri kweli wewe Heaven sent, njmejikuta napata u serious on reading your posts an comments.....nikipata mkufunzi kama wew nitafurahi.
 
Wanawake wengi yani most of them wanataka stability ila wanataka stability kutoka kwa wanaume...yan wengi wao wanajiconsider wako stable sababu wako attached kwa mtu ambaye yupo stable, yan kiuhalisia wao kama wao wanakuwa hawana cha kuoffer kwenye ralationship yao zaid ya the "cookie" and they cannot be stable by themselves (hii kitu wanawake inabid muiangalie sana). Ukimpata mwenye stability anataka equal rights kwenye kundesha hiyo relationship na hapa ndio matatizo yanapoanziaga. Anyways....

Alafu kitu kingine unaposema unataka mtu anaejitambua, what is kujitambua in broad terms ? Yan unajuaje huyu anajitambua ? ili mwanaume ajitambue inabid awaje ? what are the indicators ? je hizo indicator zina correlation yeyote na gari, nyumba, na pesa ?...

Kuna sababu ya msingi kabisa ya mwanaume kuanza kutafuta mwanamke akiwa anaweza kuishi vizuri na akiwa ameshaacomplish goals zake. Kwa mwanaume mwanamke ni kitu cha mwisho kukitafuta baada ya kuacomplish goals zako lakin hili ni tofauti kwa wanawake, na ndio maana mwaname anaweza akamwoa mwanamke yeyote(aliesoma, asiyesoma, mwenye pesa au asie na pesa), ilhali mwanaume ana hivyo vyote, ila mwanamke mwenye aliesoma na pesa na vitu vingne huwa anaona kuwa na mtu asiesoma na hana kitu ni kujikosea heshima na hata akiwa nae atamnyanyasa sana...Hii ndio sababu kuu inafanya wanaume washangae anakosaje mke na kashapata ulimbo wao ?..
Nilikaa kimya ili nije nikujibu kwa kutulia.

Najua umuhimu wa mwanaume kuwa na nguvu za kiume (nguvu za kimaumbile na za kiuchumi). Hakuna kitu kinampa mwanaume utulivu kama akiwa na nguvu zake za kiume. Chochote kibaya kikitokea kwenye nguvu zake, ni majanga. Tustick kwenye nguvu za kiuchumi/kiuzalishaji.

Na umri wangu huu; ninajua nyumba inakuwaje baba akiwa stable kiuchumi, na ninajua nyumba inakuwaje baba akiwa na changamoto za kiuchumi. Lakini haimaanishi tu kwamba kujenga familia nzurina bora kunahitaji tu kuwa vizuri kiuchumi; it is more than that. No wonder hata mabilionea pamoja na kuwa na mahela yote, bado wanatalikiana kama tu sisi maskini.

Yes mwanaume akiwa vizuri kiuchumi, anakuwa na uhakika wa kuhudumia familia yake; kwa malazi, mavazi, na chakula. Lakini haimaanishi kwamba jukumu lako linaishia kwenye ku-provide tu. Unatakiwa uwepo kwenye familia yako kihisia, kiroho, kiakili na kimwili pia. Kuwa na pesa haimaanishi kuwa ndiyo unafit kuwa mume na baba bora. Point yangu ilisimamia hapo; tunapojijenga kiuchumi, tusisahau kujijenga kitabia, kihisia, kiroho , kiakili. Familia haijengwi kwa pesa tu. Je umeshawahi kujiuliza kwamba kwa hapo nilipo, je nipo emotionally/mentally stable kuanzisha familia, au kwa tabia zangu hizi nitaweza kweli kulea watoto wema na kumpa mke wangu amani ndani ya nyumba? Utamsikiliza mkeo au wewe ndiyo mwanaume, hakuna wa kuuliza wala kupinga usemacho? Uhusiano wako na Mungu upoje, utailea familia yako kwenye misingi ipi? Kuna mambo mengi sana ya kuji-evaluate kabla hujawaza kujenga familia. Na ndiyo maana wapo watu wengi wenye vipato visiyo stable/kueleweka; lakini bado wameoa, wanatunza familia zao na wana amani kwenye nyumba zao.

Kujitambua ni nini? Kujitambua ni kujielewa binafsi kwamba wewe ni nani, unahitaji nini, una malengo gani; umetoka wapi, uko wapi sasa hivi, na unaelekea wapi. Sio kila mwanaume mwenye pesa anajitambua na anafaa kuwa mume na baba wa familia. Ni sawa na wanaume ambao wanaamini kwamba ukishakuwa na pesa hakuna mwanamke wa kukukataa; kiukweli hawajitambui kiakili. Na wengi wao ndiyo wale unakuta hata akiwa na mwanamke; hamuheshimu, hamjali, anamtreat anavyojiskia; kwa sababu tu maybe anamuhudumia anaamini kuwa amemaliza majukumu yake so mwanamke atakaa tu hapo, na hata asipokaa wapo wanawake wengi huko nje wanamtaka kwa sababu ya pesa. Kumpa mtu pesa, haimaanishi kuwa ndiyo unampenda sana au kumjali sana; what matters ni moyo wako behind his giving. Watu kibao wanahonga tu michepuko na wala hawana mpango nao zaidi ya kuwatumia kimwili.

Kuwa na pesa haimaanishi kuwa mtu anajitambua; not necessarily kwa sababu sio kila aliyepata fedha alizipata kwa kutumia akili na kujituma. Wengine wamepata pesa kujituma (legally), kiwizi, kwa kurithi au kibahati tu. Sasa meshapata hizo fedha; priorities zake ni nini, ana malengo nazo gani chanya, anaweza kuziongeza/kuzizalisha zaidi? Ni watu wangapi ambao leo unamuona ana pesa, baada ya mwezi kazitapanya zote? Na mwanaume anayejitambua, hata kama ana mali; ana utu, ana heshima, hana ulimbukeni. Hata akimfuata mwanamke, atamfuata kwa adabu. Imagine unaingia mahali unamkuta mdada wa watu amekaa, afu unapita zako, unatafuta sehemu ya kukaa afu unamtumia watu eti akufuate wewe ulipokaa; mimi binafsi hata kugeuza shingo kuangalia nani ananiita sigeuki. Jishushe mfuate alipokaa, msalimie, jichekeshe chekeshe then mambo mengine yataendelea. Be humble hata kama una pesa; approach women with respect

Mwanamke anayejitambua has so much to offer hata kama hatokuwa financially stable kwa wakati huo. Mwanamke kiasili ana reproductive power, mbegu yoyote utakayoipandikiza kwake; ataizalisha. Sasa ukikutana na mwanamke asiyetaka kufanya majukumu yake, anataka kuslay tu, na bado ukamuoa; tatizo ni wewe na si yeye; you can choose better and wisely. Wengi tumelelewa na wamama wa nyumbani; yet wamelea watoto wanaojitambua in all aspects; na hata baba asipokuwepo, bado mama alisimamia familia vizuri. Mwanamke anakulea wewe na watoto, atakupa ushauri, atasimama na wewe katika kila hali, na atakupa utulivu na amani ya moyo ili ufanye mambo yako kwa umakini. Mungu alipomwambia Adam "nitakufanyia msaidizi", hakumaanisha tu partner wa kitandani. We as women, have so so much to offer to help our men.
FB_IMG_1633072414805.jpg
 
Mmh nimekuwa mchangiaji mzuri sana wa threads za wengine ila leo limenigusa so nimeamua tu na mimi nianzishe kathread kangu lol. Excuse my gazeti

For a while nimekuwa nikisikia na kuona wakaka wengi, especially wale ambao wanataka kuoa wakilalamika "nina gari, nina nyumba, kazi nzuri, hela etc. But sipati mke wa kuoa". Jana tu I was talking to a certain brod na yeye akaniambia the same thing. Yani hiyo statement huwa inanipa a series of unanswered questions.

Najua hiyo type na humu ndani wapo kibao. Siwatukani ila najiuliza tu, hivi mnavyowazaga hivyo huwa mnakuwa kwenye akili zenu timamu au? Tangu lini gari likaoa mke, unataka mke au unataka dereva/abiria? Una nyumba..so what exactly are you looking for; a tenant, a house keeper or what? Aliyewaambia kwamba kuwa na gari, kazi na nyumba ndo kigezo tosha cha kuoa ni nani? Hivi hukai hukajiuliza mbona nina hivyo vyote but huu ni mwaka wa 3, 4, 5 natafuta "mke" na Sijapata? Kuna tatizo gani? Ungekuwa umekaa kwa kina ukajiuliza hivyo basi naamini akili yako ingekuwa imefunguka hata kidogo.

Apart from nyumba, kazi, gari.. what else can you offer?. Kama hivyo ndo vingekuwa the only vigezo, basi kila mwenye navyo angekuwa ameoa warembo wa kutosha sana tu. Hivyo mnavyoviona ndo vigezo tosha, baadhi yetu tunaviona kama "bonus" tu kwa mwanaume anayejitambua.

Mnatiana tu ujinga humu, Tafuta pesa, utang'oa mademu wa kila aina, nachokagaaa mimi mmh. Of coz utang'oa mademu wasiojitambua, sio wanawake wenye akili zao timamu unless una extra things to offer. Kila mtu anapenda pesa/gari, lakini sio kila mtu anashobokea pesa/gari. Hivi seriously unampata msichana eti kwa sababu una gari, hivi hii century kuna watu still wanashoboka na magari, unless wana matatizo. Gari ambalo unapewa lift mara moja kwa wiki/ mwezi siku zingine zote unashika bomba, ndo limfanye mtu avue tei tei?

Hivi ukiwa na mwenye gari na wewe unakuwa unaown hiyo gari au ownership yake ni sexually transfered? Wewe utakayemla huyo girl na huyo girl wote mna matatizo tena makubwa tu. Tafuta hela zako, jitambue then utapata wanawake wanaojitambua. Wanaume malimbukeni wa hela hatuwataki. Kuna watu hata watokee kwenye Forbes na WB waseme watafinance harusi yenu, hukubali kuolewa naye ng'oooo maana hajitambui.

Mtu hana cha maana anachoongea ila kujibrag tu, nina hiki, nina kile mweee yani hapo mwenyewe anaona kashamaliza mchezo. So disgusting, ndo maturity ya mtu anayetaka kuoa huyo pyeee. Huna cha maana cha kukudefine apart from gari na nyumba mmmh. Usipendwe na mtu, basi ushajistukia "au kisa nina gari" mwee jamaniii. Siku ukimiliki jet si ndo hata humu Ukipewa like utahisi "ashasikia nina jet, ananishobokea" hahahah

Afu nyie average joes ndo mnasumbua kweli. Mtu akifanikiwa tu kidogo anajikuta Bakhresa na yeye, hivyo vigezo sasa "huyu demu sio wa hadhi yangu". Wewe hadhi yako ni ipi haswa?. It reaches a stage mnatuita watoto wa watu "scrapers" hivi una uwezo wa kuumba hata kidole wewe? If you can afford someone expensive please just go for her, sie wenye sura na shape za wajomba zetu tuacheni kwa heshima tu.

Have you ever asked yourselves watu wenye hela za uhakika, mawaziri, the high profile Men wake zao wakoje? Unakuta ni mabinti wa kawaida tu wengi, but wana class. Hata kama ukikuta binti ni famous, beautiful ana status etc, lazima "ANAJITAMBUA" kwanza. Ila nyie ndugu zangu sasa ukiwa na hela tu kinachokuja ni "a very beautiful girl" washkaji wakukomeeee. please kabla beauty haijaja pima anajitambuaje.

Uzuri, hela, status ni "BONUS" jamani. Angalia ni Vitu gani mtu anavyo vya kusustain ndoa yenu. (Sijasema muoe wanawake mvutoless, sio sifa na hata hao mvutoless sometimes wanapretend kuwa decent ili kujiongezea marks. Beauty + brain+ character). Mnajikuta mnajenga mahusiano yanayobase kwenye hela za mawazo, kesho na kesho kutwa umetetereka kidogo mke kakukimbia utamlaumu? She was there for money, hela imeisha afanye nini sasa.

Oooh nina gari, sawa utaoa "dereva/abiria " na sio "mke mwema". Kesho ukiwa huna gari usishangae dereva/abiria wako akikutoroka. Abaki kufanyaje kwa mfano, acha akatafute gari lingine

Embu leo hii, ufahamu wako utanuke kidogo. Jiulize unataka mahusiano Yenye misingi ipi, na hiyo misingi yako itakupelekea kuwa na ndoa ya aina gani. Una kitu gani cha kuoffer mahusiano yako ili yawe sustainable (things that are looking for long term sustainability) apart from vigezo "bonus".

Jitafute wewe binafsi, jijenge vizuri then jikabidhi kwa Mungu akuongoze kwenye huo mchakato. Usichague kwa macho ya kibinadamu na akili tu za kawaida. Muombe Mungu akupe macho ya rohoni, utaona hadi na attributes zisizoonekana kwa macho ya kawaida. Hela ni za muhimu sana lakini sio kitu pekee kwenye mahusiano. I pray wote mnaotafuta wake mpate wake wema eeh, mtuletee testimonies nzuri nzuri jamani

Anyway zilikuwa tu ni akili zangu za wakati huu, I'm still entitled to my opinions. Additions + Polite criticisms are warmly welcome, I don't invite insults abegooooo

HAPPY WOMEN'S DAY
Hii thread ndio ilipaswa kushinda stories of change.
 
Hii comment yako mkuu nai printi na kuwekea lamination na kuning'iniza chumbani
Thanks Man..mitaa imetulea, utake usitake fedha inaplay role kubwa kwenye mapenz na masha binadamu..mfano kuna wanaume wawili tuseme wote wacha mungu na wanaupendo wa dhati, ila mmoja yuko financially stable mwingine amefulia unadhani nan ana posibility ya kumwin mwanamke mmoja wanaomfukuzia provided chances za mwanamke kumpenda yeyote yule zipo sawa ?...

Mkuu unajua moja ya kiumbe mmoja wa ajabu ni mwanaume yupo tofauti sana na mwanamke. No offense, ila mwanaume (most of them) , mwanamke kwake ni moja ya driving force ya yeye kutafuta hela kwa nguvu zote ili aweze kuish kwa namna anayotaka yeye na mwanamke wake..ila kwa wanawake huwa ni tofauti lazima tukubali utofauti
 
Back
Top Bottom