barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Walichonichekesha hao jamaa.Walitumbukiziwa kikaratasi kuulizwa kama ni wazima,wao wakajibu ni wazima ila wakaorodhesha vitu wanavyohitaji wakiwa huko chini wakisubiri kuokolewa.
Yaani katika yote wamesisitiza watumbukiziwe sigara,katika kikaratasi chao wanasema wana kiu sana ya sigara ndio moja ya shida waliyonayo huko.
Ile dhana ya maji ni uhai inaonekana haipo kabisa kwa hawa jamaa.Maana huko chini hewa ni nzito kiasi wametumbukiziwa mtungi wa Oxygen,lakini wao wanasisitiza kiberiti na sigara.
Au hii inaweza kuwa ni ombi la mchina aliyeko huko chini?Inachekesha na kusikitisha