GEITA: Waokoaji wapata kuwasiliana na waliofukiwa na kifusi mgodini, warudisha majibu kuwa wako hai

Inasikitisha sana.

Matatizo siku zote yasikie kwa mwenzako, usiombe yakukute.

Hao jamaa wapo kwenye wakati mgumu sana
 
Wamesahau kuomba bangi. Kukaa chini ya kifusi inahitaji ujasiri na kujitoa fahamu kwanza maana lolote lawezakutokea muda wowote
hawajasahau mkuu wamefanya heshima tu.izo Bange wakitoka wataomba!
 
wamenifurahisha kweli wapatikane tu yaani hawana hofu wanaomba hadi viburudisho sigara na kiberiti
 
Mkuu sio SMS, ni barua via borehole.
Kuna borehole imechimba parallel to the shaft na kufanikiwa kupata point baada ya ile ya kwanza kutoka nje ya target.
Kwa minajili iyo walishushiwa radio japo ili fail but ikaandikwa barua na wakatumiwa via borehole na wao waka responds kuwa wapo wazima na wana njaa sana mmoja wao amechomwa na msumali . wanataka chakula na fegi
Yesu wangu Na Maria jamani Mungu wasaidie., uwiiiiiiiieee yeuwiiiiiiiii auwiiiiiiii
 
61346f1cd7a78435f806e20e6acaecab.jpg
Wakati Imeelezwa kuwa waokoaji katika mgodi wa dhahabu wa Union ulioko Geita, wamebakiza mita tatu kuwafikia waliofukiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani akizungumza na ndugu wa watu waliofukiwa amesema kwamba wanafanya mpango wa kuwapelekea chakula wachimbaji hao

Amesema kwamba jana wamefanikiwa kufanya mawasiliano na wachimbaji hao na kwamba wapo kumi na tano na kuwa wanachohitaji kwa sasa ni chakula

Alisema waokoaji walifanikiwa kuwafikishia kamba na kalamu watu hao ambao waliaandika mahitaji yao na kusema kwamba wote wapo salama

Awali akizungumza na gazeti hili akiwa eneo la tukio jana, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga alisema kuwa bado walikuwa hawajawafikia watu hao lakini wamefika chini sana na kukaribia njia hizo za mlalo

"Kinachofanyika sasa ni kuondoa udongo kwenye njia kwa kutumia watu kwa kufanya taratibu na kuwa umakini mkubwa ili udongo usiporomoke tena katika eneo hilo,"alisema

Alieleza kuwa matumaini yao ya kuwakuta watu hao wakiwa hai bado ni mkubwa kwani uokoaji huo unafanyika kwa umakini lakini kwa haraka sana na sehemu iliyobaki kufikia njia hizo ni ndogo sana

Watu hao akiwemo raia wa China mmoja walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya udongo kukatika na kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka na uokoaji unaendelea kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya uokoaji

Kyunga alieleza kuwa watu wengi wapo katika eneo hilo wakiwemo ndugu wa waliofukiwa lakini kwa juhudi wanazoziona za uokoaji wametulia na kufuata maelekezo wanayopewa ikiwamo kukaa mita 500 toka eneo la tukio

Alisema wametakiwa kukaa na eneo hilo la uokoaji ili wasisongomane na watu wanaoendelea na uokoaji ili kuwapa fursa nzuri ya vikosi kujadiliana namna ya kufanywa kwa ajili ya kufanikisha uokoaji huo.

Chanzo : HabariLeo
 
Mungu aingilie kati na Tuendelee kuwaombea njia za kuwaokoa salama zipatikane haraka
 
Back
Top Bottom