Fred Mpendazoe: Siwaelewi Tundu Lissu na CHADEMA

ila kwa ushauri usipende kumwelewa mtu kwa kupindukia, mpe asilimia kadhaa mama sisi binadamu hususani watanzania si watu wa kuaminika sana..!!!!
Kumwelewa mtu hakuishii kujua ukamilifu wa mtu na kuuamini blindly.
Kumwelewa mtu ni kama kuijua sarafu, lazima utafute kuona pande zote mbili.
 
Simwelewi Tundu Antipas Lissu na Chadema.

Nilipata nafasi ya kumsikiliza Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu mbunge wa jimbo la Singida Mashariki alipokuwa akichangia hivi karibuni kuhusu suala la hatua ambazo zimechukuliwa na seriklai kuhusu makinikia au mabaki ya mchanga kutoka kwenye migodi ya dhahabu.

Kwa upande wangu nilimuona alitumia lugha kali sana na alikuwa na ghadhabu. Nilijiuliza sana kuhusu mchango alioutoa na ghadhabu alizoonyesha. Imebidi nijaribu kufuatilia misismamo yake, huu ni mtazamo wangu tu.

Nilianza kumfahamu Tundu Lissu mwaka 1997 alipokuwa akifanya kazi LEAT na alifaya kazi nyingi na baadhi zililisaidia Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira, NEMC wakati huo mimi nilikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu.Ni mwanasheria mzuri sana. Na sijasikia kashifa yoyote juu yake. Nilimweshimu sana kipindi hicho.

Nikiwa Mbunge kupitia CCM 2005-2010 moja wa wabunge walionivutia katika michango yao hasa kuhusu kupiga vita ufisadi alikuwa ni Lissu, Dk Slaa na Zitto Kabwe. Walikuwa upinzani lakini walikuwa wanajenga hoja vizuri.Walipokuwa wakijenga hoja juu ya ufisadi, hawakuacha kumtaja Lowassa.

Mwaka 2015 wakati Lowassa anahamia Chadema kutoka CCM nilipata taabu kubwa nilipomwona Tundu Lissu akiwa ndiye alikuwa akimtetea Lowassa kuhamia Chadema na akimlaumu Dk Slaa.

Wakati wa kampeni 2015 UKAWA ilikuwa na kazi ngumu kuwashawishi watanzania kuhusu suala la ufisadi. Ajenda ya ufisadi ikafa. Uchaguzi ukafanyika, watanzania wakaamua waendelee kuongozwa na CCM. CCM ikaunda serikali.

Serikali ya CCM chini ya uongozi wa John Pombe Magufuli (JPM) ikaanza kushughulikia suala la ubadhirifu, uzembe, na maadili kwa watumishi wa umma. Watumishi wengi walichukuliwa hatua kali na serikali ya CCM chini ya uongozi wa JPM. Mtakumbuka, kuna kiongozi a;liyekuwa analipwa mishahara 17.

Mtakumbuka uozo kwenye bandari ya Dar es salaam.Na mtakumbuka kwamba walipatikana wafanya kazi hewa zaidi ya elfu 10, wanafunzi hewa na suala la madawa ya kulevya.

Tundu Lissu na Chadema walilalamika juu ya hatua zilizochukuliwa na serikali, wakisema bwatu hao waliochukuliwa hatua wanaonewa au utaratibu uliotumika ni mbovu. Mashaka yangu juu ya Mheshimiwa Tundu Lissu yakazidi kuwa makubwa.

Lakini pia mtakumbuka kuhusu suala la UKUTA. Wabunge wa UKAWA walikuwa wakifunga midomo wakiwa bungeni wakidai demokrasia pana. Lakini kwa sasa ni dhahiri kwa watu wengi kuwa ndani ya CCM kuna demokrasia pana kuliko ndani ya Chadema.

Hili limedhibitishwa na uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki. CCM ilifanya mchakato wa kidemokrasia kuwapata wabunge wa Afrika Mashariki kuliko ilivyokuwa ndani ya Chadema.

Haya yote yaliyofanyika ndani ya Chadema Lissu akiwemo na ni mwanasheria Mkuu wa Chadema. Ninaanza kujiridhisha kwamba Mheshimiwa Tundu Lissu siye niliyemfahamu.

Rais John Pombe Magufuli amedhubutu kuchukua hatua juu ya upotevu wa mapato yaliyotokana na kupelekwa makinikia nje ya nchi na kuagiza uchunguzi ufanyike. Ripoti ya uchunguzi imefichua ufisadi wa kutisha kwenye usafirishaji wa makinikia nje ya nchi. Watanzania wengi wazalendo waliosikiliza ripoti hiyo wameumia sana kwa taarifa zilizomo kwenye ripoti hiyo.

Watanzania tumenyonywa kiasi cha kutosha.
Mliopata nafasi ya kumsikiliza Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu, amesema Rais amefanya jambo la hovyo sana. Na alionekana kukasirika sana.Hiki kimenishitua sana na ninashawishika kuamini kwamba Lissu hayuko sawa, ana ulemavu usioonekana kwa macho. Tundu Lissu ni mwanasheria mzuri sana lakini amekosa roho ya kuipenda nchi yake, amekosa chembe ya roho ya uzalendo.

Ninaamini vyama vya siasa vinatakiwa kuungana katika masuala ambayo yana maslahi mapana kitaifa kama hili suala la makinikia kupelekwa nje ya nchi. Aidha, wataalamu wanatakiwa kujitokeza kutoa ushauri namna ya kuboresha ripoti iliyotolewa na kuisaidia serikali ili iweze kuisaidia serikali kuchukua hatua sitahiki.
Lakini Tundu Lissu alikebehi au kudhihaki hatua ikliyochukuliwa na serikali.

Wapo watanzania wengi nwaliomwamini sana Tundu Lissu na wanataabika na misimamo yake ya hivi karibuni kama ninavyotaabika. Na ni kweli pia kwamba kuelekea uchaguzi mkuu 2015, Chadema ilikuwa tumaini la watanzania wengi. Lakini kwa sasa, ni vigumu kuelewa Chadema kama chama kinapigania nini au ajenda yake ni nini. Chadema imepoteza mwelekeo na inapoteza fursa ya kushika dola.
Sasa wewe kwa akili zako za ng'ombe aliyekatwa mkia unawezaje kumuelewa Tundu Lissu? Wewe unaweza kumuelewa Profesa Maji marefu, Kibajaji, Jah people (Mbunge wa Makambako) na wengine wenye ufahamu wa chini ya wastani walioko pale Lumumba!
 
Kumwelewa mtu hakuishii kujua ukamilifu wa mtu na kuuamini blindly.
Kumwelewa mtu ni kama kuijua sarafu, lazima utafute kuona pande zote mbili.
That's good kama ni hivyo nikajua kumwelewa kwako ni kwa maana ya kwamba huambiwi chochote kuhusu flani...!
 
ohhohooo!!! kiongozi Fred Mpendazoe umerudi tena

Na kwa kifupi hutamwelewa sababu ya fikra haziko huru kiongozi

Kama huna Analytical Skills ni kazi bure kumsikiliza Lissu
Vile unavyo muelewa wewe ni kwa uelewa wako Mpendazoe yuko sahihi na wewe analytical yako hiyo huenda na weee you need more knowledge
 
Sikiliza ndugu yangu zitto.tusiegemee sn kwenye vyama.c kweli kuwa unapokuwa mpinzani maana ake wewe ni msaliti au adui wa nchi.tunao wazalendo wengi tuu kwenye vyama vyetu vya upinzani.na c kweli kuwa waliomo ccm wote ni wazalendo.HAPANA. ccm yako magenge mengi ya waharifu.tunachotakiwa kuangalia ni uzalendo binafc wa mtu.hv unaupata wp uzalendo wa tundu lissu kwenye hili swala.anapata wp ujasili wa kusimama kwenye jukwaa na kutangaza haki za accasia kisheria, bira kugusia haki za taifa lake.kz ya wakili ni kutetea na kuwakilisha.bira kujali umehusika au huku husika.ndicho anachofanya lissu.hv lissu anaposimama kutangaza haki za accasia kisheria anafanya hvyo km mbunge au km rais wa T.L.S ???hivi anapofanya hivyo anaiwakilisha tanzania au accasia!@?? Nyuma ya mgongo wa lissu amejificha nani??!! Accasia au umma wa watanzania wanaoibiwa.!!?? Lissu ni rais wa T.LS. NA MBUNGE.anaouwezo wa kwenda moja kwa moja kumshauri rais.hivi tundu lissu.chenge.werema na karamagi aliefunga mkataba hotelin londan wanatofauti gn??!! Narudia lissu ni msaliti.na kuuona uasliti wa lissu inabidi uwe na jicho la kizalendo na mtizamo wa kizalendo.Ukiwa huna uzalendo.lazima umuunge mkono lissu.Mwisho hii tume ya profesa mruma c ya mwisho.na rais hajafanya uamuzi.ipo tume nyingne ya wanasheria km lissu haijatoa ripoti yake kwa nn asiisubiri.au kw nn asiende kuishauri.?? Hv leo lissu akiombwa asimame upande mmoja autetee kwenye huu mgogoro.ATATETEA UPANDE UPI??. ZITTO HII NI VITA KATI YA TAIFA LETU NA MABEBERU TOKA NJE.NA KZ YA MABEBERU NI KUWAGAWANYA.
Mkuu naheshim mawazo yako ila natofautiana kidogo na wwe kwenye kudefine uzalendo.... naona uzalendo ni KUONGEA UKWELI na wote tunajua kipimo cha juu zaidi cha uzalendo ni kukubali kutofautiana mawazo kma taifa!!! Hivyo lisu HAJAKATAA kuwa ACACIA wanatutapeli ila alichosema yye ni approach tofauti full stop.

Ili kumuelewa lisu inabidi uangalie je IMPACT ya ushauri wale ni nni??? Je tukichukua ushauri wake tutapoteza nini?
1. Kwanza inaonyesha ana nia nzuri na taifa maana kma angekuwa na nia mbaya asingeshauri njia nzuri ya kuwabana wezi hawa. Lisu alichishauri ni kujaribu kuepusha nchi yetu kuingia hasara kma ile ya dowans na ssa IPTL!!! au hata ile ya samaki za magufuli!!! Kma angekuwa na nia mbaya iweje ashauri kitu ambacho anahisi kitakuwa na manufaa kwa taifa??? Je sio uzalendo???

2. Lisu kakubali acacia ni wezi. Ssa kma kakubali acacia ni wezi kma ambavyo rais pia anaamini hivyo je kivp lisu sio mzalendo.

3. Lisu kasema tunaibiwa kwenye sheria sio mchanga. Kma ana nia mbaya angetukumbusha kuwa tunaibiwa kwenye sheria?? Si angekamaa kimya tu ajadili mchanga afu siri ya kuwa mikataba ni mibovu angekaa nayo kando kusubiri mambo yaharibike ndio aje kulaumu serikali kuu??? Je huo sio uzalendo???

Mkuu mimi binafsi sijaona shida kwenye tamko la lisu maana ni mawazo yake na wwe pia uko huru kuja na mawazo yako kinachosikitisha badala ya kuchukua ushauri wake muufanyie kazi mnaanza kumpinga kila mahala ssa mnafkiri dunia itaendeleaje bila mawazo kinzani??? Mnasema akaonane na rais wakati unasahau rais alishasema wakichagua mwanasiasa hatokaa akutane nao tena!!! Ssa ulitegemea atakubali ushauri wa lisu?? Lisu keshashauri sana hta akaishia kufungwa kule nyamongo na hta wakihoji sana walitimuliwa bungeni kwenye muswada wa gesi ssa mkuu kwa staili hii unafkiri kma miaka yote hawakuskiliza ndio watamsikiliza leo????

Je kivp lisu sio mzalendo??? Angeshauri???
 
Vile unavyo muelewa wewe ni kwa uelewa wako Mpendazoe yuko sahihi na wewe analytical yako hiyo huenda na weee you need more knowledge
Kivp lisu hamumuelewi?? Yye kasema mngeanza na sheria ila magufuli kaanza na mchanga??? Ssa kosa la lisu ni lipi hadi msimuelewe mumuite sio mzalendo???
 
Mpendazoe uko sahihi ila jua hata hawa wanaokupinga wsmeajiriwa kwa kazi hii. Wako kazini na ndo wabaya wasio na uzalendobkabisa wao hujali matumbo yao tu.
 
Tundu Lissu is a professional .rabble-rouser..





rabble-rouser
rab·ble-rous·er
ˈrabəl ˌrouzər/
noun
  1. a person who speaks with the intention of inflaming the emotions of a crowd of people, typically for political reasons.
    synonyms: agitator, troublemaker, instigator, firebrand, revolutionary, insurgent, demagogue
    "both the Republicans and the Democrats reluctantly have their own brand of rabble-rousers to contend with"

leo nimejifuza neno jipya...............
 
Kwa haraka haraka nimemsikiliza Tundu Lissu amekuwa na taharuki kubwa sana, amekulia katika zama za yeye kuwa ndiye kinara wa kushutumu wengine mafisadi. Kwa takriban miongo miwili ametambulika kama yeye ndiye mwenye hati miliki ya kuita wengine mafisadi.

Hata katika andiko lake linalozunguka amelalamikia ripoti ya Prof.Ossoro kuwa imefanya 'plagiarim', kwa wasioelewa maana ya neno hili 'plagiarism' ni kunukuu kazi ya mtu mwingine bila idhini au kumtambua. Tundu anamaanisha ya kuwa hata yale mapendekezo ya kamati ya pili kwa kiwango fulani yamenukuu kazi zake bila kumtambua,hivyo kapata jazba. Yaani yeye tu ndie aliyetakiwa aseme yale na yatambulike kuwa ni yakwake na apewe hati miliki na taifa na dunia litambue kuwa ni yeye Tundu Lissu.

Hii ina maana kuwa kamati ya Prof.Ossoro na wenzake hawakuwa na chao,walichofanya ni 'kugandamizia' maoni ya Tundu Lissu.

Hakika Tundu Lissu anabakia kuwa mtu mwenye kuchekesha na vituko vya kudumu kwa muda wote.
 
Kwa namna mambo yanavyokwenda, endapo Chenge na wenzake watapandishwa kizimbani haitashangaza kumuona Lissu mahakamani akiwatetea kama wakili wao. Naweka tahadhari tu makamanda msinishambulie!
 
Cha ajabu nini?
Yaani hilo Ndio tatizo linalowasumbua ccm! Mnataka mkisema Fulani mbaya basi asionekane wa kumtetea!
Shame!
 
Back
Top Bottom