Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi

equrorial guine ya malabo wanauchumi mzuri kuliko south africa
 
Watakuja hapa kutoka povu wakati hata hapo msumbiji hawajafika..

Tanzania tunafanya vizuri sana kiuchumi kwa nchi za Africa.. kuwa na fedha yenye thamani haimaanishi uchumi upo vizuri.. hata sisi pesa yetu ilikuwa na thamani miaka ile ya fixed exchange rate ila uchumi ulikuwa hoi.

Kuwa na fedha yenye thamani ndogo ni advantage kwa kuwa unavutia exports.. na hicho China walikifanya kwa kushusha thamani ya fedha zao ili wapate exports kubwa.

Sisi Tanzania ndio tunauzia chakula nchi nyingi zinazotuzunguka na nyingi ni zenye pesa ya thamani kubwa i.e. Zambia, Kenya etc.. sisi kuwa na pesa yenye thamani ndogo imepelekea mazao yetu kupata soko huko nje ya nchi..

Wanaoelewa wameelewa..
 
Zambia nilikwenda miaka 7 iliyopita fedha yetu ilikuwa na thamani kubwa kuliko yao sasa Kama wametuzidi mmh Not to that extent watch it. Natafakar kuhama nchi.
 
Hata vijijini hapa Wadanganyikaland nako unatokwa machozi maisha ya watu. Watu wanakunywa maji ya mtoni pamoja na mifugo na wanyamapori? Wanalala kwenye makeshift huts?
"Masomo niliyoyasomea yananitaka nifanye kazi remote areas kwa hiyo ninchokisema hapa siyo cha kishabiki.Naandika comment hii nikiwa Mpanda vijijini ndani huku.Tuna matatizo sawa sasa najaribu kulinganisha haya ya kwetu na nchi ambazo nimepita kwenye mazingira ya kufanana.Nimepita vijiji vya Congo DR,Central Africa,Togo,Ghana,Benin Burkina Faso,Ghana,Mali,Zambia,Senegal,Uganda,na sehemu za Afrika ya kusini Sasa nalinganisha maisha ya raia wa huko na sisi.Kusema kweli Viongozi wetu wa serikali wamejitahidi sana yaani sana.Nikupe mfano mdogo:Kutoka Lubumbashi kwenda Kinshasha ni mwendo wa saa 2 hivi kwa ndege.Ukitumia barabara na Landcruiser mpya hizi 71 series unatumia siku 30 kutoka Lubumbashi hadi Kinshasha na uwe na spare tyres kama 30.Ile barabara ni Makorongo kwa kwenda mbele.Narudia tena,Tanzania tuko vizuri kwa kulinganisha na nchi nyingine za Kiafrika.Mungu ibariki Tanzania.
Tanzania Shillings
1Kg ya maharagwe sawa na Dollar 1.5.
Shilling inaendelea kuimarishwa kwa uchumi wa viwanda
 
Ghana na Zambia wanashusha fedha zao baada ya inflation rate kuwa kubwa na hata Congo DR kama alivyopendekeza dada FaizaFoxy kwamba Sh.10,000 tuibadili isomeke Sh 10
TZS 10,000 iwe new TZS 10
Tzs 5,000 iwe new TZS 5
Tzs 1,000 iwe new TZS 1.
 
Kwa Zambia uongo mtupu.....mi juzi kati nilienda Lusaka...pale Tunduma nilichenji Tsh 100,000 nilipata kwancha 440,000

Sasa hapo currency gani yenye thamani?

Acheni uongo
 
Nimeishi Nairobi, Ela yao iko na Thamani kuliko Tanzania lakini Maisha yao ni magumu mno...Nikarudi fasta Bongo...
Kuna Tofauti kubwa kati ya unafuuu wa Maisha na Thamani ya Fedha...
 
Tupeane ramani mkuu
 
Ukiwa hospitali kwenye wodi ya mapumziko unaweza kujiona wewe unaumwa sana.. tena unaweza kuwa unalalamika madaktari hawakupi huduma nzuri.. ila inuka uende wodi ya wagonjwa mahututi utarudi ukishukuru Mungu..

Maendeleo yetu hayawezi kuja kwa kuwa negative kwenye kila kitu.. kila kitu tunapinga.. waTanzania tumeshindwa kujithamini na kutambua kuwa tuna bahati sana.. tunajisahau mno na kushindwa ku appreciate vile vidogo tulivyo navyo, hata kama sio perfect at least tu appreciate juhudi ambazo tumefanya mpaka hapa leo..

Hapa tulipo kuna watu hawajawahi hata kusikia mlio wa bunduki.. tunaishi kwa amani kwenye nchi ambayo ina fursa zisizoisha.. tunasahau kuna watu wamesoma lakini ni wakimbizi wanaishi kwenye mahema kwa kuwa nchi zao zimkosa amani..

Kuna nchi hapa Africa watu simu bado ni anasa.. ila leo asilimia 75 ya waTanzania wana simu za mkononi.. leo tuna uhuru wa kwenda popote, barabara nzuri na unauwezo wa kufanya biashara au kazi popote.. leo tuna lugha inayotuunganisha sisi wote ila bado hatujithamini kutwa kucha ni kulalamika tu. Hatuna shukrani kabisa.
 
Tuko mbali kwa maana ipi kwamba Hotel ni bei ya chini au nini maana hata hapa ukienda vijijini unatokwa machozi
 
Wewe nawe unatoa povu Tanzania tunafanya vizuri kuliko Nani? Au kwakuwa jamaa katoa mifano ya Vinchi ambavyo hata watu wa Bodaboda wanaweza kwenda kutupa mawe Ikulu ndio useme tunanafuu
 
Nimeishi Nairobi, Ela yao iko na Thamani kuliko Tanzania lakini Maisha yao ni magumu mno...Nikarudi fasta Bongo...
Kuna Tofauti kubwa kati ya unafuuu wa Maisha na Thamani ya Fedha...
Maisha yao ni Magumu au ni ghali?
 
Ni ghali na Magumu ...Kuishi mjini unatakiwa kuwa na akili nyingi ns uwe unapenda kufanya kazi kweli...Kuna mitaa ya Uswahilini Dar afadhali...
Maisha ya Nairobi ni ghali sio magumu wewe ukienda na hela zako za Bongo unakimbia sasa ukienda Kinshasa hadi balozi wetu anabeba chakula nyumbani hapafai
 
Maisha ya Nairobi ni ghali sio magumu wewe ukienda na hela zako za Bongo unakimbia sasa ukienda Kinshasa hadi balozi wetu anabeba chakula nyumbani hapafai
Ugumu wa Maisha ni nn???...Vitu gani vinasababisha ugumu wa Maisha??...Kuns uhusiano Wowote wa ugumu wa Maisha na Vitu kuwa ghali???
 
Ugumu wa Maisha ni nn???...Vitu gani vinasababisha ugumu wa Maisha??...Kuns uhusiano Wowote wa ugumu wa Maisha na Vitu kuwa ghali???
Kipato chao ni kikubwa wakati kipato chako kidogo sasa ukifika kule unashindwa. Mfano Nairobi parking ni Ksh 300 na gari zimejaa hapo Dar ni shilingi ngapi kwa siku na watu wanalia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…