Askarimaji
JF-Expert Member
- Jan 28, 2016
- 258
- 626
Mataifa 9 yenye uwezo mkubwa wa silaha hatari za nyuklia duniani
Kufuatia uvamizi wa Ukraine uliotekelezwa na Urusi, kitengo cha BBC Reality Check mwaka 2018 kiliangazia kule ambapo silaha za kinyuklia zipo na nani anayezimiliki.
Huku mkusanyiko mkubwa wa silaha hizo za kinyuklia ukidaiwa kupungua kwa kiasi kikubwa tangu vita baridi, kuna mamia ya vichwa vya kinyuklia ambavyo vinaweza kurushwa kwa ilani fupi, na wataalamu wanasema kila taifa linalomiliki silaha za kinyuklia lina mpango wa kuboresha zana zake za kivita.
Mataifa mengi yamekuwa yakiweka maelezo mengi kuhusu zana zake za kinyuklia kuwa siri kubwa , lakini inajulikana kwamba kuna mataifa tisa yanayomiliki zaidi ya silaha 9000 za kinyuklia ambazo zipo katika huduma za kijeshi.
Silaha hizi huenda zimepelekwa maeneo tofauti - ikiwemo ardhini, baharini na mengi zikiwekwa katika kambi za kijeshi ama hata katika hifadhi tu.
Takriban silaha 1800 zimewekwa katika hali ya tahadhari na huenda zikafyatuliwa bila onyo lolote.
Marekani na Urusi ndizo zinazomiliki idadi kubwa ya silaha za kinyuklia duniani.
Tangu mwaka 1970, nchi takribani 191 ikiwemo Marekani, China, Urusi, Uingereza na Ufaransa zilisaini makubaliano kuhusu masuala ya kudhibiti silaha za Nyukila (NPT). India, Israel na Pakistan hazijatia saini makubaliano hayo na Korea Kaskazini ilijiondoa mwaka 2003.
NPT inayatambua mataifa matano yenye silaha za nyuklia - Marekani, Urusi, Ufaransa, Uingereza na China - ambayo yote yalifanya majaribio ya silaha za nyuklia kabla ya makubaliano hayo kuanza kutekelezwa.
Chini ya mkataba ama makubaliano haya nchi hizi hazipaswi kumiliki silaha hizo wakati wote.
Mkataba huo unazuia mataifa yasiyotambuliwa na NPT kutengeneza silaha za nyuklia. Afrika Kusini, na nchi za zamani za Umoja wa Kisovyeti Belarus, Kazakhstan na Ukraine zote zimeacha kumiliki silaha hizo.
Mataifa yanapiga hatua za kuziondoa silaha za nyuklia?
Marekani, Uingereza na Urusi zote zimekuwa zikipunguza uwezo wake wa kumiliki vichwa vya kivita vya silaha hizo, Israel na Ufaransa zinasemekana kubaki na msimamo ule ule huku China, Pakistan, India na Korea Kaskazini zinaaminika kuzalisha zaidi silaha hizo, kwa mujibu wa Shirikisho la Wanasayansi wa Marekani.
Lakini kwa uchache sana, wataalam wanasema, kila nchi yenye silaha za nyuklia ina mipango ya kuboresha hifadhi yake ya nyuklia.
Kuziboresha silaha hizo ni kinyume na misingi ya Mkataba huo wa kudhibiti kuenea kwa nyuklia, anasema Shannon Kile, mkuu wa mradi wa nyuklia wa Sipri.
Uingereza inapanga kuibadili manowari yake ya nyuklia ya Vanguard, ambayo hubeba makombora yake ya nyuklia ya Trident. Ukubwa wa silaha hizo ztapunguzwa mpaka kufikia 180 katikati ya 2020s.
Marekani inaweza kutumia zaidi ya $1 trilioni mpaka kufikia 2040s kuboresha uwezo wake wa nyuklia. Baadhi ya vichwa vya silaha hizo vinapatikana maeneo mengi ya Ulaya kama Ubelgiji, Ujerumani, Italia, Uholanzi, na Uturuki, nchi ambazo zinahifadhi karibu vichwa 150 kati yao.
Korea Kaskazini ilifanya jaribio lake la sita la nyuklia mwezi Septemba na haijawa wazi kama mpango wa nyuklia wa Kim Jong-un una uwezo wa kuambatisha vichwa hivyo na kombora la masafa marefu.
Katika miezi ya hivi karibuni, Korea Kaskazini imeonyesha kuwa imezidi imarisha makombora yake ya kiwango cha juu.
Je, kutakuwa na ulimwengu usio na silaha za nyuklia?
Miezi michache baada ya kuingia madarakani, Rais wa Marekani Barack Obama aliwaambia maelfu ya umati wa watu mjini Prague kwamba chini ya utawala wake, Marekani "itatafuta amani na usalama wa dunia bila silaha za nyuklia".
.
Ilionekana kukaribia kufikia hatua ya dunia bila silaha za nyuklia kufiatia Julai 2017 zaidi ya nchi 100 ziliidhinisha mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupiga marufuku kabisa silaha za nyuklia.
Hadi sasa nchi kadhaa zimesaini makubaliano ya kisheria, yakiwa ni makubaliano ya kwanza ya aina yake kupiga marufuku wazi silaha za nyuklia. Hata hivyo mataifa yenye silaha za nyuklia yalisusia mazungumzo hayo.
Uingereza na Marekani zinasema kamwe hazina nia ya kujiunga na mkataba huo kwa sababu unadhoofisha NPT. Nchi washirika wa NATO pia zilishindwa kuyakubali makubaliano hayo mapya.
Askarimaji