Clemence Baraka
JF-Expert Member
- Sep 4, 2012
- 1,694
- 650
Ukweli umenena haswa. Watanzania tumlilie Mhe rais arejeshe jukumu hilo kwa hicho chombo cha serikali TPDC. Tumeshaumizwa sana. Moderator huu uzi ni muhimu sana na ingekua jambo la maana wachangiaji wawe wengi mpaka rais atambue kilio chetu kwa kuwa naamini anafuatilia sana jf binafsi au kupitia system zake.NILISEMA EWURA NI MZIGO IONDOLEWE KABISAA WAPEWE MADARAKA TPDC..WATUWALITENGENEZA MAWAKALA KWA MASLAHI YAO BINAFSI
NANII ASIEJUA UCHAPAKAZI WA TPDC...LEO TPDC INAKAZI GANI.....MH WAZIRI TUREJESHEE TPDC YETU
Sawa na Tshs 1,200. Huku Njombe Tshs 2,000Mafuta kenya ni kshs 60/= kwa lita.
Umenena mkuu, Mh. Magufuli tunaomba turudishie Maseru hapo ndio anapajulia, wapiga kazi bongo wana puuzwa sana sijui kwanini.Ewura ni jipu.
Ewura wanajua sisi ni vilaza,ni kweli mafuta yalitakiwa kuuzwa bei Hiyo hata wanauchumi wamesema diesel ilitakuwa iwe 1200 na petrol iwe 1350.Hoja na utetezi wa ewura ni too low na usanii mtupu, hakuna hoza yoyote yamsingi.
1. Gharama za usafiri
Mathematically kwenye hili anguko la bei hupaswi kuliongelea wala kulijumuisha suala la usafiri.
Mafuta yapande au yasipande variation za transport cost zita-vary kwa mfumo wake wa kawaida hatakama balaa la anguko hili lisingekuwepo hii variation ingekuwepo na contribution yake to this crisis nikama hakuna, (Hakuna sababu yamsingi hapa ila ulaghai wakutupwa)
2. Bei halisi ya mafutayaliyosafishwa.
Dunian kote hii bei sio fixed
ulaya na usa gharama kubwa ukilinganisha na middle east, iran, saudiarabia nk
Hawa ewura wanaongelea soko gan hasa la mafuta yaliyosafishwa/refined ambalo linaacount kwa ujumla wake anguko la mafuta ghafi dunian kote? huu ni uwongo na ubabaishaji wa hali ya juu. mfano kuwait na iraq gharama za chin mno .....
3. Ghara kupanda hapa kwetu kwa tofauti ya miezi miwili mbele baada ya huko yatokako.
Ewura wanashikiwa akili?....Mafuta yameanza kuporomoka zaidi ya miaka miwili ilopita 2013/2014.
Je miezi miwili anayoongelea huyu ewura anamaanisha miaka miwili? zaid ya miaka miwili bei imeshuka kutoka Tsh 2300 hadi tsh 2100/lita petrol (2300-2100)/2300 x 100 = 8% au shiling miambili tu ndo imepunguwa kwa kipindi cha miaka miwili......huu ni wizi wa waziwazi na uchafuzi wa uchumi kwa taifa letu kuukabidhi mikononi mwa wajanja wachache wagawane tuliowengi tukose.
4. kuporomoka thamani ya shilingi yetu dhidi ya usd.
a. Jan 2015 1 usd = tsh 1729 mafuta tsh 2300/litre of petrol (data zake ewura)
b. Dec 2015 1usd = tsh 2118 mafuta tsh 2100/litre of petrol (data zake ewura)
-pecentage change in usd cost = (2118-1729)/1729x100
=22.5% ....thaman ya tsh kuanguka .....hii itasabisha mafuta yapande bei kwa 22.5%
-percentage change in fuel tsh/lita petrol (2014 - 2016 Jan)
(2300 - 2100)/2300 x 100 = 8.7% yaan mafuta yameanguka kwa asilimia 8.7 sawa na tsh. 200 tu kwa miaka zaid ya miwili.
- kuporomoka mafuta ghafi ambayo kimahesabu anguko lake litaendasambamba kabisa na anguko la mafuta yaliyosafishwa kwa maana ya asilimia
(cost of crude oil fall price will vary directly proportional to fall in cost of refined oil all other costs remain unchanged...overhead cost, maintenance cost, transportation cost, tax etc)
percentage fall per berrel usd 130 in 2014 to usd 30 nov 2016
(130-30)/130 x100 = 77% yaan mafuta yameshuka kwa asilimia 77% katika miaka miwili tu sawa na anguko la usd 100 per berrel.
A. Jumla ya kupanda bei hapa nchin mafuta kwa lita ni sawa na asilimia za kushuka thaman shilingi yetu (hii inafanya mafuta yande ) kutoa anguko la bei ya mafuta kwa sasa.
= shilingi dhid ya usd - anguko halisi
= 22.5% - 8.7% zipo hapo juu nilivyozipata
= 13.8% (Hii ndio thaman halisi ambayo itaathili moja kwa maja uporomokaji wa bei yamafuta kutoka uds)
B. mafuta yameporomoka kwa 77% kwa sabab wamerikan wamefungulia zaid ya kiwango sokon na dola imeyapandisha kwa 13.8% hapa nchin kwetu, hivyobasi.....
Anguko halisi lilipaswa kuwa
= Anguko la mafuta sokon kutoa gharama zitokanzo na usd ......hapo juu
= Anguko la mafuta soko la dunia - Madhara ya usd .......hapo juu.
= 77% - 13.8%
= 63.2% .....hivyo basi, ilipaswa mafuta yashuke bei kwa asilimia kati ya 40 had 50 ukiacha asilimia zingine 13.2 for other unforeseen events kwa wafanya biashara.
Ewura wanatuletea maelezo yakisiasa mengi yauwongo na yasiyonaushawishi
kwa kadrio la chin ilipasa tuuziwe mafuta kwa punguzo la walau 40% ya bei ya january 2014 ambayo ilikuwa tsh 2300/lita ya petrol
= 1- 40/100 x 2300
= 1380/lita ya petrol
pamoja na punguzo la 40% bado mfanya biashara kabakiwa na zaid ya 20% inaelea mfukoni mwake kwa kila lita kukabiliana na mambo mengine tuki- assume faida yake haijaguswa atapata kama alivyokuwa akipata 2014
This EWURA IS A DEADLY ANIMAL.
Haina haja ya kuwepo Ewura sioni wanacho moderate,bulk procurement ipo Bora soko tu liamue bei na sio hao wapuuzi Ewura...kila sehemu wanatuumiza shenzi zao.Jamani kama kuna taasisi inayotakiwa kuvunjwa basi wangeanza na hii EWURA. Hiyo taasisi haijawahi abadani kumfarahisha mtanzania yeyote yule toka kuanzishwa kwake hamuwezi kuamini!? Zaidi zaidi imekuwa mzigo tu mana nayo ipo kati ya zile tozo unazolipa wewe mlaji wa mwisho... Mpaka kwenye LUKU,Maji n.k EWURA is the middle man.
Wao ndio Vilaza wa kutupwa,msomi Tangu Lini unakuwa mchumia tumbo? Ewura wafutwe jukumu wapewe TPDC ambao hawana % yeyote kwenye manunuzi.Mkurugenzi wa Ewura anasema Watanzania wanalalama hatujui kitu na pili anasema yanayoshuka ni mafuta ghafi si mafuta masafi..yangekuwa yanauzwa mafuta masafi pekee katika soko la dunia nadhani kwa mfumo wa Ewura tusingeweza kununua yangekua ghari sana..Hao Ewura hawajui kitu chochote waondoke tuu mimi sioni Faida ya wao kuwepo..
Wakuu, kuna issues hapa ziko straight na tuwe wakweli:
1. Amesema bei zinazotajwa per barrel ni za crude oil, na hivyo ni vizuri kuzingatia gharama zinazoongezeka kwenda white product. Hata tunapobisha lazima tuzingatie pia kwamba kuna gharama za refinery na transportation zitaongezeka tukizungumzia bei ya mafuta safi.
2. Kuna gharama za usafiri na Bima (CIF ) zinaongezeka pale kwenye bei ya mafuta safi.
3. Mafuta yaliyopungua bei leo hapa yatauzwa baada ya miezi miwili kwa sababu za kuyanunua, kusafirisha
4. Tusisahau kuwa serikali yetu inachukua kodi kwenye mafuta karibu sh 600.
5. Kwenye website yea ewura kuna matangazo ya bei ambazo hutolewa kila Jumatano ya kwanza ya mwezi, ni vema tukaangalia iwapo bei ya mafuta imekuwa na tabia gani hivi karibuni? Nimeangalia katika miezi miwili ya hivi karibuni bei zimekuwa zikishuka.
6. Kwa nini tunasema mafuta huwa yakipanda soko la dunia basi bei huwa zinapanda mara moja wakati ukweli ni kuwa bei hutangazwa mara moja tu kwa mwezi? Kila Jumatano ya kwanza ya mwezi. Tujadili haya kwa ufahamu wetu, bila hiyana wala choyo.
Weka Data za kweli na si za kukisia,navyojua pipa moja linaingia litres 200 that means 1 ltr inanunuliwa kwa Tsh 315,Wameweka Bulk Procurement kupunguza gharama na serikali ilisema ni very cheap hapa tuweke gharama za kusafirisha,tuweke gharama za kusafisha,tuweke kodi ya serikali,na tuweke Faida ya muuzaji,je ni halali kuuza 2000?Wakuu, kuna issues hapa ziko straight na tuwe wakweli:
1. Amesema bei zinazotajwa per barrel ni za crude oil, na hivyo ni vizuri kuzingatia gharama zinazoongezeka kwenda white product. Hata tunapobisha lazima tuzingatie pia kwamba kuna gharama za refinery na transportation zitaongezeka tukizungumzia bei ya mafuta safi.
2. Kuna gharama za usafiri na Bima (CIF ) zinaongezeka pale kwenye bei ya mafuta safi.
3. Mafuta yaliyopungua bei leo hapa yatauzwa baada ya miezi miwili kwa sababu za kuyanunua, kusafirisha
4. Tusisahau kuwa serikali yetu inachukua kodi kwenye mafuta karibu sh 600.
5. Kwenye website yea ewura kuna matangazo ya bei ambazo hutolewa kila Jumatano ya kwanza ya mwezi, ni vema tukaangalia iwapo bei ya mafuta imekuwa na tabia gani hivi karibuni? Nimeangalia katika miezi miwili ya hivi karibuni bei zimekuwa zikishuka.
6. Kwa nini tunasema mafuta huwa yakipanda soko la dunia basi bei huwa zinapanda mara moja wakati ukweli ni kuwa bei hutangazwa mara moja tu kwa mwezi? Kila Jumatano ya kwanza ya mwezi. Tujadili haya kwa ufahamu wetu, bila hiyana wala choyo.
Savimbi,Weka Data za kweli na si za kukisia,navyojua pipa moja linaingia litres 200 that means 1 ltr inanunuliwa kwa Tsh 315,Wameweka Bulk Procurement kupunguza gharama na serikali ilisema ni very cheap hapa tuweke gharama za kusafirisha,tuweke gharama za kusafisha,tuweke kodi ya serikali,na tuweke Faida ya muuzaji,je ni halali kuuza 2000?
Product after refining Diesel+LPG+oil+petrol.
2000 = 315+X+Y+Z+V???
Naomba tujue gharama
X=Usafirishaji per litre
Y=Kusafisha per litre
Z=Kodi ya serikali per litre.
V= Je Faida inatakiwa iwe ngapi?
Twende kwa Data ,Ewura watupe majibu hayo na si bla bla,wekeni data.
Aiseee Mchawi wetu kumbe ni serikali Daaa nimechoka kodi za utitiri hadi basi khaaaa ndio shida ya serikali isiyo bunifu badala ya kukusanya kwenye migodi huko wanabana huku kwa the multitude.Savimbi,
Mkuu Savimbi, hesmima mbele mkuu. Kama unavyosema, ni busara tu tuzungumze kwa data. Kwanza upate uhakika ukisikia barrel ni lita ngapi? Kuna tofauti kubwa ya ujazo na kila product itatoka kwa kiwango gani kwenye hilo pipa? Hapa chini ni baadhi ya argument nilizopata na inaonesha kuna viwango mbali mbali...huwezi kupata kiwango kimoja cha dizeli kwa mfano, inatoka lita ngapi kwenye crude oil.
"It differs based on the type of Crude Oil. It can be 70 litres or 40 litres or even less. There are different types of crude oil in the market.
One barrel = 157 litres. But after proccessing it comes to 166 litres. There are some 1500 byproducts which can be produced from crude oil. The IOC produces around 150 byproducts.
source: Mtandao.
Katika kodi za Tanzania, Petroli ni sh 752 katika kila sh 1,800 unayotoa kununua mafuta. Dizeli kodi ni sh 628, Kerosene ni sh 575.
Freight haiko fixed. Inabadilika kutokana na msafirishaji atakuwa amequote kiasi gani kwenye tender za Bulk Procurement System. Zaidi ya kodi za serikali na freight, kuna handling charges za Bandari, Processing fees za TRA (hii siyo kodi), handling charges za Weight and Measures, EWURA, na Local Authorities, pengine nitazitafuta kwa uhakika nilete hapa. Lakini zaidi ya hapo kuna faida ya tunaowekeza kwenye hiyo biashara ambayo ina vary kati ya sh 109 na na 90 kwa lita kutegemea ama Muuzaji wa jumla au wa reja reja.
Hii ina maana kuwa,mafuta hata ukipewa bure kule, kwanza utalipia usafiri na kodi, ambazo ziko hapo juu.
At least kwa figures tunaweza kudadavua jambo, lakini Adolay mbona umelundika figures za assumption tu bila hata kodi, ambayo ni component kubwa sana katika pricing?
Mkuu Heshima kwako Mchawi nishamjua ni nani.Savimbi hicho unachokishangaa ndicho usichokijua. Kodi siyo jambo la siri. Pekua hata bajeti ya serikali itamwambia. Na zinaongezeka kila mwaka. Tatizo wengi tunasikilizia kodi za laga kwanza. Hiyo 100 yako siyo kodi. Ni tozo ya mfuko wa umeme vijijini...JK alishaondoa ruzuku kwenye mafuta ya taa miaka 3 iliyopita wewe unashtuka leo?
Shikamoo..Weka Data za kweli na si za kukisia,navyojua pipa moja linaingia litres 200 that means 1 ltr inanunuliwa kwa Tsh 315,Wameweka Bulk Procurement kupunguza gharama na serikali ilisema ni very cheap hapa tuweke gharama za kusafirisha,tuweke gharama za kusafisha,tuweke kodi ya serikali,na tuweke Faida ya muuzaji,je ni halali kuuza 2000?
Product after refining Diesel+LPG+oil+petrol.
2000 = 315+X+Y+Z+V???
Naomba tujue gharama
X=Usafirishaji per litre
Y=Kusafisha per litre
Z=Kodi ya serikali per litre.
V= Je Faida inatakiwa iwe ngapi?
Twende kwa Data ,Ewura watupe majibu hayo na si bla bla,wekeni data.
Mkuu Heshima kwako Mchawi nishamjua ni nani.