Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 3,893
- 7,426
Nipo Coco beach now nimepitia hapa kupunga upepo kwani niliumiss flan hivi.
Kulia kwangu kuna Akina dada wanapanda farasi huku wanapiga picha kuweka kumbukumbu,nyuma kidogo kuna wamasai ambao wamechill Chini ya mnazi wanawaza mambo yao, mbele yangu wanapita wadada watatu wa kizungu wanafurahia Jambo Fulani kutokana na mwonekano wao.
Sasa hivi kuna mwamba mmoja anapita na mtoto mkali wa kizungu, halafu huyu mwamba anaswaga za old school coz ameshika Redio kubwa na mapiano ndiyo Ngoma inayosikika.
Kwa mbali kuna wadau wanaogelea na wanainjoy kana kwamba hawana madeni kabisa.
Kwa kifupi we are having gud time hapa.
Anyways ngoja nifungue code husika
Upande wa kushoto kama Mita 50 toka nilipokaa kuna mabinti wawili wamechill kwenye viti vya plastic, mara mwamba mmoja anagitaa mkononi akawasogelea na kubadilishana mawili matatu, jamaa naona ni wale jamaa wanaotumbuiza Kwa malipo.
Mara jamaa anaanza kuimba na huku anapiga gitaa lake, nafuatilia Kwa Makini Sana kama muandishi WA Al Jazeera!
Naona jamaa kamaliza kisha kuna jambo kaongea halafu watoto Wazuri wakaanza kucheka, nikaongeza umakini zaidi coz Kule Cuba tulifundishwa tuwe Makini zaidi na watu ambao wako na furaha Sana au huzuni Sana coz huwa wanajisahau na kuuza mafaili yao.
Mara jamaa anatoa Simu yake na kumkabidhi binti mmoja na mara paap binti anabonyeza bonyeza kumaanisha anampa namba mwamba, na Simu inarudishwa kwa mwamba na furaha inatawala pale.
Swali langu je Mabaharia mnafeli wapi kupata namba za Warembo?
Huu Uzi unakujia live toka Coco beach
Ngoja niendelee kuinjoy.
Ni hayo Tu!