JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,666
- 6,428
"Madhali umetia nia kugombea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Naomba simama imara, usitetereke, usiwe na hofu na wala usikubali kutishwa. Chama kiko pamoja na wewe. Pia tuna Wanasheria; ambao wako tayari kukusaidia wakati wowote." amesema Ester Thomas.
Aidha, Bi. Ester Thomas amewakumbusha watia nia hao dhima na wajibu wa Mwenyekiti wa Mtaa kwenye maendeleo ya mtaa. Amesema kwenye mitaa na vijiji ndiko wanakoishi wananchi na huko ndiko inapopita na kufanyika miradi ya maendeleo.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji utafanyika Novemba 27, 2024 na ACT Wazalendo ni miongoni mwa vyama vinavyokwenda kushiriki uchaguzi huo.