Epuka kuweka vifaa vya kuwasha na kuwaka moto karibu na watoto

RIGHT MARKER

Senior Member
Apr 30, 2018
136
498
Mhadhara (82)✍️
CHUKUA TAHADHALI KABLA YA HATARI.


Watoto wa sikuhizi ni watundu sana, hivyo katika uzi huu tunakumbushana mambo madogo ambayo yanaweza kusababisha madhara makubwa ndani kwako.

Wale wavuta sigara mnaotumia viberiti vya aina mbalimbali kwa ajili ya kuwashia sigara zenu. Wamama mnaotumia viberiti kwa ajili ya kuwashia majiko ya kupikia ndani kwako, na matumizi ya vifaa vingine ambavyo vinawaka moto.

Hakikisha baada ya kumaliza kutumia kifaa hicho (kiberiti) weka mbali na watoto, weka eneo ambalo si rahisi mtoto kufikia au kuchukua. Kinyume chake mtoto mtundu anaweza kuchukua kiberiti na kuwasha kwenye mapazia, sofa, nguo, godoro, au popote ndani ya nyumba.

Wale ambao mnatumia majiko ya gesi (hasa majiko ya mitungi mikubwa) ni vizuri unapomaliza kutumia jiko lako zima kwenye mtungi (kwenye sehemu ya kuzima na kuwasha) ili kama mtoto atachezea jiko isiwe rahisi kutokea chochote. Kinga ni bora kuliko tiba.

RIGHT MARKER
Dar es salaam.
 
Back
Top Bottom