SoC04 Elimu za shule ya msingi (masomo) ni mzigo mkubwa sana hasa kwa watoto ambao hawajui maisha yao ya baadaye

Tanzania Tuitakayo competition threads

ofmae

New Member
May 11, 2024
2
1
Elimu za shule ya msingi (masomo) ni mzigo mkubwa sana hasa kwa watoto ambao hawajui maisha yao ya baadaye yatakuja kuwa upande upi, labda huenda mtoto akawa daktari, rubani, mcheza soka au michezo miingine ya sasa inayoingizia vijana kipato.

Mwanafunzi wa shule ya msingi anaposoma masomo zaidi ya tisa inakuwa ni mzigo mkubwa sana na baadhi yao huwa hawaelewi wasome yapi zaidi na kuacha yapi kwa sababu suala la kuchagua masomo yapi yatakuwa bora kwa mtoto sio suala dogo kwa sababu pale wengi huwa hawajui ni nini hasa wanaweza zaidi isipokuwa ni wazazi na baadhi ya walimu ndo wanaweza kujua kiurahisi.

Ushauri wangu kama ifuatavyo.
Watoto wafundishwe jinsi ya kuwa wazalendo na wawe ni wenye kuipenda nchi kuliko maslahi ya mmoja mmoja kama walivyo viongozi wengi wa Afrika na hata hapa kwetu Tanzania. Yapo mafunzo mengi ambayo mtoto anaweza kufundishwa na akaelewa thamani ya nchi yake na hii itasaidia kuepuka kupata viongozi wala rushwa na mafisadi. Badala ya kuweka masomo mengi yasiyo na faida yachaguliwe masomo kadhaa tangu darasa la nne na hapo mtoto ataweza kujifunza masomo machache na somo la uzalendo likiwepo na huku watoto wakishiriki kwa vitendo kuipenda nchi yao na kuwa wazalendo, licha ya kuwa na somo la uzalendo pia somo liingine ambalo ni muhimu zaidi ni elimu ya fedha kuanzia shule za msingi kwa sababu kuna watu wengi wamefanya vizuri wakiwa shule ila kwenye maisha wanashindwa jinsi ya kutumia pesa zao na wengi wao wanakufa maskini kwa sababu tu ya kushindwa kutumia pesa kama inavyotakikana hatakama walipata pesa nyingi kipindi cha nyuma.

Masomo yawe machache na wanafunzi waanze kuchagua/kuchaguliwa masomo yao wanapofika darasa la nne tu kulingana na ufaulu wao kwa maana hakuna haja ya mtoto/mwanafunzi kusoma masomo kwa mda mrefu bila kuyafanyia kazi.

Kwa maana kwa kawaida binadamu hawezi kujua vitu vyote tangu anazaliwa mpaka anapokufa, tukifanya hayo ndani ya miaka 5-25 ijayo tutakuwa tumepata mabadiliko makubwa sana kwanza serikali itakuwa haitumii nguvu kubwa kupata wataalam wabobezi kwenye sekta fulani fulani kwa maana tayari mwanafunzi anapochagua upande wa kuupigania tangu akiwa darasa la nne au la tatu anakuwa ana masomo yake kadhaa ambayo atakuwa na uwezo wa kuyafanyia kazi kwa mda mrefu na hii inaongeza umakini na ubobezi kwenye taaluma ambayo anakuwa ameisomea kwa mda mrefu.
Yapo masomo kwa mfano Historia umuhimu wake ni mdogo sana kwa sababu dunia imebadilika sana na sasa tupo ulimwengu wa taarifa ambao sidhani kama historia ni muhimu sana, yapo mambo muhimu kama elimu ya fedha ambayo tangu pesa imeanza kutumika mpaka sasa inaendelea kutumika kila mahali ila wengi wetu hatujui ni kwa namna gani tunaweza kukuza kipato kidogo kwenda kuwa kikubwa na bado tunapambana na historia 🤣

Wanafunzi wanasoma masomo mengi sana bila maana ndomana unakuta wanafunzi wanasoma ili wafaulu mtihani tu, ukimpeleka akafanyie kazi kitu alichosoma unakuta hajui.

Ufupisho
1. Wanafunzi wapewe nafasi kwa kuchagua masomo ya kusoma darasa la nne tu na idadi ya masomo ipunguzwe hapo.

2. Watoto wafundishwe uzalendo shule ya msingi na sekondari.

3. Elimu ya fedha iwe rasmi mashuleni kuanzia shule za msingi.
 
mtoto ataweza kujifunza masomo machache na somo la uzalendo likiwepo na huku watoto wakishiriki kwa vitendo kuipenda nchi yao na kuwa wazalendo, licha ya kuwa na somo la uzalendo pia somo liingine ambalo ni muhimu zaidi ni elimu ya fedha
Nikipendekeza kwamba hiki ulichokinena hapa, ndiyo haswaa kilichopelekea hayo masomo mengi yakawepo. Yameonekana kuwa na faida na ndiyo maana ikaitwa elimu ya msingi. Masomo yote yalionekana ni ya msingi kwa watoto kabla hawajafikia kuchagua huko sekondari.

Maana anaweza tokea mzazi akauliza kuwa, ya nini kumjaza masomo ya fedha na uzalendo wakati mtoto anataka kusomea urubani wa ndege za biashara na kuishi ulaya. Kuhusu mambo ya fedha atamlipa 'financial analyst' wake kama tu tunavyowalipa wanasheria utamjibuje??
 
Nimezungumzia masomo machache ikiwa na maana baadhi ya masomo yapuguzwe na watoto wachaguliwe masomo yao mapema kwa sababu inapofikia darasa la nne, waalimu, wazazi na hata mwanafunzi mwenyewe anakuwa na mwanga wa kuwa anafanya vizuri hasa kwenye masomo gani.

Kuhusu elimu ya fedha sio kila mzazi anaweza kumlipia mwanaye (financial analyst)
 
Back
Top Bottom