Elimu ya juu huleta umasikini

Nimekuwa nikijiuliza Mara nyingi kuwa elimu inayotolewa nchini Tanzania hulenga nini na ni faida kwa nani? Sio Siri imechukua muda mrefu kutambua kuwa elimu ya Tanzania hususani ya juu huwapoteza watu katika direction ya maisha. Serikali ingeweka mfumo ambao mtu akisoma awe na uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri pia tofauti na ilivyosasa.

Mtu anamaliza chuo kikuu akirudi mtaani hana tofauti na yule aliyekomea la saba labda tofauti ya kuvaa yaani msomi atakuwa anamodoa nguo zake lakini wa la saba anavaa kipapaa.

Wale ambao wameajiriwa ni watumwa, mfano mwalimu anakipindi kimoja kwa wiki lakini analazimika kuhudhuria shuleni muda wote wa kazi yaani SAA 7:30 mpaka 3:30 harusiwi kutoka njee ya kituo cha kazi kufanya Mishe zake.

Umewahi sikia kuna mwalimu tajiri? Umewahi sikia kuna nurse tajiri? Umewahi sikia kuna askari tajiri? Umewahi sikia kuna dactari tajiri? Utajiri umeumbwa kwa ajili ya nani? Kwanini ung'ang'anie kutafuta ajira? Watu wamekuwa wakisoma ili wapate makaratasi(vyeti) bila kujua makaratasi hayo yanamchango gani kimaisha.

TAFUTA FEDHA USITAFUTE ELIMU

Umeanza vizuri ila hapo kwenye bold umechemka. ..
Kwanza tupe scale ya utajiri.
Pili kwa taarifa yako wako madaktari matajiri, walimu maskari n.k
Kuhusu elimu ya Tanzania ... kasoro kubwa iliyopo ni kwamba ile inayoitwa elimu ya msingi siyo kabisa. Haimpi msingi mwanafunzi huyo.
Wataalam wa elimu wangeifumua na kuweka somo la Umahili wa kazi somo ambalo lingemfanya kila mtu awe makini kwa lolote analofanya.
Mi nawafahamu mafundi wa kushona ambao ni matajiri kabisa na wamefikia hatua ha kuajiri.
Namfahamu mwalimu mmoja mfugaji wa kuku wa kienyeji aliamua kuhachana na ajira na kuendelea na ufugaji,,, ni tajiri mkubwa tu.
Kuhusu maaskari ao sitaki kuwaongelea kwa sababu kila mtu anajua utajiri wao umeegemea wapi.
Nasisitiza UMAHILI WA KAZI ... hili ndilo somo ambalo kimsingi lingemkomboa mtanzania.
 
Tukumbuke kusoma sana sio kuelimika ila kuwa na busara ni zaidi ya elimu ya darasani
Kitu cha kujiuliza ni je! yale unayoyaelewa yanakusaidia kwenye maisha? kama jibu ni ndiyo shukuru Mungu, kama jibu ni hapana ujue we ni maskini kama maskini wengine.

Kuna vijana wanajua kunyoa tu nywele wana maisha mazuri sana ...

na

Kuna vijana wame graduate fani mbali mbali wanaishi maisha ya shida.

KATI YA HAO WAWILI NANI AMEELIMIKA?
 
Alie na uhakika wa kula ndo ameelimika
 
Hapa ndio unafiki wa watanzania unapojidhihirisha! Sasa mnatajaje? Mtu asiposoma mnamwita kilaza/bashite wanaosoma, mnawaambia wanapoteza muda! Sasa mnataka nini?
 
Sio unafiki, ukiwa hujasoma lakini ukaendesha mambo yako kadri inavyotakiwa (bila uongo) nani atakusema.
Huyu kijana wa Arbert, Kihiyo na wengine wanasemwa kwa kuwa walidanganya umma kuwa wamesoma kumbe hakuna.
 
MTU mwenye Mali huilinda Mali yake
MTU mwenye elimu .elimu yake humlinda
MTU mwenye Mali kadiri anavyoitumia hupungua
MTU mwenye elimu kadiri anavyoitumia huongezeka MTU mwenye Mali huwa na maadui wengi
MTU mwenye elimu huwa na marafiki wengi
 
Lakini naomba kuuliza wasomi wengi wenye elimu kuanzia masters na kuendelea si wanazichukua nje ya Tanzania? Je usomi wao nje ya nchi umeleta utofauti na wale walio soma ndani ya nchi? Majibu pls
 
Nimeishaliongea hilo ... MSINGI
 
Sasa naamini jF ina members ambao hamjitambui kabisa. Ni nchi gani duniani umesikia kila anayasoma basi kaajiriwa? Na si kila mtu eti kwa sababu kasoma basi anaweza jiajiri, baadhi ya fani lazima ziwe financed na serikali au mashirika mengine. Mfano wewe ni Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo, utaweza kuanzisha hospitali ya upasuaji moyo???
Soma kitabu kinaitwa Rich CASHFLOW Quadrants kifanyie kazi kitabu baada ya miaka mitano niletee zawadi ya subaru ni moja ya vitabu vimebadilisha maisha yangu.
Watanzania wengi tunasoma ili tu professional employer instead to be professional investors.
Wakati mwingine kama huna hoja ya maana kuleta jF bora ukae kimya.
 
Back
Top Bottom