Elimu ya juu huleta umasikini

nombo toby

Member
Aug 9, 2016
47
41
Nimekuwa nikijiuliza Mara nyingi kuwa elimu inayotolewa nchini Tanzania hulenga nini na ni faida kwa nani? Sio Siri imechukua muda mrefu kutambua kuwa elimu ya Tanzania hususani ya juu huwapoteza watu katika direction ya maisha. Serikali ingeweka mfumo ambao mtu akisoma awe na uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri pia tofauti na ilivyosasa.

Mtu anamaliza chuo kikuu akirudi mtaani hana tofauti na yule aliyekomea la saba labda tofauti ya kuvaa yaani msomi atakuwa anamodoa nguo zake lakini wa la saba anavaa kipapaa.

Wale ambao wameajiriwa ni watumwa, mfano mwalimu anakipindi kimoja kwa wiki lakini analazimika kuhudhuria shuleni muda wote wa kazi yaani SAA 7:30 mpaka 3:30 harusiwi kutoka njee ya kituo cha kazi kufanya Mishe zake.

Umewahi sikia kuna mwalimu tajiri? Umewahi sikia kuna nurse tajiri? Umewahi sikia kuna askari tajiri? Umewahi sikia kuna dactari tajiri? Utajiri umeumbwa kwa ajili ya nani? Kwanini ung'ang'anie kutafuta ajira? Watu wamekuwa wakisoma ili wapate makaratasi(vyeti) bila kujua makaratasi hayo yanamchango gani kimaisha.

TAFUTA FEDHA USITAFUTE ELIMU
 
Mkuu huwa una akili sana ukiacha pombe za kienyeji.

Kimsimgi China wanatoa vocational skills education kwa kundi kubwa ambalo ndilo linaloendesha uchumi kwa maana ya cheap skilled labour na kundi dogo wanapata higher educational wawe administrators na ndio reasons US na dunia nzima wanashift viwanda vyao kule maana wanataka cheap labour ila sio kama hawa wa kwetu ambao ni unskilled labour.

Kwa maandishi hayo nadhani utakuwa umeona suluhisho na madhara ya kutengeneza kundi kubwa la wasomi wasio na vigezo na walio na Elimu kubwa isiyowasaidia.
 
Serikali kuweka mfumo ni vigumu ww mwenyewe unayesoma unatakiwa ujitambue kwa nn unasoma elimu ya juu ,faida /hasara za kusoma elimu hiyo lazima uzitambue, tofauti na hapo utakuwa unatwanga Maji kwenye kinu.
 
Unaposema askari tajiri,mwalimu tajiri,nurse tajiri unatumia kigezo gani kuujua utajiri wa MTU? Au utajiri wa namna gani unaouelzea hapa?
Kwani watu wa kada tajwa hapo wanafanya kazi usiku na mchana ili iweje!?

Its simple wa nataka utajiri wa masese, shekeli, au visenti mkuu. Utajiri wa roho wangeenda kwa Gwajima na kuachana na kazi zao maana huo unapatakina huko.
 
Kwani watu wa kada tajwa hapo wanafanya kazi usiku na mchana ili iweje!?

Its simple wa nataka utajiri wa masese, shekeli, au visenti mkuu. Utajiri wa roho wangeenda kwa Gwajima na kuachana na kazi zao maana huo unapatakina huko.
Unatafsiri VIP utajiri ndugu? Unadhan kua na hela ndio utajiri? Unajua kutofautisha mwenye Mali na MTU aliefanikiwa?? Unajua kuutofauyisha utajiri na mafanikio??? Labda unachanganya HIV vitu viwili
 
Unatafsiri VIP utajiri ndugu? Unadhan kua na hela ndio utajiri? Unajua kutofautisha mwenye Mali na MTU aliefanikiwa?? Unajua kuutofauyisha utajiri na mafanikio??? Labda unachanganya HIV vitu viwili
Nafahamu Niko kazini nachapa kazi ila nitarudi kukufafanulia zaidi juu ya hili na utaelewa vizuri tu.
 


si kila mtu lazima awe tajiri hapa duniani wengine wanatoa huduma kwa jamii imagine tusingepata madaktari, profesa, halafu umeongelea nesi mbona huwa wanaishia form four tu wanaenda chuo hawafiki elimu ya juu
 

Sasa naamini jF ina members ambao hamjitambui kabisa. Ni nchi gani duniani umesikia kila anayasoma basi kaajiriwa? Na si kila mtu eti kwa sababu kasoma basi anaweza jiajiri, baadhi ya fani lazima ziwe financed na serikali au mashirika mengine. Mfano wewe ni Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo, utaweza kuanzisha hospitali ya upasuaji moyo???

Wakati mwingine kama huna hoja ya maana kuleta jF bora ukae kimya.
 
havaimplicationsost: 19962116 said:
Tena elimu ya bongo ndio uchafu kabisa unakuta MTU anaelimu ya theory tu lakn implications hana uwezo wowote
Hapo kwenye implications ndo umenifurahisha! Yaani kwa kweli elimu ya bongo hakuna implications kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…