Dunia kusimama kuelekea mpambano wa kukata na shoka kati ya Anthony Joshua na Wladimir Klitschko

AJ ndio habari ya dunia kwasasa ....huyo hana ngumi za kupapasa ....anapiga kama anaua ....


Bora na wewe umeliona hili ,ndio maana nikamuuliza huyo jamaa hapo juu kama anamjua AJ kweli au amesimuliwa tu ,maana bwana mdogo balaa lake sio la kitoto ,huyo Klitshko asipoangalia atatolewa knockout round za mwanzo kabisa
 
Kweli ngumi zimekosa wababe siku hizi yaani Wradimir toka enzi za kina lewis bado ana hadhi ya kupigana uzito wa juu??..dah..enzi zile wababe kibao huku tyson kule lewis huku bruno pale evander kule oliver macall huku rahman pale botha huku nani sijui yaani ilikua ni ubabe mpaka mtu unatetemeka kuangalia mechi..lkn siku hizi eti joshua na mzee gani sijui linaitwa pambano la kihistoria
Enzi zile kila pambano ni la kukata na shoka
 
AJ anawarudisha wengi kwenye ushabiki wa heavyweight boxing, na ataleta washabiki wapya na wapenzi wengi wa mchezo huo
 
Aj yupo vizuri...kadri kila pambano anavyopigana ana improve..kinachomsaidia ngumi zake zina power ambapo mpinzani ikikupata lazima ukae chini..
..Klitschko tatizo moja ngumi zake hazina power Kama Aj..itachukua mda mpaka amkalishe chini.

..Favourite mpaka Sasa AJ..but in boxing anying can happen.
 
Nenda you tube kachungulie knockout za AJ then urudi hapa ....
Mkuu wataje mabondia watatu wa hadhi ya kua contenders ambao AJ kawapiga, nani na nani? Hakuna. Wote aliowapiga ni journeyman (last time I checked). Huyu na Deontay ilibidi wazipange kwakua wote walikua na lengo la kutengeneza rekodi wakakimbiana Deontay akaenda kwa Chris Arreola.

AJ kwa Klistchiko kaenda kwa sababu hata akipigwa tutasema kapigwa na the best, angepigwa na Deontay angechukua muda kurudisha reputation.

Sina 1m ya kuweka dau, lakini tukikubaliana kununuliana soda mimi nawekeana hilo dau.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom