Dr. Ndalichako anaonesha njia, tumuunge mkono

Binafsi nmefurahishwa sana na juhudi anazofanya huyu waziri katika kuhakikisha anarudisha nidhamu na ubora wa elimu yetu hapa Tanzania. Nasema haya kwa mambo makuu mawili aliyoyasimamia huyu mama:

1. Suala la wanafunzi wa St Joseph ambao walikuwa wanasoma degree huku wakiwa wametoka direct form 4 ambako pia hawakuwa na sifa hata za kuchukua cheti.

Inasadikika kwamba takribani wanafunzi 480 walikuwa wanaendelea na masomo yao ya degree katika chuo hicho. Hii ni dhahiri kwamba baaada ya miaka miwili ijayo tungekuuwa na waalimu ambao hawana sifa kabisa za kutufundishia watoto wetu.

Waziri kalisimaia suala hili na kwakweli anastahili pongezi na tumuunge mkono katika hili.

2. Suala la wanafunzi takribani 8000 wa special diploma ya ualimu UDOM. Nilishawahi kuhoji kuhusu uhalali wa hawa wanafunzi ambao walikuwa ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na wengi wao wakiwa na ufaulu hafifu wa div 3 (Tena ndo zilee za GPA). Program hii ilianzishwa kwa agizo la Raisi aliyepita ikiwa ni njia ya kupunguza uhaba wa waalimu wa science mashuleni.

Ni kweli kabisa kwa idadi yao wangeweza kuziba pengo la waalimu wa science mashuleni, lakini Je, ubora wao ukoje? wanastahili kweli na wanao uwezo wa kufundisha hesabu, physics na chemistry kwa ngazi ya o-level na mwanafunzi akaelewa?.

Ni dhahiri tulikuwa tunaandaa vijana weng wasio kuwa na sifa kwa ajili ya kuwafundisha vijana wetu. Naamini kwa waalimu wa haya masomo na yeyote aliyesoma PCM advance ataelewa ninachosema,

Ingawa suala hili bado lipo kwenye mjadala, ni dhahiri kuwa Waziri na wizara nzima wanalitafakari kwa makini jambo hili. Kwa ushauri wangu kwa kuwa vijana hawa wamepotezewa muda wao mwingi, wangesambazwa kwenye vyuo vya ualimu vilivyopo nchini kwetu wakamalizia masomo yao, halafu wakasambazwa kwenye shule zetu za msingi. Huko wangekuwa na ufanisi mkubwa sana kuliko kwenye shule za sekondari.

Tumuunge mkono waziri Ndalichako na serikali kwa ujumla kwa juhudi hizi wanazofanya za kufufua elimu yetu.
kwa anayofanya Mh ndalichako na serikali kwa ujumla katika kurudisha ubora wa na heshima kwa elimu ya tanzania in sahihi kabisa ila kwa swala wanafunzi takribani 7000 wa chuo kikuu cha Dodoma waliokua wanasoma special diploma ya elimu kwa msomo ya sayansi kupewa masaa 24 kwa siku ya jumapili Jana siyo sahihi kabisa kwani serikali ingetafuta njia sahihi ya kuwasaidia hao wanafunzi kama vile kuwasambaza kwenye vyuo vya ualimu na wakihitimu wanaenda kuwa walimu katika shule zetu za msingi na Haya yote yasingetokea, naomba kuwasilisha
 
"Kwenye nchi za wenzetu huwezi kusomea ualimu kama huna division one" mwisho wa kunukuu

"Kwenye nchi za wenzetu huwezi kumfukuza mwanafunzi kama mwizi tena chini ya ulinzi mkali kwa kosa ambalo siyo la kwake" mwisho wa kunukuu.
 
huyu mama yuko sahihi ila wengi walioguswa wako huku wanachangia hoja kumpinga, bahati mbaya kwa uwezo wao duni wa kielimu wanashindwa kujenga hoja huyu mama aachwe arudishe hadhi ya elimu
 
Hao wanafunzi hawana sifa za kufundisha Sekondari labda serikali iwahurumie tu iwasambaze kwenye vyuo vya ualimu ili wamalizie kozi yao then wapelekwe shule za msingi lakini sekondari jamani HAPANA, kwanza wengi wao hawana ufaulu mzuri na ukizingatia hao ndo wapelekwe tena sekondai!!! hapana.

Namna walivyoondolewe nadhani serikali italifanyia kazi tu hakuna tatizo
hapo umenena mkuu nakupa 100%
 
"Kwenye nchi za wenzetu huwezi kusomea ualimu kama huna division one" mwisho wa kunukuu
Wanafunzi wenye Div one wanasoma udaktari,uhandisi ama uhasibu ambazo baada ya kumaliza na kafanikiwa kupata ajira. muda mfupi tu baada ya kupata ajira wataweza kulipa madeni yote waliokopa kwa ajili ya kufadhili masoma na pia kuweza kuwa na maisha mazuri tofauti na ualimu.
 
Binafsi nmefurahishwa sana na juhudi anazofanya huyu waziri katika kuhakikisha anarudisha nidhamu na ubora wa elimu yetu hapa Tanzania. Nasema haya kwa mambo makuu mawili aliyoyasimamia huyu mama:

1. Suala la wanafunzi wa St Joseph ambao walikuwa wanasoma degree huku wakiwa wametoka direct form 4 ambako pia hawakuwa na sifa hata za kuchukua cheti.

Inasadikika kwamba takribani wanafunzi 480 walikuwa wanaendelea na masomo yao ya degree katika chuo hicho. Hii ni dhahiri kwamba baaada ya miaka miwili ijayo tungekuuwa na waalimu ambao hawana sifa kabisa za kutufundishia watoto wetu.

Waziri kalisimaia suala hili na kwakweli anastahili pongezi na tumuunge mkono katika hili.

2. Suala la wanafunzi takribani 8000 wa special diploma ya ualimu UDOM. Nilishawahi kuhoji kuhusu uhalali wa hawa wanafunzi ambao walikuwa ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na wengi wao wakiwa na ufaulu hafifu wa div 3 (Tena ndo zilee za GPA). Program hii ilianzishwa kwa agizo la Raisi aliyepita ikiwa ni njia ya kupunguza uhaba wa waalimu wa science mashuleni.

Ni kweli kabisa kwa idadi yao wangeweza kuziba pengo la waalimu wa science mashuleni, lakini Je, ubora wao ukoje? wanastahili kweli na wanao uwezo wa kufundisha hesabu, physics na chemistry kwa ngazi ya o-level na mwanafunzi akaelewa?.

Ni dhahiri tulikuwa tunaandaa vijana weng wasio kuwa na sifa kwa ajili ya kuwafundisha vijana wetu. Naamini kwa waalimu wa haya masomo na yeyote aliyesoma PCM advance ataelewa ninachosema,

Ingawa suala hili bado lipo kwenye mjadala, ni dhahiri kuwa Waziri na wizara nzima wanalitafakari kwa makini jambo hili. Kwa ushauri wangu kwa kuwa vijana hawa wamepotezewa muda wao mwingi, wangesambazwa kwenye vyuo vya ualimu vilivyopo nchini kwetu wakamalizia masomo yao, halafu wakasambazwa kwenye shule zetu za msingi. Huko wangekuwa na ufanisi mkubwa sana kuliko kwenye shule za sekondari.

Tumuunge mkono waziri Ndalichako na serikali kwa ujumla kwa juhudi hizi wanazofanya za kufufua elimu yetu.
Awamu ya nne uchafu
 
njia gani hiyo watoto wa shule tena wa kike wanateseka look at u.

swissme
 
Nimeshangaa wabunge wametoka nje eti kupinga maamuzi ya spika.. Hivi wabunge walitaka wajadili nini kuhusu awa watoto.. Bunge linaingilia kazi za executive waache kielehele.. Hizi ni ishu za kitaaluma hao wabunge karibia wote hawajui chochote kuhusu utengenezaji na usimamizi wa mitaala.
 
Kwenye education hakuna kitu kinaitwa special diploma ya miaka mitatu.. Kuna certificate mwaka mmoja, diploma miaka miwili na degree miaka mitatu... Hii special diploma ni jina kupunguza makali ila hii ni degree.. Imagine mtoto wa form four anaenda kusoma degree ya ualimu wa sayansi.. Kisha akitoka hapo anaenda kufundisha secondary.

Sielewi ata walitumia mtaala wa wapi kupanga hii course... Mbaya zaidi kuna watu wanatetea alafu kesho awa awa watakuja kusema walimu wetu ni mabomu.

Ni heri tuumize kwa muda watu elfu 7 kuliko kuja kuumiza vizazi vingi sababu ya walimu feki.

Ndalichako kafanya uamuzi mzuri sana sema kawa too strict angeingiza siasa kidogo kuwa wanawapa likizo ya muda ili washughulikie swala lao then wawapangie vyuo vya certificate za primary education.
 
Serikali iwapeleke kwenye vyuo vya shule ya msingi,huu ni upuuzi yaani fm 4 mwenye Div 3 ndo akafundishe sayansi O level? Upuuzi ulioje si bora hata wale walimu wa vodafasta walikua fm 6.Ndalichako tuko pamoja komaa,next year hakikisha div.2 and above ndo wanaenda ualimu na anzisha mpango wa kuwapa mafunzo kazini walimu wote na wawe certified kwa kufanya mitihani kwa grade 3 tofauti,watakaofeli wapishe maana huko kuna failures wengi sana
 
Ifikie hatua watu tukaachana na siasa katika masuala nyeti kama elimu,swali la kujiuliza kama Jk asingetoa wazo la kuwa na kozi hiyo maalumu kama inavyodaiwa na watu,hao vijana waliotimuliwa wangekuwa wapi hivi sasa?na wangekuwa wanafanya nin? inapaswa tutafakari hali ambayo wangekuwa nayo wakati huo kisha tufananishe na mbeleke waliyobebwa nayo kama ingeweza kuwa na tija kwa taifa,.

Haiwezekani taifa linalojipanga kuja kuwa taifa la viwanda kuwaandaa wataalamu wa hivyo viwanda chini ya usimamizi wa watu ambao hawajakizi viwango vya kielimu,

Kumbukeni si kila jambo linapaswa kupingwa kwa kuwa unamihemko ya kupinga na kufuata upepo,piga picha asara ambayo taifa lingepata endapo hao vijana wangekuja kuwa waalimu hapo baadaye,utagundua kuwa anaweza kuzalisha vilaza zaidi ya milioni 2 kwa miaka mitano ijayo,sasa hapo ndoto ya kuwa na taifa lenye viwanda itakuwepo tena?
 
Mleta mada utakuwa moko sio bure uwezi kusema watu wasome diploma miaka mi3 chem&maths&phys&biology af wakafundishe shule ya msingi
 
Tatizo watu wanafikiria kila mtu anaishi kwa kupigiwa kura. Kwamba hata shughli za kitaalamu kama ya huyu mama na elimu yake, eti apigiwe kura kama anafaa kuw awaziri wa eilimu ama hafai!. Ujinga!.

Mama Ndalichako alikuta Elimu ya kina Mulugo na Binam Shukuru iko kama jumba la sanaa kaole.

Huyu mama anakazi kubwa kuliko unavyoweza kufikiria. Ninachoomba asiondolewe kupisha uchunguzi kwa sababu hakuna cha kuchunguza. Kinachotakiwa aombwe atoe mwongozo wa mwelekeo wa elimu, atautekeleza naman gani kwa miaka mitano na apimwe kwa lipi. Kumshikia kasi kwa wizara hiii ilvyokuwa ni sawa na kuhalalisha watu wote wakiwa hyo wizara wawe kama mulugo na kawambwa, wafanye kama awamu ya jk ili wasiulizwe maswali.

Ninaomba watendaji wa wizara wampe ushirkiano sana. Tatizo na uzuri wa huyu mama si mtu wa maneno mengi. Ni mtu wa malengo na vitendo. Waliozoea talalilah wanaona hafanyi kwa kuwa hapigi domo.

Ninarudia tena kusema. Mama Ndalichako aachwe akomboe elimu ya taifa. Apewe muda aandae mpango wa kukabiliana na changamoto zilizopp ambazo kazikukuta likiwemo la ufaulu wa kubumbwa, kushuka kwa elimu, n.k. Apewe ushirikiano katika mahitaji ya raslimali za kutekeleza mpango huo na kwa uzito wa kipekee, usomi na umakini wake uheshimiwe.

Wabunge nawaomba sana watambue siyo kila mtu anapigiwa kura. Lazima wajue kama wangelikuwa wanachunguzwa wao kwa utaalamu, basi wenye vyeti fake wasingekuwemo bungeni. Wengye ufaulu kama wa Ms Marwa wasingekuwemo. Ni vizuri wtambue nafasi yao na inapoishia lakini waache maswala ya kitaalamu wasiyaingilie unless iwe ni katika kusaidia katika uboreshaji. Kama vile elimu ya jk na washikaji wake waliyvoua elimu na bunge halikuweza kupima wala kushtuka wala kuhoji na hata Mbatia aipojitahidi kuwaeleza hawakuelewa, ni dhahiri haya mambo kwao ni makubwa sana.

Majungu hayatalisaidia taifa. JK aliharibu sana hii nchi na kwa kuonyesha mauaji ya taifa ni pale alipoua elimu. Huyu mama hana kazi ndogo. NINARUDIA KUSEMA APEWE USHIRIKIANO LAKINI SI KUMWABIA APISHE UCHUNGUZI. UCHUNGUZI WA NINI? MBONA JESHI LA POLISI PAMOJA NA KASHFA YA LUGHUMI HAKUNA ALIYEPISHA UCHUNGUZI? HABARI ZA MAKONTEINA YA BANDARINI, NANI ALIPISHA UCHUNGUZI? HABARI ZA ESCROW HATUJASIKIA UCHUNGUZI WOWOTE?

TUNAOMBA SERIKALI IANZA KUCHUNGUZA HAYA MAUFISADI SUGU, KABLA HAIJAANZA KUWAVURUGA WATAALAM WANAOFANYA KAZI YA ZIADA KULIKOA TAIFA.
Mkuu, hii ndiyo tunaita Great thinker. Kitu ambacho watu wrngi sana wanakikosa. Hongera mkuu
 
Ukiona mtu anampinga Profesa Ndalichako utambue kuwa mtu huyo either ana cheti feki au ana elimu ya kuungaunga aliyoipata kiujanjajanja hivyo ana hofu kuwa elimu yake itabatilishwa.Kwa watu wasio na maslahi binafsi ya kuficha elimu feki zao ni lazima wamuunge mkono Profesa Ndalichako, tunataka elimu bora na sio bora elimu.
 
Ifikie hatua watu tukaachana na siasa katika masuala nyeti kama elimu,swali la kujiuliza kama Jk asingetoa wazo la kuwa na kozi hiyo maalumu kama inavyodaiwa na watu,hao vijana waliotimuliwa wangekuwa wapi hivi sasa?na wangekuwa wanafanya nin? inapaswa tutafakari hali ambayo wangekuwa nayo wakati huo kisha tufananishe na mbeleke waliyobebwa nayo kama ingeweza kuwa na tija kwa taifa,.

Haiwezekani taifa linalojipanga kuja kuwa taifa la viwanda kuwaandaa wataalamu wa hivyo viwanda chini ya usimamizi wa watu ambao hawajakizi viwango vya kielimu,

Kumbukeni si kila jambo linapaswa kupingwa kwa kuwa unamihemko ya kupinga na kufuata upepo,piga picha asara ambayo taifa lingepata endapo hao vijana wangekuja kuwa waalimu hapo baadaye,utagundua kuwa anaweza kuzalisha vilaza zaidi ya milioni 2 kwa miaka mitano ijayo,sasa hapo ndoto ya kuwa na taifa lenye viwanda itakuwepo tena?
Naaam, well said mkuu. Tatizo letu kama watanzania ni kwamba tunachukulia kila kitu kama siasa tu. Katika kujenga taifa la wasomi na viwanda kama kweli watu mko serious ni lazima kwenye masuala ya elimu kama haya watu muweke siasa pembeni mfanye kazi. Tunalaumu namna walivyoondolewa chuoni, lakini Je ni namna gani walitakiwa kuondolewa? Na issue hapa sio kwamba hawa vijana wamefukuzwa, naamini ni mabadiliko tu ya utaratibu na naamini serikali itawapeleka sehemu ambayo wanastahili kuwepo na wakawa na uafanisi kwa taifa kama waziri alivyosema.
 
ELIMU hasa ni nini?.Na mtu mwenye elimu yukoje? Hivi kuna tofauti gani kati ya mtu mwenye elimu na mtu aliyeelimika?
 
Kwenye education hakuna kitu kinaitwa special diploma ya miaka mitatu.. Kuna certificate mwaka mmoja, diploma miaka miwili na degree miaka mitatu... Hii special diploma ni jina kupunguza makali ila hii ni degree.. Imagine mtoto wa form four anaenda kusoma degree ya ualimu wa sayansi.. Kisha akitoka hapo anaenda kufundisha secondary.

Sielewi ata walitumia mtaala wa wapi kupanga hii course... Mbaya zaidi kuna watu wanatetea alafu kesho awa awa watakuja kusema walimu wetu ni mabomu.

Ni heri tuumize kwa muda watu elfu 7 kuliko kuja kuumiza vizazi vingi sababu ya walimu feki.

Ndalichako kafanya uamuzi mzuri sana sema kawa too strict angeingiza siasa kidogo kuwa wanawapa likizo ya muda ili washughulikie swala lao then wawapangie vyuo vya certificate za primary education.
Kipi kimebadilika zaidi ya watu? Chama kilekile sasa wakat wote hamkujua mtanguliz wake anavuruga elimu acheni unafiki hii wizara hovyo tangu kipind cha Mkenya akija waziri mpya anakuja na mambo yake yaani hatuna mipango yenye muendelezo
 
Mkuu TUTUO haya maisha ni ya kwetu na yanaendelea, kitu ambacho amekiharibu aliyepita sio lazima kibaki vilevile eti kisa kisafanywa. Kama kuna nafasi ya kukirekebisha hebu tukirekebishe. Hawa vijana wateteeni waende huko mashuleni ni sisi wenyewe tutakaoanza kulaumu tena kwamba walimu hawafundishi, watoto wanafeli. Wanafunzi, watoto wangu na wa kwako watafaulu vipi ikiwa mwalimu mwenyewe hakufaulu?
 
Back
Top Bottom