Dodoma: Wabunge Ester Bulaya na Halima Mdee Wafungiwa Vikao vya Bunge kwa mwaka mzima

kwanini spika hakutaka kumskiliza Mnyika hili nalo swali,furaha yenu nikuwa bunge litaendelea kuwa la ndiooo bila challenge za hawa wazalendo
furaha yetu mimi na nani?
mambo mengine ni mnayakuza tu, aliitwa mwizi, wewe unajua aliesema mwizi ni nani?
challenge ziwakilishwe kwa ustaarabu msifanye upinzani uonekane kama genge la wahuni, halafu watata alwys ni walewale inamaana wapinzani wengine humo bungeni sio wazalendo
Sijawahi kuona Mbowe anatolewa juujuu hivyo kama imewahi kutokea nikumbushe? je na yeye si mzalendo?
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Baada ya wabunge watatu wa CHADEMA kukiuka maadili ya Bunge, hatimaye Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge imetoa hukumu na hatimaye kuridhiwa na Wabunge wengi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika azimio hilo la Bunge imeamriwa kuwa wabunge Esther Bulaya, Halima Mdee na John Mnyika watasimama kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda wa mwaka mmoja na kwamba wataanza kushiriki vikao hivyo kuanzia Bunge la Bajeti la mwaka 2018/2019.

Hii ni adhabu kali sana hasa kwa mbunge Esther Bulaya ambaye mapema leo amesikika akijutia makosa yake na kuomba bunge limsamehe kutokana na majukumu aliyonayo kichama na kifamilia.

Naye John Mnyika amesema hajui nini kilitokea mpaka akasababisha kutolewa nje kwani anaamini kuwa haikuwa ni utashi wake kuzua mabishano.

Walio jirani na Halima Mdee nao wamemsikia akisikitika makosa aliyofanya. Hata hivyo kwa vile alishaonywa na bunge kumuombea msamaha, yupo tayari kutumikia adhabu atakayopewa kwani kwa kosa alilotena hadhani kama bunge litamsamehe tena.

Poleni sana CHADEMA
Kwa hiyo tuitane wezi bungeni na kuchafua "jina la MTU" kisha ndio unaamua hivyo. Kesho mwingine akikuita mwizi utamfungia anaetaka urekebishe kauli au????
 
Hayo ndo maajabu ya bunge letu la tz. Ukubwa wa adhabu na kosa lenyewe haviendani kabisa. Inatuonyesha jinsi uchama ulivyo mbele kuliko utaifa. Hebu jiulize wabunge wa ccm hawana makosa??
 
Kama hukumu imepita, Mbona adhabu kubwa sana hii ... 1 year duuuh something wrong here!!!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Adhabu imetolewa na Lizabon hao ndio CCM bwana
Hahahahahaaaaa! Juzi nilitaka maoni yenu baada ya wabunge hao kuonesha utovu wa nidhamu. Niliwahoji kama Bulaya na Mdee wanastahili msamaha tena. Kwa masikitiko makubwa napenda kuwafahamisha kuwa wachangiaji wengi walitaka wabunge hao wanyukwe adhabu kali
 
Duh mkuuu uko serious???? Hivi hii nchi tunaipeleka wapi??? Yaani mtu anaonewa watu wakiretaliate wanaonekana ndio wauwaji afu aliyekosea anabaki ndani
Kuna wakati ni rahisi kuona majibu ya ni kwanini Tanzania ni maskini. Katika akili ya kawaida kabisa inashangaza kuona mtu anadhani kwamba kufukuza wabunge bungeni ni jambo la maana zaidi kuliko kuwaacha wakashiriki mijadala yenye kuisaidia nchi. Halima na Bulaya, kwa bahati nzuri ni resources na michango yao ina msaada mkubwa kwa nchi. Huwezi kulinganisha michango ya wabunge hao wawili na wabunge wa aina ya Kibajaji! Sasa kuwafukuza wasishiriki mijadala bungeni kwa sababu ambazo haina shaka zimechangiwa na kiti chenyewe kushindwa kudhibiti hasira na mhemko tu wa kiitikadi, ni kielelezo kwamba kama taifa tuna tatizo.

Kiti makini tayari kingekuwa kiliishabaini kuwa chenyewe ndicho kilisababisha yote yaliyotokea, na hivyo suala la akina Halima na Bulaya lingeweza kumalizwa kwa hekima tu. Kufukuzafukuza wabunge bungeni haina tija kwa nchi maskini kama hii ambayo inahitaji mijadala na mawazo yenye tija kutoka kwa wabunge wenye tija. Kutimuatimua wabunge bungeni ni kuzima mijadala, ni kuwanyima wananchi haki ya kuwakilishwa na ni kuikosea serikali ambayo inahitaji sana michango ya wabunge katika kuwaletea maendeleo wananchi. Tufike mahali sisi waajiri wa kiti (kwa maana ya analipwa kodi zetu) tukipigie kelele mambo kama haya maana bado ni kweli kwamba kufukuzafukuza wabunge haiwezi kuwa ndio suluhu kwa uadilifu kama kiti chenyewe hakiwezi kuwa sehemu ya huo uadilifu wenyewe!
 
Hahahahahaaaaa! Juzi nilitaka maoni yenu baada ya wabunge hao kuonesha utovu wa nidhamu. Niliwahoji kama Bulaya na Mdee wanastahili msamaha tena. Kwa masikitiko makubwa napenda kuwafahamisha kuwa wachangiaji wengi walitaka wabunge hao wanyukwe adhabu kali

Yule aliyemtukana Mnyika amepewa adhabu gani hujajibu?
 
Back
Top Bottom