Dodoma: Wabunge Ester Bulaya na Halima Mdee Wafungiwa Vikao vya Bunge kwa mwaka mzima

Kwahiyo unaona sawa kina bulaya kufungiwa ilihali mbunge wa CCM aliyesababisha yote haya yupo nje anadunda????hivi we dada unajielewa kweli
 

Kuwa mbunge atakuwa mpaka watu wa KAWE tuseme basi.Na kama kutukanwa kwa wapinzani ni sahihi kweli walifanya kosa,lakini waliomtukana Mnyika amechukuliwa hatua gani?
 
Mkuu sikutarajia kila mpenda haki kushabikia ujinga huu..... yaani mnyika kaonewa hamuoni shida ila wakiretaliate ndio mnaona kuna shida?? Hivi nchi mnaipeleka wapi?? Muufute upinzani basi tujue kimoja
 
Spika Ndugai amedhibitisha hivyo kwa kusoma vifungu vya bunge na hukumu iliyotolewa na kamati ya Haki na maadili ya bunge kutoa hukumu hiyo ya kutokuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya bajeti ya mwaka 2017/18
Amesema kwamba Halima mdee ambaye ni mbunge wa Kawe amepewa adhabu hiyo ambayo ni baada ya msamaha wa adhabu aliyopewa mara ya kwanza lakini bado akavunja kanuni nyingine pamoja na Mbunge wa Bunda Ester Bulaya
 
Kwa kiwango chako cha uelewa, uamuzi kama huu una faida gani kwa Bunge lenyewe, serikali na kwa wananchi? Nini maana ya maadili?
 
hii yote katika kutetea maslahi ya taifa na ni ujinga mkuu kwa mtu mwenye utimamu kama wewe kuandika upuuzi kama huu,huku ukishangilia ndioo za wabunge wa ccm alafu kesho wanaruka kimanga yale waliyo yapitisha,so endelea kuota ndoto zako za mchana kuwa 2020 hawata rudi wakati kwa upuuzi waccm na raisi wao watanzania hawatakubali kurudisha tena akili ndogo kuunda serikali
 
kwa bunge hili la wagonga meza waende tu. bungelimepoteza dira. limeshindwa hata kupitisha bajeti zenye maana....

Ile ilikuwa ni azma ya Bunge kuwatoa wapinznai ili BAJETI zao zipite.Nitashangaa sana kama Upinzani hawakujua hilo.Na ukimsikiliza between the lines NDUGAI amesema wawe wanasoma mienendo ya wabunge wa CCM,kwa hiyo yule aliyetukana alipangwa kutukana,na hawezi kuchukuliwa hatua sababu ilipangwa
 
Kwahiyo unaona sawa kina bulaya kufungiwa ilihali mbunge wa CCM aliyesababisha yote haya yupo nje anadunda????hivi we dada unajielewa kweli
hio adhabu ni sawa kabisa, sasa kama Bulaya kilichomtoa nje ni nini?
alitaka akapumzike ndio kapewa likizo hio
Ofcoz Ndungai alitakiwa ampe warning aliesababisha hilo kama alivyowapa warning upinzani waliomtukana
Kuitwa mwizi mnafanya big deal maneno mangapi mabaya yametamkwa bungeni mpaka hilo liwe kubwa kwa Mnyika kama sio mpenda attention tu!!!
hio adhabu inawafaa, siku nyingine wakiambiwa kaa chini waheshimu kiti cha spika period!
 
Ukimsikiliza Ndugai alivyohitimisha ni kwamba alijazwa na chuki na visasi dhidi ya Halima Mdee na Esther Bulaya.Sijui kama anakumbuka kuna mbunge wa CCM aliyetukana wabunge na hajaguswa
 
kwanini spika hakutaka kumskiliza Mnyika hili nalo swali,furaha yenu nikuwa bunge litaendelea kuwa la ndiooo bila challenge za hawa wazalendo
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Baada ya wabunge watatu wa CHADEMA kukiuka maadili ya Bunge, hatimaye Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge imetoa hukumu na hatimaye kuridhiwa na Wabunge wengi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika azimio hilo la Bunge imeamriwa kuwa wabunge Esther Bulaya, Halima Mdee na John Mnyika watasimama kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda wa mwaka mmoja na kwamba wataanza kushiriki vikao hivyo kuanzia Bunge la Bajeti la mwaka 2018/2019.

Hii ni adhabu kali sana hasa kwa mbunge Esther Bulaya ambaye mapema leo amesikika akijutia makosa yake na kuomba bunge limsamehe kutokana na majukumu aliyonayo kichama na kifamilia.

Naye John Mnyika amesema hajui nini kilitokea mpaka akasababisha kutolewa nje kwani anaamini kuwa haikuwa ni utashi wake kuzua mabishano.

Walio jirani na Halima Mdee nao wamemsikia akisikitika makosa aliyofanya. Hata hivyo kwa vile alishaonywa na bunge kumuombea msamaha, yupo tayari kutumikia adhabu atakayopewa kwani kwa kosa alilotena hadhani kama bunge litamsamehe tena.

Aidha, Mheshimiwa Rhoda Kunchela, Suzan Kiwanga, Saed Kubenea, Kahtan Kahtan wamepewa onyo kali baada ya kusikika wakimtukana Spika Ndugai kwenye viunga vya Bunge

Poleni sana CHADEMA
 
Halafu unaowasemea wote wako Moshi,hebu acha uongo Lizabon.Wakikaa Bungeni ndiyo familia zao zinalishwa au wanapata mishahara yao?
 
NADHANI WAMEPEWA ADHABU KUBWA SANA KULINGANA NA MAKOSA WALIYOTENDA. HAWA NI WABUNGE WAZURI TU, VIJANA, NA WAJENGA HOJA IMARA KUSAIDIA NCHI. WAMELIFANYA BUNGE LICHANGAMKE. TATIZO NI KWAMBA SERIKALI INA STRESS NYINGI WAKATI HUU NA WANAONA HAWA KAMA MAHALI PA KUTOLEA HASIRA. BINAFSI NAONA HARUFU YA UBAGUZI NA UPENDELEO WA KICHAMA UNAOFANYWA NA SPIKA WA BUNGE, SIUNGI MKONO. WALA HAITUSAIDII.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…