Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,011
- 6,753
Serikali ya Tanzania imetangaza kuwaruhusu wanafunzi waliokatiza masomo yao kwa kwasababu ya kupata mimba kurejea masomoni kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi.
Akizungumza na wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi nchini humo, Katibu mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk Leonard Akwilapo amewataka wakuu hao wa vyuo kuhakikisha kuwa wanafunzi wa kike walioshindwa kuendelea na masomo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba wanarudi na kuendelea na masomo. Amewataka wakuu hao wa vyuo kutekeleza agizo hilo la kudahili wanafunzi hao kupitia mpango wa elimu haina mwisho ifikapo mwaka 2022.
Pamoja na kutaka vyuo vyote vya maendeo ya wananachi viwe vimesajiliwa kama vituo vya kufanyia mitihani ya kidato cha pili na kidato cha nne, amesema hatua hiyo ya kurejesha wanafunzi wa kike waliokatiza masomo yao yanatokana na majadiliano ya muda mrefu ya wizara hiyo na benki ya dunia.
Katibu mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk Leonard Akwilapo
'Tulikuwa na mabishano mazungumzo marefu kwenye mpango wa kuimarisha na kuboresha elimu ya sekondari hapa nchini, moja ya makubaliano , ilikuwa ni kutoa fursa kwa wasichana ambao wamekatiza masomo kwa njia yoyote ile, wapate fursa ya kurudi na kuendelea na masomo, na tukasema tutatumia vyuo vya maendeleo ya wananchi, lazima tuanze hatuna uwanja, sio suala la kujadiliana, mambo mengine ya walimu mtatuachia sisi', alisema Dk. Akwilapo.
Kwa mujibu wa maelezo hayo, wanafunzi hao watarejea darasani katika vyuo 54 kuanzia mwakani, ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano ya kuboresha elimu ya sekondari pamoja na kuwapa fursa wasichana waliokatiza masomo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba kupata haki ya elimu.
Aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli alipiga marufuku wanafunzi wanaopata mimba mashuleni kuendelea na masomo ya shule ya msingi na sekondari hali iliyozua mijadala na makelele kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu nchini na nje ya nchi hiyo.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania Zitto Kabwe aliwahi kuiandikia Benki ya Dunia kusitisha kuikopesha Tanzania dola milioni 500 za elimu kabla ya mabadiliko ya kisera kufanyika.
Vyama vya upinzani nchini Tanzania na wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo na wa kimataifa wamekuwa wakitishia shinikizo la kutotolewa kwa mkopo huo mpaka pale Tanzania itakaporuhusu wanafunzi wanaopata ujauzito waruhusiwe kuendelea na mfumo rasmi wa elimu.