Dkt. Koboko tosheka na majukumu ya Udaktari, mwache Mfamasia kwenye eneo lake la madawa

Kama mfamasia Hawezi kuprescribe anatoaje dawa KWa mgonjwa direct KWa mgonjwa ,hoja zake hujajibu hata MOJA ,unazunguka mbuyu na kuludi pale
 
Sidhani kama ulimuelewa Prof Koboko
Nilimwelewa sana!! Hataki mfamasia atoe dawa moja kwa moja kwa mgonjwa pale pharmacy! Ati kwa sababu mfamasia hayajui magonjwa!! Nimemnukuu hapa:

"✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa, kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwa hiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa."

Mfamasia hatibu, ila ni mtaalamu wa madawa na anaweza kutoa dawa kwa mgonjwa kwa mujibu wa prescription kwa dawa zinazohitaji prescription. Koboko hataki kabisa mfamasia kutoa dawa kwa mgonjwa!! Anataka daktari ahudumie hospitalini na kwenye pharmacy pia!!
 
Kama mfamasia Hawezi kuprescribe anatoaje dawa KWa mgonjwa direct KWa mgonjwa ,hoja zake hujajibu hata MOJA ,unazunguka mbuyu na kuludi pale
Si kazi ya mfamasia kuprescribe dawa wala pharmacy si mahali pa kuhitaji prescription!! Anayehitaji prescription aifuate kwa daktari hospitalini!! Ni makosa makubwa kwa mgonjwa kwenda pharmacy halafu ategemewe huko kupata prescription. Ni lazima jamii ielimishwe!! Tukiendekeza watu kufuata prescription pharmacy, hizi pharmacy zitageuzwa kinyemela kuwa dispensary!!
Mfamasia hawezi kutoa dawa kwa mgonjwa kama hiyo dawa inahitaji prescription ya daktari na hayo ndiyo maadili ya wafamasia!

Hakuna haja ya daktari kuwa pharmacy maana pharmacy si mahali muafaka pa ku-practice udaktari!! Daktari akiona anahitaji kukaa pharmacy na aende kusomea tena shahada ya pharmacy miaka 5 (pamoja na internship yake)!!
 
Nakupongeza kwa uelewa wa kutokwenda directly pharmacy kununua dawa bila kumwona daktari!! Ila kwa suala la cheti cha mfamasia kuwepo dukani huo ni uthibitisho kuwa hiyo pharmacy inahudumiwa na inasimamiwa na mtaalamu wa madawa hivyo kuhakikisha usalama wa huduma inayotolewa hapo!! Ni takwa la lisheria duniani kote, vinginevyo kila mtu atajifanya kufanya kazi hiyo na ni hatari sana kwa jamii. Huo siyo ulaji bali ni kazi muafaka inayostahili MALIPO!! Wanapata hayo malipo kihalali kwa kusimamia usalama wa dawa na wateja!
 
wafamasia ni nyoka wakubwa sana, wala rushwa na wezi wa madawa ya serikali. ninyi watu ninyi, kama kuna mtu huyu aja duka la dawa au pharmacy hahitaji kulijua hili. na pia wana bifu kubwa na madaktari hata sijui kwanini.
 
Dakika ya 89'
Prof Koboko 3-0 Mbingunikwetu
Ni sawa kabisa kama refari ni wa mitaani asiyejua sheria ya mchezo!!!
Anachodai Kobobo ni yeye kupractice udaktari kwenye pharmacy wakati kwenye pharmacy siyo mahali pa kupractice udaktari!! Kwa refa asiyejua sheria za mchezo wa tiba atampa goli Koboko, lakini kwa refa anayejua vizuri mchezo wa tiba atasema goli nsiyo halali maana umefunga kwa kuotea kinyume na sheria.
Pili Koboko anamzuia mfamasia kupractice kwenye pharmacy wakati mahali sahihi pa mfamasia kupractice ni kwenye pharmacy!!!!
 
Kilichonishangaza eti Pharmacist hajui diagnosis... Eti Pharmacist hajui chochote...
Huyu Koboko ndiye anampotosha Waziri wa Afya..
 
wafamasia ni nyoka wakubwa sana, wala rushwa na wezi wa madawa ya serikali. ninyi watu ninyi, kama kuna mtu huyu aja duka la dawa au pharmacy hahitaji kulijua hili. na pia wana bifu kubwa na madaktari hata sijui kwanini.

Hawa wafamasia wasiofuata sheria jamii iwashitaki panapohusika. Kosa la mfamasia mmoja au baadhi ya wafamasia lisichukuliwe kuwa ni kosa la taaluma yote ya pharmacy!! Anayekiuka au aliye mwizi wa dawa za serikali ashughulikiwe kivyake!!
Kwani nani hapa anaweza kusema madaktari wote hawachukuagi rushwa? Kati ya sehemu zinazosumbua kwa rushwa ni pamoja na hospitalini, polisi na mahakamani!!
Anayekiuka ashughulikiwe bila kupepesa macho na siyo kulaumu taaluma yote!!
 
Kama mfamasia Hawezi kuprescribe anatoaje dawa KWa mgonjwa direct KWa mgonjwa ,hoja zake hujajibu hata MOJA ,unazunguka mbuyu na kuludi pale
Kisheria kuprescribe ni kazi ya daktari na sio mfamasia na kazi ya kutoa dawa kwa mgonjwa ni pharmacist. Kutoa dawa kwa mgonjwa ni ishu pana na haishii kwenye 2×3 tu.

Pharmacist lazima ajue habari ya mgonjwa A TO Z ili aweze kudispense hiyo dawa iliyoandikwa, lazima a- review vitu vingi kama medical history,medication history,drug alergies n.k ili abaini contraindications, polypharmacy, incorrect indication,drug interactions, compliance na mambo mengine ambayo yatafanya afanye maamuzi ya mwisho kama ni kumpa dawa kama ilivyoandikwa au awasiliane na daktari ili kubadilisha dawa, kupunguza dawa, dose adjustment, kuongeza dawa n.k.

Kinachofanya wafamasia hapa wapingane na maboko ni vile ambavyo yeye kama profesa hajui mipaka ya kazi yake. Pia hajui ni kwanini program ya ADDO ilianzishwa na kwanini wafamasia wanapinga. sidhani hata kama anajua ni dawa gani hasa zinaruhusiwa kwenye ADDO na zipi ni prescription only na zipi hazihitaji cheti. Angejua wala hata asingeng'ngania maana ni dawa chache sana zinaruhusiwa kwenye ADDO

Watanzania wengi hawajui majukumu ya pharmacist na ndio maana hata wewe umeuliza swali ambalo linaonyesha ni jinsi gani hujui kitu kuhusu pharmacy. Nadhani kwa haya machache umepata mwanga, Google upate mwanga zaidi.
 
Nimetembea mikoa mingi, nishafanya biashara ya pharmacy mikoa kadhaa, wote wanafanana. Ni kama polisi, popote utakapoenda Tanzania, polisi wote wanafanana. Ni kama watoto wa baba mmoja, si mwanaume si mwanamke. Usije kuwaamini hata kama ni watoto wako. Mwanao akiwa polisi, usimwamini sana tena. Ndio maana watoto wangu hawatakuja kuwa polisi, kamwe. Bora awe mwanajeshi.

Tukija kwenye mada, namfahamu mfamasia mmoja, tena yule amesoma kwa kuungaunga tu. Mme wake ni mchungaji, yeye ni mama mchungaji. Baada ya mwenzake kufumuliwa na kuondolewa mkoa huo, watu tukasema mama mchungaji amekuja labda hatahitaji rushwa. Ndani ya miezi kadhaa, shetani kamuingia, na sasa tunamtafutia tu zengwe aondolewe. Ni mla rushwa na muonezi balaa.
 
kwa hayo uliyoandika, kazi ya doctor ni nini sasa? na kuna umuhimu gani kwenda na cheti cha doctor eneo la kuchukulia dawa? daktari ameshafanya kila kitu na kuelekeza apewe dawa hii na hii, kwa mfamasia unaenda na kikaratasi, anaangalia, hata muda kuongea au kukuuliza unaumwa nini, tangu lini n.k, yeye ni kuchukua dawa, kuandika matumizi na kukupatia. kitu pekee anachoongea na wewe ni, " dawa hizi tumia hivi mara hivi...n.k" nothing more. kama tungekuwa tunaenda kuelezea matatizo yetu kwa mfamasia kusingeuwa na umuhimu wa kwenda kwa daktari. msituchanganye.
 
Ni vile tu watu wanarahisisha kazi lakini principles of pharmaceutical care hutakiwi kudispense dawa bila kujua inatumika kwa ajili ya nini. Kuna muda madaktari wanakosea kuandika dawa kwa kujisahau tu na wakati mwingine ni kwa kuwa hawana ujuzi mkubwa wa dawa na mtu wa kusahihisha ni mfamasia. Unaposema daktari kamaliza kila kitu unakua unakosea, pharmacy ndio sehemu ya mwisho kabisa mgonjwa anapitia kabla ya kuondoka na kama mfamasia hatakua competent kugundua shida yoyote basi mgonjwa ataondoka nayo.
 
Naungana na Dr.
Kama Dr ndiye anayekuandikia dawa gani itakufaa, basi kwenda kwa pharmasist ni ukilitimba na kupoteza muda au kutumia vibaya rasilimali.
Yaani m pharmasia yuko hapo kusubiri Dr aandike mpe mgonjwa dawa hizi? Kwanini asimpe moja kwa moja?

Waende viwandani wazalishe dawa. Ova
 
Tuna la kujifunza kutoka kwa dr
1.Anayo yasema ni uongo au sikweli?
2.Majukumu ya mfamasia ni yapi?hapa nauliza kwa ngazi ya hospitali
3.Huu utatu wa daktari,mfamasia na muuguzi unassembled kuhusu sheria ya usimamizi wa dawa na sumu?
 
Soma hii job description utapata kitu.

We are therefore seeking enthusiastic and qualified experienced personnel for the following positions for The Aga Khan Hospital Mwanza:

PHARMACIST – (1 POSITION)

JOB RESPONSIBILITIES

Verify billing, filling and dispensing of drugs to in and out patients are done in the right, orderly and timely manner.
Answer drug information queries from doctors, junior staffs and patients.
Identify, intervene and correct medication errors.
Train and educate juniors on current good pharmacy practices and hospital policies
Takes inventory of prescription and over-the-counter medications and other pharmaceutical products and records results and check of expiry dates on medicines.
Responds to patients’ questions about medications as well as communicating with prescribers about patients and medications
Independently profile and process Oncology CPOE
Admixture sterile products under aseptic techniques
Prepare store indents and to ensure drugs availability & storage in the pharmacy
Any other roles assigned by the Supervisor.
 
Sikia usipende underestimate watu kisa upo apo bila kujua jf ni kisima kilichojaa wabobezi wa Mambo mengi

Haya mafunzo ya ADDO ya mwezi na week 2-3 ndo yanamfanya mtu Sasa kuwa na uwezo wa kujua pharmacodynamics vs pharmacokinetics ,nimetumia terminology hizo mbili maana misingi muhim ya mtu wa pharmacy

KWa hoja za prof na hoja zako unazotoa ,ni Kwamba bado mtu anaetakiwa kujua dawa GANI mgonjwa apewe ni dr na si vinginevyo, na huwezi ilazimisha utakavyo

Hivyo bado hoja za prof inasimama kwamba
1.pharmacy lazima iwe na mfamasia na dr au nurse
2. Ni wizi na ujinga kwamba dr aksaome ADDO tena Ili kuendesha pharmacy maana bado pharmacology kaisoma pia

3. Huwezi pika watu KWa miezi miwili KWa mafunzo uchwara ya ADDO alafu ukaja na kelele kwamba Sasa wameiva katika pharmacodynamic vs pharmacokinetis ,hii ni kucheza na afya za watanzania, na ni wizi mtupu

Mwisho nimpongeze prof na naunga andiko lake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…