Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,071
- 5,457
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange amesema uchaguzi wa serikali za mitaa utazingatia ‘R-4’ za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kila chama kipate nafasi sawa.
“Uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024 utazingatia maono ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kama ambavyo tumesikia katika majukwaa mbalimbali akisisitiza “Four R” kwa maana ya Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga Upya,” Amesema Dkt. Dugange.
Dkt. Dugange ameyasema hayo Ijumaa Juni 14, 2024 Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha kupitia rasimu za kanuni za uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu.