Dharau za Tundu Lissu kwa sisi Watanzania

Kwa sasa hoja yoyote ya kumpinga Magufuli itakuwa ngumu sana kusikilizwa.
Kwa sababu upinzani wenyewe ndo uliwalisha watu sumu hii kwa Tabia yao mbaya ya kupinga mambo ya maana.
Kwa sasa hata wakiwa na hoja za msingi bado wataonekana vituko tu.
Unapingaje kwanza kabla ya kamati ya ushauri wa kisheria haijatoa findings zake?

Anachokifanya Lisu ni mind set watu waukatae ushauri wa Kamati kabla haujatoka.

Anadhoofisha utashi wa rais kwa taifa lake.
 
Nimejiuliza mpaka nakosa majibu sahihi.

Hili sakata la Mchanga wa madini ambao haujataifishwa na serikali lakini tayari mheshimiwa (shame) Lisu amesha-pre empt kuwa umetaifishwa kupitia upuuzi anauongea kila anapofungua mdomo iwe bungeni au nje ya bunge.

Najiuliza, mbona yeye ndiye kaumizwa zaidi kuliko hata mwizi mwenyewe?

Lakini najiuliza haya kwa sababu zifuatazo.
  1. Alisimama kidete kutaka hatua kama alizochukua Magufuli zichukuliwe tangu mwanzoni kabla hata hajawa mbunge (au ndiyo ametumia ule msemo wa If you can't fight them, join them?
  2. Hatua za uundwaji wa tume ya prof. Mruma aliipinga na kutoa sababu lukuki za kudhoofisha tume isifanye kazi yake
  3. Matokeo ya tafiti ya Tume ambayo ni ya wataalam wa madini tofauti na lisu ambaye ana utaalam wa kisheria tu na hajui lolote kuhusu chemicals na atoms. Anayaita matokeo hayo ni RUBBISH yaani takataka. Anasema rais anapewa takataka.
  4. Jana Bungeni anasema maamuzi ya rais ni ya kijinga na hayapaswi kuungwa mkono na anaowataka wasiyaunge mkono (wabunge) anawaambia ni illiterate hawajui lolote.
  5. Anasimama kulielezea taifa kupitia Bunge kuwa tunapaswa kuweka hands down tusikubali kupambana na wezi wa rasilimali zetu kwa sababu tutatengwa...
Haya yote na mengine yananipa mashaka kuhusu weledi na uwezo wa akili wa Lisu kwa sababu. kwa miaka kumi aliongoza kampeni nchi nzima kuwa Lowassa ni fisadi na ushahidi wanao, lakini leo baada ya fisadi kuingia katika chama cha mabepari wanamsafisha kuwa siyo fisadi bali ni msafi.
Sasa tunaambiwa mikataba ya wizxi iheshimiwe. na kama the other part ya mkataba ametenda mambo yanayokiuka msingi wa mkataba ni haki yake na achwe asiguswe.

Jamani hii GOLDEN FLEET hii ipoje?
Pole mbona umeandika kwa hasira saana....kwa uzi huu tuachie sisi wasomaji tunyambulishe kati ya wewe na Lisu nani mwenye weledi kwa maoni yenu..Duh..watu wanakurupuka...Hasira hasara...
 
Onyesha Hansard za Bunge wapi alikuwepo katika kupitisha hii mikataba mnayoitetea leo.
Humber ile kupinga mikataba mlikuwa mnatengeneza motion ili ipitishwe?
Kwa hili magufuli hawezi kwepa mana alishiriki kikamilifu sasa wewe endelea kumsafisha kwa sabuni ya lumumba nchi hi linapokuja swala la pesa hakuna mwenye uchungu wote njaa na uroho wa pesa za posho ndo umelifikisha taifa hapa
 
Mimi nina wazo tofauti.Nchi yetu imebarikiwa kuwa na wataalamu lukuki wenye weledi wa hali ya juu katika sheria.Jambo baya sana ni kuwa kwa miaka mingi wataalamu hawa waliosomeshwa kwa kodi za wavuja jasho wamekuwa si msaada kwa Nchi na watu waliowasomesha.Mikataba isiyo na tija kwa taifa na watu wake imeasainiwa wao wakiwa wasimamizi ama wakishindwa kutumia weledi wao kutoa ushauri makini.TL ni mtu tofauti,anasema wazi anachoona kina walakini,anatoa ushauri ambao watawala hawapendi kuusikia.Anatoa tahadhari pale kwenye shari!!!Anaongea bila dhihaka ili tusijekuta tumeamsha madude badala ya kutatua tatizo!!

Nyakati kama hizi "contadiction" ni muhimu kwa afya ya nchi yetu
Tundu Lisu anajua kwamba HAKUNA MTANZANIA ambaye anakuwepo kwenye grading ya Madini zaidi ya kupelekewa ripoti na hata kwenye smelter hakuna mtanzania ambaye anakuwepo hapo. Analijua hilo na hajawahi kusema wala kupigia kelele.

Najiuliza kwa nini hata baada ya kumtukana rais bado ana haha kutaka kuonana naye Ikulu? Si anamuona rais ni mjinga? basi amuache atimize wajibu wake yeye aendelee na akili zake za upepo
 
Naamini katika umri wako haujafikia nusu ya umri wangu. Sasa kama leo wewe unajiuliza maswali hayo ulipaswa kuwauliza babu zako nini kilimtokea Mrema aliposimama na kupinga hayo na leo yupo wapi na waizi wakaendelea kuiba.

Hebu niambie jana umesoma kitabu gani? maana seems hauna utamaduni wa kujisomea ndo maana unapopata wapotoshaji kama kina Tundu Lisu hauwezi kuwahoji wanapata wapi ujasiri wa kifisadi
Kama una umri mkubwa,ubarikiwe i see.
 
Kwa hili magufuli hawezi kwepa mana alishiriki kikamilifu sasa wewe endelea kumsafisha kwa sabuni ya lumumba nchi hi linapokuja swala la pesa hakuna mwenye uchungu wote njaa na uroho wa pesa za posho ndo umelifikisha taifa hapa
Toa ushauri wewe mtwana wa Lisu.
 
Sipati picha chadema wangeingia ikulu 2015 wangefanya kazi gani. Mtu anayempinga Rais katika hili APIMWE AKILI. Ikumbukwe alikuwa waziri lkn Mara flani alisikika akisema I wish I could be president maana asingeweza kudili na kitu chochote kwa ukamilifu wake wakti yuko chini ya mtu. Mimi nadhani waliomtangulia ndio wametufikisha hapa na sasa anajaribu kuitengeneza upya Tanzania na namshukuru hasikilizi upuuzi huu mnaousema mitandaoni maana anawajua baadhi ya watanzania walivyo wapumbavu. Bnafsi Namuombea ktk vita hii. BADILIKENI NA WAKATI WATANZANIA NANI KAWALOGA?????
 
Naona mtoa Uzi ndio katoka usingizini. ,,fikicha akili yako kwanza
Soma avatar yangu mkuu. naomba unisaidie kuhusu Golden Fleet mkuu. Hii ni kampuni ila kuna tetesi huku umangani na kinachofanyika ni mind scramble ili watu wasiijadili

Sina imani na usomi wa Tundu Lisu.
 
Tundu Lisu anajua kwamba HAKUNA MTANZANIA ambaye anakuwepo kwenye grading ya Madini zaidi ya kupelekewa ripoti na hata kwenye smelter hakuna mtanzania ambaye anakuwepo hapo. Analijua hilo na hajawahi kusema wala kupigia kelele.

Najiuliza kwa nini hata baada ya kumtukana rais bado ana haha kutaka kuonana naye Ikulu? Si anamuona rais ni mjinga? basi amuache atimize wajibu wake yeye aendelee na akili zake za upepo

Nampongeza kwa jitihada zake za kutaka kuonana na Mkulu,huenda ana jambo muhimu anataka kumtonya moja kwa moja.Huuu pia ni uzalendo.Kumbuka Tanzania ni ya Watanzania wote hata mimi na wewe,hata Mzee Mkomigumunyo kule kijijini kwetu.
 
Acha tu atudharau tunastahili kabisa kwa mihemko yetu kisiasa. Tulithamini chama tukafanywa vipofu tukawa tunapiga makofi bila kufikiri. Lissu anaona mbali siyo kama kina Change wana elimu lakini hawaoni. Siasa hapo Lissu akitutukana kosaclipo wapi
 
Nampongeza kwa jitihada zake za kutaka kuonana na Mkulu,huenda ana jambo muhimu anataka kumtonya moja kwa moja.Huuu pia ni uzalendo.Kumbuka Tanzania ni ya Watanzania wote hata mimi na wewe,hata Mzee Mkomigumunyo kule kijijini kwetu.
Mpongeze kwa juhudi hizo na kumtukana rais pia...

Mtaalam wa mchanga wa madini ndugu Lisu ana nini la kumshauri rais zaidi ya alichosema Bungeni kuwa ana maamuzi ya kijinga?

Jamani ni kweli kabisa tumefikia kumdharau mkuu wa nchi kiasi hiko? Hapana aisee namsihi magufuli asitume hata msaidizi wake kuonana na traitor.
 
Kwa hili nakuapia. Watanzania tumevaa Mkenge. Na Tutajuta. Tumekurupuka. Na Tutakoma, Naiona Tanzania ikigeuka Zimbabwe soon.
Nenda kaishi Canada mkuu.
Tuachie tuijenge nchi yetu kwa vizazi vijavvyo
 
Sitaki kuamini kuwa hatima yako imefikia hapo.
Yaani uwezo wa kuchambua na kuhoji umeshapukutika sasa unaishi kwa kila neno litokalo kinywani kwa Lisu
Yaelekea jamaa yetu unajiona kama una hojaaaa, na una akili sanaaaaaaa.

Kabla ya yote, acha nikuambie kitu kimoja: Tundu Lissu sio saizi yako. Unaweza tu kumjadili, lakini kamwe huwezi kujadiliana naye. Hiki ni kidokezo tu, turudi kwenye mada.

Hakuna anayesema kuwa HATUIBIWI. Shida iliyopo ni:
1. Tunafahamu kwa nini tunaibiwa?
2. Nani alifungulia wezi mlango?
3. Njia tunayotumia kukabiliana na mwizi ni sahihi?
4. Sheria inatoa ruhusa ya kumuua mwizi au inatutaka tumpeleke mbele ya sheria?

Mimi nitakupa mfano mdogo sana wa mgomo wa matumizi ya akili. Bwana ABC kaenda manispaa kuomba ardhi ajenge Fuel Station. Mtumishi mmoja wa Manispaa mwenye dhamana ya kuidhinisha matumizi ya ardhi kamuidhinishia Mr ABC ujenzi wa fuel station kwenye hifadhi ya barabara.

Ikiwa leo imebainika kuwa Mr ABC kajenga kwenye hifadhi ya barabara, unadhani busara ni kumshambulia Mr ABC kwa kubomoa Fuel Station yake ilhali ni kitengo katika mamlaka hiyo hiyo ndio kilimuidhinishia ajenge hapo? Jijibu mwenyewe.

Bwana Msanii, akili ni nzuri ukiwa nayo. Haya ni matokeo ya 'Timu Ndioooooo' huko bungeni na mfumo wa Uwanja Wetu na Refa ni wetu. Wapinzani walihoji haya, yakaitwa siri na mambo mengi yakapitishwa kwa hati ya dharura. Hapa tunatokwa na povu madini, kumbuka kuna GESI na sasa Bombadier nazo zimenunuliwa kimvulini. Kwa sasa tunashangilia, likibuka lenye mzozo ndio tunaanza kuoneshwa parts of the articles na kuombwa kuwa wazalendo.
 
Acha tu atudharau tunastahili kabisa kwa mihemko yetu kisiasa. Tulithamini chama tukafanywa vipofu tukawa tunapiga makofi bila kufikiri. Lissu anaona mbali siyo kama kina Change wana elimu lakini hawaoni. Siasa hapo Lissu akitutukana kosaclipo wapi
Acha akudharau wewe mkuu.
Nilipinga mikataba na sasa sipingi hatua zinazoanza kuchukuliwa
 
Walio sababisha taifa tuingie hasara kwa mikataba mibovu wote mahakamani na kuanzia leo mikataba yote iwe wazi.
Naam hapo mkuu umenena.
Waliotuingiza mkenge huu wachukuliwe hatua
 
Back
Top Bottom