Dhana ya Kutofumua Makaburi

Mkuu umesha wasahau UKAWA? Wao kazi yao ni kubadilisha maneno ili wapate agenda ya kuzungumza! Kama wameweza kubadili gia angani, watashindwaje kubadilisha maneno ya JPM ili wapate tu sababu ya kukosoa!
Sio kila mtu anayekosoa baadhi ya vitendo vya JPJM ni Mwana-UKAWA!
 
Kama siyo ushabiki, basi kauli hiyo umeielewa ndivyo sivyo. JPM alikuwa anawaeleza wana CCM wenzake kuwa waache kufitiniana kwa kigezo cha kusalitiana wakati wa uchaguzi. Kwamba hatabagua mwana CCM yeyote (wakati wa kuteua) kwa kigezo cha kuwa mhusika aliwasaliti wakati wa uchaguzi. hiyo ndiyo dhana ya rais ya kutofukua Makaburi. Tusipotoshe.

Hapo nimekuelewa mkuu, nilianza kufikiria vibaya kuhusu dhamira yake
 
Aisee wapinzani mnatishaaaa. Kila analotamka Magu kwenu ni ajenda
Wewe hujui kuwa kila analosema ni kama sheria? Yeye ni Rais hivyo anapaswa kufikiri kabla ya kusema, na ndio maana Ikulu kumejaa washauri kibao tunawalipa kwa kazi hiyo ya kumshauri aseme nini.
Sasa kama yeye anafikiri ni mbunge wa chato anaweza kusema lolote shauri yake!
 
Wewe hujui kuwa kila analosema ni kama sheria? Yeye ni Rais hivyo anapaswa kufikiri kabla ya kusema, na ndio maana Ikulu kumejaa washauri kibao tunawalipa kwa kazi hiyo ya kumshauri aseme nini.
Sasa kama yeye anafikiri ni mbunge wa chato anaweza kusema lolote shauri yake!
"Kama" Sheria, right?
 
Kwenye Kampeni ndio majipu yanaruhusiwa?

Siyo majipu mkuu, hapa ni misuguano ya kimakundi ndani ya chama chao CCM kipindi cha campain. Kwamba wasifikirie kuna kulipa visasi, hayo yamepita. Ni sawa na yamekufa na hatufukui makaburi, tunaendelea mbele. Usiangalie sana upande mmoja, jaribu kuwa neutral na flexible ili usibaki au usifungwe na itikadi za vyama.
 
Siyo majipu mkuu, hapa ni misuguano ya kimakundi ndani ya chama chao CCM kipindi cha campain. Kwamba wasifikirie kuna kulipa visasi, hayo yamepita. Ni sawa na yamekufa na hatufukui makaburi, tunaendelea mbele. Usiangalie sana upande mmoja, jaribu kuwa neutral na flexible ili usibaki katika mlengo wa itikadi za vyama.
Kwa akili yako unafikiri kwenye Kampeni kulikuwa na "misuguano" tu basi? Na hao waliofanya nchi kuwa "shamba la bibi" sio wa kutoka Chama chake ambao ni wanasiasa? Kwa kifupi chama kiko clean, right?
 
Back
Top Bottom